muvika online
JF-Expert Member
- Nov 27, 2016
- 374
- 283
Makampuni mengi yanazidi kuwekeza katika teknolojia za magari rafiki wa mazingira. Toyota inazidi kuwekeza pia na inategemea moja ya gari zuri na la kisasa zaidi kutoka kwao la Toyota Prius PHV litafanya vizuri sana sokoni.
Gari la Toyota Prius PHV limeingia sokoni wiki hii nchini Japani, kwa nchini Marekani gari hilo linauzwa kwa jina la Prius Prime na lilianza kuuzwa mwishoni mwa mwaka jana.
Toyota Prius PHV ni gari lenye uwezo wa kutumia mafuta na pia umeme wa kuchaji. Kati ya teknolojia bora za kipekee kwa gari hilo ni pamoja na uwezo wa mtumiaji kuweza kulichaji kwa kutumia umeme wa nyumbani tuu, hii ni tofauti na magari ya umeme kutoka kampuni ya Tesla ambayo yanaitaji kuchajiwa kwenye vituo vyao spesheli.
Toyota wanategemea kuuza zaidi ya magari 2,500 kwa mwezi ya toleo la Prious PHV nchini Japani, gari hilo litaanza kupatikana katika masoko mengine duniani kote
Dereva anaweza kuendesha hadi umbali wa kilometa 68.2 kwa kutumia umeme wa betri la gari hilo, hii ni takribani mara tano zaidi ukilinganisha na toleo la zamani la gari hilo (lilikuwa na uwezo wa kwenda umbali wa km 26.4).
Pia kingine kikubwa ni kwamba gari hilo linachukua muda mchache kujaa chaji – takribani masaa 2 na dakika 20 kujaa kwenye chanzo cha umeme wa volti 200, wakati kwenye chanzo cha umeme wa volti 100 itachukua masaa 14.
Ila kama ukitumia mashine yake spesheli ya kuchajia kiwango cha chaji kitaongezeka kutoka 0 hadi asilimia 80 ndani ya dakika 200 tuu.
Toyota wanaamini hadi kufikia mwaka 2050 asilimia kubwa ya magari yatakayokuwa barabarani yatakuwa yanatumia teknolojia flani rafiki kwa mazingira.