Tosamaganga Sekondari kwachafuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tosamaganga Sekondari kwachafuka

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KIMBURU, May 30, 2011.

 1. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  HALI ya usalama kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Tosamaganga wilayani Iringa mkoani hapa leo ilikuwa tete baada ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia kulazimika kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya wanafunzi zaidi ya 1000 wa shule hiyo ambao walikuwa katika maandamano ya amani kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya uongozi wa shule hiyo.
  Pamoja na askari hao kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao kama njia ya kuwazuia wasiandamane bado waandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo wakichukua madai ya wanafunzi hao walizuiwa na polisi hao kuendelea kuchukua habari za wanafunzi hao pasipo kibali cha polisi huku wananchi wa maeneo ya Mseke wakizihama nyumba zao kwa muda na kukimbilia porini kukwepa mabomu hayo.
  Tukio la mapambano kati ya FFU na wanafunzi hao lilianza majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana kwa polisi kufukuzana na wanafunzi hao kuwarudisha kwa mabomu shuleni pasipo mafanikio baada ya idadi kubwa ya wanafunzi kukimbilia porini na wengi wao kujificha porini na katika nyumba za wenyeji wa maeneo hayo.
  Kabla ya polisi kufika na kuwatawanya wanafunzi hao waliwaeleza waandishi wa habari kuwa sababu ya wao kufanya mgomo wa kutoingia madarasani na kutaka kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Iringa umetokana na uongozi mbovu wa shule hiyo usiozingatia haki za binadamu.
  Waliyataka madai hayo yao kuwa ni pamoja na mfumo wa ufundishaji kutofuata taratibu na kanuni za ualimu ,pia ukosefu wa vitendea kazi kama madawati na vitabu , makamu mkuu wa shule hiyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kujinufaisha binafasi badala ya kusaidia kukuza kiwango cha elimu na kuwa amekuwa akidhalilisha wanafunzi kwa kuwapekua simu hadharani hadi kanisani .
  Waliwataja walimu wengine zaidi ya 6 wakiwemo wa kike (majina tunayo) ambao wamekuwa wakiwadharirisha kwa kuwapekua sehemu za siri hadharani na kupokonya simu zao kwa faida yao .
  Aidha walidai kuwa chakula wanacholishwa shuleni hapo hakina ubora kama wanaoelezwa wazazi huku wakimtaka mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kutolea ufafanuzi juu ya bajeti inayotengwa shule hiyo kwa ajili ya chakula.
  Madai mengine ambayo wanafunzi hao wanapinga ni pamoja na ubadhilifu wa mali za shule pamoja na fedha zinazochangwa na wanafunzi hao .
  Walisema kuwa mfano wamekuwa wakichanga rim mbili kwa mwaka rimu zenye thamani ya shilingi 8500 kila moja ila matokeo yake uongozi wa shule hiyo umekuwa ukiziuza rim hizo kwa wafanyabiashara na kununua rim za shilingi 3500 zisizo na ubora kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi hao.
  Hata hivyo walipinga matumizi mabaya ya fedha za shule hiyo yanayofanywa na mwasibu na kuwa wana kama wanafunzi wanataka uongozi wa shule hiyo kuweka wazi matumizi ya michango yao mbali mbali ambayo wamekuwa wakichangia .
  “Tunatoa pia kujua kuhusu Fund ya wasomi waliosoma hapa Tosamaganga inatumikeje na leo tunaiomba wizara ya elimu ,mkuu wa mkoa wa Iringa ,mkuu wa wilaya ,mkurugenzi na afisa elimu kufika shuleni hapa na kuja kusikia kilio chetu wanafunzi”
  Mwandishi wa habari hizi alishuhudia askari polisi hao wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) wakikabiliana na wanafunzi .
  Hata hivyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi aligoma kutoa ushirikiano wowote kwa madai kuwa vyombo vya habari vimeripoti sivyo habari za kutekwa magari juu milima ya Kitonga.Mkuu wa shule hiyo hakuweza kupatikana kuzungumzia madai ya wanafunzi hao kutokana na vikao mbali mbalina vyombo vya dola ambavyo vilikuwa vikiendelea shuleni hapo. IMG_9564.JPG IMG_9577.JPG IMG_9577.JPG IMG_9577.JPG

   

  Attached Files:

 2. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  HAYO NDIO mAMBO ,POLICE WATANZANIA SIJUI WAPO SAYARI GANI NA VIONGOZI WAO MASKINI ,BADO WANATUMIA MBINU ZA KIZAMANI KWANI TOKA LINI POLICE WAMEPEWA MAMLAKA YA VIBALI VYA WAANDISHI WA HABARI,KILA SIKU POLICE POLICE ,,,,,,,,, TOO MUCH KUPATA HABARI NI HAKI YA RAIA
   
 3. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hongera mkuu kwa bandika lako lenye kila k2. Sasa wale jamaa wa kudai sources watasemaje sasa? Labda watasema saa ngapi hlo tukio limetokea?
  ny hao wanafunzi watatuliwe kile wanachodai, hv hao polc hawana watoto ama ndugu wanaosoma hapo? Yaani wao kla k2 mabomu.
  swain zao!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hapa sielewi ilikuwaje sweta na viatu vikabaki porini...mambo ya vijana haya bana!
  View attachment 31165
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
 8. h

  hans79 JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  cdm vijana taifa la leo,choka mbaya ccm vijana taifa la kesho huo ni uroho wa madaraka wa magambaz.kuna kona gambaz n wez shule,kura,pembejeo,uwezeshaj hewa madin,vipolis ua raia,ahad hewa,safar fek,semina posho fek etc
   
 9. K

  Kalila JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahaha boys nimesoma hapo huwa inatokea kipindi hamna pesa then walimu wanawazingua na hizo fujo haziishi hadi solution ipatikane polisi wanatumia nguvu sana hata kwa wananchi dah viva boys washakunywa uji wa malata hapo
   
 10. Z

  Zempugwa Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na huo ndo uelewa wa polisi wetu.kweli nimekubali ya roma kwamba kimbilio la walioferi ni polisi na ualimu.vyombo vya habar vipo kutuhabarisha kwa nini polisi wazuie?.nazani walizuia kukumbatia uovu walionao viongozi wao
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Watasema wametumwa na CHADEMA
   
 12. daudthefarmer

  daudthefarmer JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2017
  Joined: Apr 30, 2016
  Messages: 3,449
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Sitakaa nisahau hii siku maishani mwangu.
  Sauti ya umoja ndo ilikuwa kauli mbiu.
  Ukiuliuzwa na polisi kwa nini mnaandamana unasema ni sauti ya umoja.
   
 13. nsharighe

  nsharighe JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 643
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 80
  Ukiwa msomi lazima consciousness uwe nayo, migomo na maandamano ni njia ya kuonesha hisia zako..

  70% ya watanzania ni waoga na wengi elimu hawana na ndio maana hawanhawana uthubutu Wa kuhoji, kukodoa na kudai haki zao za kimsingi..
  Wengi wanapenda umbea na udaku... Mambo ya Msingi hawaweki mijadala ila maswala ya mabango ya mtaa Wa Voctor Wanyama ndio wanapenda..

  Mungu saidia Tanzania
   
 14. l

  lutataza JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2017
  Joined: Jun 14, 2016
  Messages: 730
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  Kwani mkuu wa mkoa kazi yake nini.
  Si angewafuata hao watoto na kuwasikiliza point zao.
  Atumbuliwe hajui anacho fanya
   
 15. bro kay

  bro kay JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2017
  Joined: Sep 5, 2016
  Messages: 238
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Mkuu hilo bandiko sio la leo, huyo unaesema atumbuliwe hayupo tena madarakani
   
Loading...