cbandiho
Member
- Sep 2, 2012
- 67
- 47
Kwa maoni yangu,wagombea wafuatao ni hatari kwa uhai wa ccm,kama miongoni mwa hawa atapitishwa kupeperusha bendera ya ccm,kuna hatar kubwa ya ccm kupoteza urais.
1. Lowassa- Ana kashifa kubwa ya ufisadi wagombea wote wanamnanga kama fisadi,ana makundi(mtandao) ambao ni hatari kwa chama,CCM watatumia nguvu nyingi kujibu hoja dhidi yake (hasafishiki kwa urahisi)
2.Sitta- Kapoteza mvuto hasa baada ya kupuuza maoni ya wananchi kwenye mchakato wa katiba,ana mtandao ingawa umeishiwa nguvu,anaonekana mnafiki na akipitishwa team Lowassa itajitenga naye.
3.Mwakyembe- Huyu naye hana mvuto kwa sasa,kuna kashifa ya bandari inamuandama,yeye na Sitta wanashabiiana katika mienendo yao.
4.Membe- Ana mtandao pia ambao ni hasimu wa mtandao wa Lowassa,anaonekana hana uwezo wa kuwabana mafisadi,hana mvuto sana.
5.Fredrick Sumaye- Hana kashifa nyingi lkn amejiapiza kutoshorikiana na mafisadi,hatari kubwa kwa CCM ni kuogopa mpasuko na kushughulikiwa baadhi ya viongozi mafisadi,lakini hana mvuto sana.
Kwa ujumla CCM ina wakati mgumu,karata itakayocheza ikikosea itakuwa ni turufu nzuri kwa ukawa,kwa hali ilivo naipatia turufu UKAWA kuchukua nchi kwani naiman CCM imeshapoteza ushindi mpaka sasa.