Mkuu mtazamaji,
Ni wazo zuri sana hilo lakini Metropolitan Police ni taasisi kubwa sana na ndio maana unaona kuna mambo mengi mno.
Kuna thread moja nilizungumzia kuhusu uundwaji upya kwa jeshi letu la polisi na nilitoa baadhi ya mapendekezo nafikiri ni mbali mno (si unafahamu tena sisi watu wa siku nyingi hapa JF?)
Met police ni kama wizara nzima na wana kamishna na ambae ndio kama IGP wetu, halafu ana assistant wake na pia anatawala jeshi la police la London au City of London Police, kwahio tovuti yake inabeba mambo mengi sana.
Baada ya hapo kuna vikosi vya polisi nchi nzima vikiongozwa na chief constables ambao ni kama RPC wetu. Ukitoka hapo unakuja kwenye taasisi zingine kama vile chama cha maofisa wa polisi ambao wana asili ya Afrika na Asia.
Halafu kuna idara shiriki au partners kama vile fire brigade, ambulance service na fire brigade. Baada ya hapo unakuta kuna taasisi za kimataifa ambazo zinashirikiana na met police kama vile CIA, Interpol, FBI na internationall police association.
Sasa mwenye jukumu la kuandaa website ya jeshi la polisi la anatakiwa awe amepewa blue print yenye maana yaani iliyojaa mambo mengi ambayo yamesheheni elimu msaada kwa wasomaji na mambo mengi tu, ili siku ikiwa tested online watu tuseme alaa kumbe!
Lakini mtu hawezi kukurupuka na kuja na tovuti kama hii ambayo ni ya mtoto wa sekondary anaejifunza kutengeneza tovuti. Tumefika miaka 50 ya uhuru halafu ndio mtu anakuja na hii tovuti yaani ni mambo ya ajabu kabisa.