Toothless TAKUKURU: Uchaguzi UVCCM watawaliwa na rushwa na vurugu

Breaking News
Uchaguzi wa UVCCM unaoendelea huko Dodoma umetawala vimbwanga watu wanatoa Rushwa kama ni agizo la chama!!Vijana wa vigogo wamemwaga mshiko sana na hawaogopi Takukuru!!!

CCM ni chama cha kifisadi si chama cha wafanyakazi na wakulima tena! Hawawezi kuogopa takukuru kwa sababu takukuru si taasisi huru, ni taasisi yao
 
Mafisadi watarajiwa hao leo wanachaguliwa kwa rushwa yani hii nchi imeshauzwa na rais yupo kimya
Mbona nimeangalia ITV usiku huu na nimemsikia JK akikemea rushwa na kuwataka wasikubali kununuliwa? Na isitoshe, vijana pia walipohojiwa na waandishi wa Habari walisema hakuna rushwa wala makundi. Hii ni kumaanisha walikuwa wanatupiga changa la macho?
 
Mambo mengine hata kama ni mabaya Mungu anaweza kuyaruhusu kwa mfano kama naye ameamua CCM sasa ni basi. Watakaopita kwa Rushwa maana yake hawatakuwa na hoja nzuri mwaka 2015 za kuwashawishi wananchi na hatima yake ni kushindwa uchauzi. Hawataweza kuhonga nchi nzima.
 
Dr.Hosea alishasema "anaogopea usalama wake baada ya wimbi la Richmond" Sofia Simba alikuwa Boss wa hao makachero, mtandao hawaogopi vidagaaa, kwani mapapa yote ni ya kwao
 
This is very true. Chaguzi zote za ndani ya CCM zimegubikwa na rushwa ya kutisha! Sumaye alitamka hivyo siku kadhaa zilizopita. Na sasa head of State, Jakaya Kikwete, amethibitisha bila shaka yoyote kuwa, rushwa ndani ya chaguzi kwenye jumuiya zote za CCM, ikiwemo UWT na UVCCM, ni ya kutisha na inaelekea kukizika chama hicho kikongwe hapa nchini. Sasa swali dogo tu la kumuuliza JK, kama hilo analijua, wakati anajua chaguzi zote za ndani ya CCM, huwa vijana wa Hoseah huwa wanajaa, wakijidai wanadhibiti rushwa. Sasa kama hiyo TAKUKURU inashindwa kufanya kazi inayotakiwa kuufanya hadi JK analalamika badala ya kuchukua hatua ya kuivunja TAKUKURU,na kurudia chaguzi zote za jumuiya na wakati huo huo amtimue kazi Hosea,kwa kutumia bure pesa za walipa kodi! Hapo sasa JK anataka tumweleweje, wakati tunajua Hosea amemteua yeye na kama kashindwa kazi anapaswa kumfukuza kazi na wala si kulalamika kwa wananchi. Kama safari hii asipomfukuza kazi Hoseah tutajua ni maigizo ya kawaida ya CCM, ambayo yeye JK mwenyewe kama alivyoasisi kile kitu kinaitwa kujivua gamba, ambapo kila Mtanzania hivi sasa anajua gamba limeishia kiunoni na limeshindwa kuvuka!! Hivi JK ataacha lini haya maigizo yake ya kitoto? ambapo anawafanya wa-TZ wote kama ni wavivu wa kufikiri! Tunathibitisha kwa mara nyingine tena kuwa janga kuu la Taifa kwa hivi sasa ni yeye mwenyewe JK!!!!!!!

NDUGU YANGU ANAYETOA RUSHWA NI HATARI NADHANI HATA KWA RAISI MWENYEWE REJEA HOTUA ALIYOTOA HUYO RAISI WA CCM WAKATI WAMEPITISHA MAJINA YA WAGOMBEA LAKINI TUNACHOONA SASA RAISI AMEKUWA MTU ANAYELALAMIKA TUUUU SASA SIJUI alichaguliwa kulalamika tu na kusafiri ziara kibao mi nimeshindwa sana kuelewa kwanini aonyeshe udhaifu maana naona LOWASA Anamtisha na nafikia mahali kuamini hata makamanda wa TAKUKURU ni mtandao wa LOWASA maana hata 2010 walishughulikia baadhi ya watu katika kura za maoni baada ya hapo TAKUKURU Ikaenda Likizo mfano. Arusha ilimshughulikia Felix Mrema akashinda Batilida tukammalizia mbalia mbali
 
Hivi ni Baba gani mkulima atamshangaa mwanaye kuwa mkulima? Atamshangaa tu yule mtoto atakayekua mwanasayansi, si ndiyo? Tena watoto hutokea kuwa wakulima bora zaidi.
 
KAMA RUSHWA IKO OFFICIALLY "ENDORSED" WHY DO WE NEED TAKUKURU?
OBSOLETE INSTITUTIONS SHOULD BE DISBANDED FORTHWITH!
Walipa kodi kwanini wanabebeshwa mizogo isyo na faida?
 
Ili kukinusuru chama cha magamba,wangefuta matokeo ya chaguzi zao yaligubikwa na rushwa.Kwa kuyabariki matokeo yaliyogubikwa na rushwa chama kitasambaratika kabla ya 2012.
 
Tangu lini kinyago cha kwenye majaruba kikatishia ndege wala mpunga? Takukuru= kinyago cha majarubani.
 
Mh Raisi aliwaambia jana kuwa watakapo shindwa kupambana na Rushwa katika uchaguzi huu "Mungu Ibariki CCM" haya alitamba baba yao... kwa hiyo maneno ya nabii yanatimia...
 
kwani Takukuru wapo?
Mie nawaona hapa vijana walimwagwa kwa wingi maeneo haya yana vijisenti vya rushwa kwa wingi tu ..
Ndani ya mwaka mmoja kila mmoja ana Bangaluu la kutosha .. magari makali ya kutembelea
msinimeze nasema tu yale ninayoyaona
 
Katika uchaguzi wa umoja wa vijana magamba rushwa ilitawala kama kawaida yao. Ilifika mahali wana uvccm walikuwa hawataki kuona na kusoma sifa za wagombea wao kupitia vipeperushi na wengine walitamka bayana kwamba hawataki vipeperushi ila vipeperushwa.

Kiongozi aliyeingia madarakani kwa kununua kura hafai kabisa kuongoza Tanzania ya leo kwani atakuwa anafikiria zaidi namna ya kurejesha mali zake alizowekeza kupitia kura. Watanzania hususan vijana tuamke na tuwasaidie watu wetu kuwakomboa katika lindi la umasikini kwa kuipiga vita na kutokomeza kabisa ccm

Mungu Tanganyika
Mungu wabariki watanganyika

Source: Raia Mwema
 
chanzo TBC1

wanadai uchaguzi uligubikwa na Rushwa. wanataka urudiwe. wanakataa uongozi mpya

Ilifika mahali wana uvccm walikuwa hawataki kuona na kusoma sifa za wagombea wao kupitia vipeperushi na wengine walitamka bayana kwamba hawataki vipeperushi ila vipeperushwa.

Walioko Dodoma tunaomba habari zaidi.

nipo hapa chuo cha mipango dom nimeona vurugu kubwa zikifanywa na vijana wa ccm baada ya waandishi wa habari kua na press conference na baadhi ya wanachama wa ccm waliokuwa wakilalamikia uchaguzi ulivyofanyika,vurugu hizo zimefanywa na vijana wanaodaiwa kutoka kambi ya lowasa ambao walikuwa wanapinga hakukukwa na rushwa wakati vijana wengine walioshindwa kwa pesa kama Ahmed Nyanganyi na wenzake walikuwa wanalalamika kua BEN MALISA,MH NYALANDU,FRED LOWASSA NA RIDHIWANI,walikuwa wanagawa pesa kama njugu wakati uchaguzi ukiendelea kila mtu akiwa anawakilisha kundi lake hata hivyo cha kushangaza matokeo tiyari yameshavuja kabla hata hayajatangazwa rasmi huku ikisemekana mh SADIF JUMA KHAMIS ameshinda uenyekiti wa uvccm na MBONE MHITA,akishinda umakamu wa uvccm,pia kuna vijana toka kanda ya ziwa wanajiandaa kwa maandamano kwenda ikulu ndogo hapa dom kwenda kumpelekea barua ya malalamiko ya uchaguzi wakitaka kumshinikiza mh rais ayatengue haya matokeo;SOURCE;mimi mwenyewe niko eneo la tukio
 
Back
Top Bottom