TOT Bonanza 2020

TOT Bonanza 2020

thA goD

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
1,943
Reaction score
1,857
Habari,

Wakuu leo ilikuwa bonanza watanzania wanaotumia twitter yaani Tanzanians on Twitter. Nilifanikiwa kuhudhuria na kujifunza mambo kadha wa kadha. Kubwa katika hili Bonanza ni kuimarisha Upendo mitandaoni lakini pia kupanua wigo wa kuchangamana.

Ni dhima ya post hii? Naam, nashawishika sisi kama jamii inayotumia JAMII FORUMS mnaonaje kama tutaamua nasisi kama Great Thinkers tukaja na kitu cha namna hiyo lakini kwa utofauti na upekee wa aina yake?

Mitandao ya kijamii leo hii imekuwa ni sehemu ya aina ya Ulimwengu ambao unegubikwa na kila aina ya fursa kwa mwenye jicho la kuchungulia fursa. Wazo langu hili laweza kufungua milango zaidi kwa vijana wengi ambao leo hii yamkini tayari wameshajikatia tamaa ya maisha.

Nakaribisha michango yenu Wakuu.
Wasalaam[emoji120]
 
Back
Top Bottom