permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 10,027
- 11,222
Spurs walicheza mchezo mzuri, shida ya umaliziaji bado ipo, defence inamatatizo bado hasa kutokana na full backs kucheza kama mawinger.Come On You Spurs.
Jana tumepokea kipigo nyumbani. Timu iliweza kutengeneza nafasi ila defense ikaendelea kuwa uchochoro.
Ni dhahili sasa ndoto za top four zinazidi kufifia. Ngoja tusubiri tuone.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kikosi siyo bora. Kukosekana kwa wachezaji watatu muhimu KANE, SON na SISSOKO kunaiathiri timu

Bergwijn ni majeruhi. Pia Delle Alli na Moura ndiyo pekee wanaweza cheza kama target men angalau. Kwa kasi ya RB Leipzig huwezi mchezesha Ndombele mwenye mwendo wa kobe.Ubora ni depth ya squad inayompa different options kama akiamua kubadili mfumo.
Kwanini Asicheze 4 3 2 1
Lamela akiwa kama target man halafu Geovani/ Bergwijn na Lucas Moura/Delle Ali wakacheza nyuma yake, hao watatu Harry Winks Tanguy Ndombele na Gedson Fernandez.?
Au akacheza 4 4 2 diamond akamtumia Lamela tena kama target man ?
Sent using Jamii Forums mobile app
Bergwijn ni majeruhi. Pia Delle Alli na Moura ndiyo pekee wanaweza cheza kama target men angalau. Kwa kasi ya RB Leipzig huwezi mchezesha Ndombele mwenye mwendo wa kobe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Lamela amewahi kucheza kama target man enzi hizo Harry Kane hajawa wamoto sana.
Delle Alli na Lucas Moura hawawezi kuwa target man cause they are typical mobile wingers na hawana instincts za striker.
Lamela ana insticts za Striker na ni mrefu you can count on his aerial qualities.
Ana art ya uchezaji ambayo ni ideal kwa Strikers.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye hoja ya ugomvi nakubaliana na wewe ingawaje tuliona hata akina Furgerson wakiwapiga wachezaji viatu vya kichwani, lakini pia Mou hata mchezaji akifanya vizuri humsifia hadharani pia.HALI si hali kwa Jose Mourinho tangu atue Tottenham Hotspur mambo yanazidi kumwendea kombo, badala ya kuiinua miamba hiyo ya London Kaskazini anazidi kuizamisha.
Katika mechi sita zilizopita amepigwa kwenye mechi tano, timu imetolewa katika Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu inazidi kuwa ndoto kwao, lakini je, ni wapi kocha huyu wa Kireno amekosea tangu atue Spurs? Makosa yake haya hapa.
1. Ugomvi wake na Tanguy Ndombele
Kwani kuna mtu hajui kama Mourinho anapenda ugomvi? Kama hujui habari ndiyo hiyo, kila sehemu anayoenda lazima azinguane na wachezaji wake. Inawezekana mwenyewe anaamini hiyo ni njia sahihi ya kuwafanya kuwa bora na kuthibitisha utawala wake, huwezi kujua. Pale Spurs tayari ameshamzingua mtu, Tanguy Ndombele ameingia kwenye orodha yenye watu kama kina Luke Shaw, Paul Pogba, Iker Casillas na Joe Cole kama mmoja kati ya watu waliowahi kuuona ubaya wa Mreno huyo.
Ni ajabu, ukiacha tu kwamba haipendezi kumponda mchezaji wako hadharani, lakini inakera zaidi unapomponda mchezaji ambaye amesajiliwa kwa dau la rekodi na klabu. Usajili wa Ndombele wa Pauni 62 milioni ndiyo unashikilia rekodi pale Spurs.
Sawa, amekuwa na majeraha ya mara kwa mara, lakini kila anapocheza amekuwa mchezaji bora kwenye kikosi cha Spurs. Inawezekana ni kweli kuwa Ndombele hayuko sawa sana, lakini ni jukumu la kocha kumrudisha vizuri na si kumtukana.
Lakini, Mourinho badala ya kumsaidia mchezaji wake mwenye kipaji zaidi kaamua kumzingua - tena kamzingua sana na hili ni kosa kubwa hasa kwa wachezaji wa kileo ambao ukiwazingua kidogo tu wanaacha kujitolea matokeo yake kocha anaharibikiwa.
2. Anakosea kumtumia Dele Alli
Dele Alli amefunga mabao manne katika mechi nne za kwanza chini ya Mourinho pale Spurs. Straika huyo alionekana kama amezaliwa upya kwa sababu takwimu zake zilianza kuzungumza.
Lakini, sasa mambo yamebadilika baada ya Spurs kukumbwa na majerahi wengi, ameamua kumtoa Delle kutoka nafasi ya straika wa pili ambayo amekuwa akifanya vizuri na kumsogeza mbele acheze kama mshambuliaji kamili.
Kilichopo, Delle anachukia sana kucheza kama straika, anapenda kucheza nyuma ya mshambuliaji, yeye aina yake ya soka haina tofauti sana na Thomas Muller, lakini kwa bahati mbaya Mourinho kaamua kumchezesha mbele zaidi.
Delle anaweza kuipa Spurs mabao, lakini ili kufanya hivyo anatakiwa kurudi kwenye nafasi anayoimudu zaidi, kitendo cha Mourinho kuendelea kumkomalia asimame mbele kabisa ni kosa lingine ambalo linamtafuna.
3. Ishu ya golini
Mourinho alipopewa jukumu la kuinoa Spurs kipa namba moja Hugo Lloris alikuwa majeruhi, hivyo Paulo Gazzaniga akakaa golini. Lloris alipokuwa fiti alirudishwa tena golini, safi sana. Lakini shida ikaanza hapa.
Lloris aliumia nyonga na kukosa mechi kadhaa. Wakati huu Gazzaniga alikuwa fiti, hivyo alitakiwa kurudi golini, lakini Mourinho akaamua kumrudisha kikosini Michel Vorm. Vorm hakuwa amecheza kwa miezi 18 wakati Mourinho alipompa nafasi, matokeo yake alitoa boko kwenye mechi dhidi ya Norwich na kuipa timu hiyo bao la kusawazisha kabla ya mechi kwenda matuta na Spurs kutolewa kwa mikwaju ya penalti katika Kombe la FA.
Mechi iliyofuata akamrudisha golini Lloris ambaye hakuwa fiti vya kutosha badala ya kumpa nafasi Paulo Gazzaniga, kilichotokea sasa Lloris aliruhusu bao la kizembe dhidi ya Burnley, mechi iliyofuta aliiruhusu RB Leipzig kufunga mabao mawili. Kama Mourinho angempa nafasi Gazzaniga ni wazi kuwa alikuwa kwenye kiwango bora kuliko wale makipa wawili ambao yeye aliwakimbilia kwenye Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
4. Kumbania Troy Parrott
Mwenyewe akiiangalia safu yake ya ushambuliaji anadai kuwa ni sawa na kwenda kwenye vita na bunduki bila risasi, hii ni kwa sababu Harry Kane na Son Heung-Min ni majeruhi na hao ndiyo wafungaji wakubwa wa mabao ya Spurs.
Mourinho amejaribu kuziba mapengo yao kwa
kuwatumia Lucas Moura na Delle akiamini lolote linaweza kutokea, lakini kosa kubwa analofanya ni kumnyima nafasi Troy Parrott, ambaye ni straika wa asili ambaye yuko kwenye kikosi cha vijana cha timu hiyo ambacho ni zao la Spurs.
Inashangaza kuona Mourinho kila siku analia na kukosa watu kwenye safu yake ya ushambuliaji, wakati hataki kumtumia mtu mmoja ambaye ni straika wa asili aliyefiti katika kikosi chake. Parrott amefunga mabao matatu katika mechi mbili alizoanza akiwa na kikosi cha Spurs chini ya miaka 23 na mabao sita katika mechi nne za michuano ya vijana ya UEFA.
Kumtumia Parrott si tu kutamsaidia kwa sababu dogo anajua, lakini pia kutatoa nafasi kwa Delle kurudi kwenye nafasi yake ya mshambuliaji wa pili ambayo huwa anafanya vizuri zaidi.
5. Anapoteza asili yake
Mourinho alikuwa mpambanaji kwenye, siku zote ilijulikana kuwa timu yake lazima itakuwa na ukuta wa chuma. Si unakumbuka enzi zile yuko Chelsea, kikosi chake kiliweka rekodi ya kufungwa mabao machache zaidi katika Ligi Kuu England (15).
Lakini, sasa amebadilika kikosi chake cha Spurs kina ukuta dhaifu, kinaruhusu sana mabao chini yake kimesharuhusu mabao 23 na hadi sasa kimecheza mechi tatu tu bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
Ukizitazama takwimu hizi unaweza kujikuta ukijiuliza kuwa huyu ni Mourinho kwenye au mfano wake? Maana inashangaza, sawa timu yake haifungi, lakini hata kuzuia kunamshinda, na hili ni kosa hasa kwa kocha ambayo amezoea kushinda idadi ndogo ya mabao.
Miaka ya nyuma alifanikiwa kwa sababu hata alipokufunga bao moja ilikuwa ngumu sana kugusa nyavu zake, lakini pale Spurs watu wanajipigia tu, hivyo kama anataka kurudisha ufalme wake kwanza arudi katika asili yake ya kutengeneza timu yenye ukuta wa chuma ambayo inaweza kujilinda hata kama inashambuliwa kwa dakika 120.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui kama unafuatilia vema mwenendo wa Spurs. Lakini kwa kifupi ni kuwa yeyote anayejua mpira asingempanga Delle Alli namba 10 na kumwacha nje Lo Celso.HALI si hali kwa Jose Mourinho tangu atue Tottenham Hotspur mambo yanazidi kumwendea kombo, badala ya kuiinua miamba hiyo ya London Kaskazini anazidi kuizamisha.

Siyo mbaya. Kipi bora? Kushiriki UCL na kuishia fainali au kushiriki UEL na kulibeba? Mafanikio hupimwa kwa vikombe na si idadi ya fainali ulizocheza.