Toothless TAKUKURU: Uchaguzi UVCCM watawaliwa na rushwa na vurugu

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,555
8,552
Breaking News
Uchaguzi wa UVCCM unaoendelea huko Dodoma umetawala vimbwanga watu wanatoa Rushwa kama ni agizo la chama!!Vijana wa vigogo wamemwaga mshiko sana na hawaogopi Takukuru!!!

================UPDATE==============
Vijana wa EL kwa kupitia kwa Bashe wamepeta!!Mgombea wa Riz aanguka waliowengi ni wa Bashe kwa maana hiyo nikwamba Edward Lowassa kuwa Rais 2015 nimkuwa zaidi!

chanzo TBC1

wanadai uchaguzi uligubikwa na Rushwa. wanataka urudiwe. wanakataa uongozi mpya


Ilifika mahali wana uvccm walikuwa hawataki kuona na kusoma sifa za wagombea wao kupitia vipeperushi na wengine walitamka bayana kwamba hawataki vipeperushi ila vipeperushwa.

Walioko Dodoma tunaomba habari zaidi.

chanzo TBC1

wanadai uchaguzi uligubikwa na Rushwa. wanataka urudiwe. wanakataa uongozi mpya


Ilifika mahali wana uvccm walikuwa hawataki kuona na kusoma sifa za wagombea wao kupitia vipeperushi na wengine walitamka bayana kwamba hawataki vipeperushi ila vipeperushwa.

Walioko Dodoma tunaomba habari zaidi.
nipo hapa chuo cha mipango dom nimeona vurugu kubwa zikifanywa na vijana wa ccm baada ya waandishi wa habari kua na press conference na baadhi ya wanachama wa ccm waliokuwa wakilalamikia uchaguzi ulivyofanyika,vurugu hizo zimefanywa na vijana wanaodaiwa kutoka kambi ya lowasa ambao walikuwa wanapinga hakukukwa na rushwa wakati vijana wengine walioshindwa kwa pesa kama Ahmed Nyanganyi na wenzake walikuwa wanalalamika kua BEN MALISA,MH NYALANDU,FRED LOWASSA NA RIDHIWANI,walikuwa wanagawa pesa kama njugu wakati uchaguzi ukiendelea kila mtu akiwa anawakilisha kundi lake hata hivyo cha kushangaza matokeo tiyari yameshavuja kabla hata hayajatangazwa rasmi huku ikisemekana mh SADIF JUMA KHAMIS ameshinda uenyekiti wa uvccm na MBONE MHITA,akishinda umakamu wa uvccm,pia kuna vijana toka kanda ya ziwa wanajiandaa kwa maandamano kwenda ikulu ndogo hapa dom kwenda kumpelekea barua ya malalamiko ya uchaguzi wakitaka kumshinikiza mh rais ayatengue haya matokeo;SOURCE;mimi mwenyewe niko eneo la tukio
 
Ni rushwa ya aina gani safari hii? maana tumezoea vitumbua, na ya foleni vyooni!
 
Mafisadi watarajiwa hao leo wanachaguliwa kwa rushwa yani hii nchi imeshauzwa na rais yupo kimya
 
Kusafisha hii nchi lazima CCM iondolewa madarakani kwanza. Ni wazi ukiindoa CCM kwenye utawala unakuwa umeondoa rushwa kwa zaidi ya 50%. Wanayoyafanya kwenye chama chao na hasa chaguzi ni zaidi ya aibu.
 
chaguzi za CCM na rushwa ni kama mapacha.. hawawezi kutengana ..mmoja hata kuwa na raha au kufa kabisaaaaaaaaaa
 
Jakaya kwa maneno yake amesema 'wanaowapa rushwa chukueni, lakini msiwapigie kura'. leo kasema wakati akiwahutubia hao wanaojiita vijana (wanafiki).
 
Breaking News
Uchaguzi wa UVCCM unaoendelea huko Dodoma umetawala vimbwanga watu wanatoa Rushwa kama ni agizo la chama!!Vijana wa vigogo wamemwaga mshiko sana na hawaogopi Takukuru!!!

Usiongelee kitu general, uwe specific, ni watoto gani wa vigogo, je ni ile orodha ya watoto wa vigogo walioko BOT, ni ile orodha ya watoto wa vigogo walioko NEC, au ni ile orodha ya watoto wa vigogo walioko TANROADS; maana orodha tunazolishwa ni nyingi tu!!
 
Tumeshawazoea,hosea aliwahi kusema wayasemayo hayapewi uzito bali wanayachukulia kama mazungumzo baada ya habari.
 
Takukuru ni kichaka cha mafisadi.

This is very true. Chaguzi zote za ndani ya CCM zimegubikwa na rushwa ya kutisha! Sumaye alitamka hivyo siku kadhaa zilizopita. Na sasa head of State, Jakaya Kikwete, amethibitisha bila shaka yoyote kuwa, rushwa ndani ya chaguzi kwenye jumuiya zote za CCM, ikiwemo UWT na UVCCM, ni ya kutisha na inaelekea kukizika chama hicho kikongwe hapa nchini. Sasa swali dogo tu la kumuuliza JK, kama hilo analijua, wakati anajua chaguzi zote za ndani ya CCM, huwa vijana wa Hoseah huwa wanajaa, wakijidai wanadhibiti rushwa. Sasa kama hiyo TAKUKURU inashindwa kufanya kazi inayotakiwa kuufanya hadi JK analalamika badala ya kuchukua hatua ya kuivunja TAKUKURU,na kurudia chaguzi zote za jumuiya na wakati huo huo amtimue kazi Hosea,kwa kutumia bure pesa za walipa kodi! Hapo sasa JK anataka tumweleweje, wakati tunajua Hosea amemteua yeye na kama kashindwa kazi anapaswa kumfukuza kazi na wala si kulalamika kwa wananchi. Kama safari hii asipomfukuza kazi Hoseah tutajua ni maigizo ya kawaida ya CCM, ambayo yeye JK mwenyewe kama alivyoasisi kile kitu kinaitwa kujivua gamba, ambapo kila Mtanzania hivi sasa anajua gamba limeishia kiunoni na limeshindwa kuvuka!! Hivi JK ataacha lini haya maigizo yake ya kitoto? ambapo anawafanya wa-TZ wote kama ni wavivu wa kufikiri! Tunathibitisha kwa mara nyingine tena kuwa janga kuu la Taifa kwa hivi sasa ni yeye mwenyewe JK!!!!!!!
 
Kama JK angekuwa kweli hapendi wala kuvumilia rushwa, angeitisha Baraza la Wadhamini wa CCM, Washauri na Waasisi wa CCM na kuangalia uwezekano wa kufuta chaguzi zote ziligubikwa na rushwa na kuwasimamisha uanachama wote waliotuhumiwa kwa rushwa.
Hapo zoezi la kujivua gamba lingekuwa rahisi mno, na CCM mpya ingezaliwa. Tatizo, Mwenyekiti muoga na hajiamini.
 
kikwete amedhihirisha kuna yeye ni dhaifu maana kamchagua hosea na hafanyi kazi yake alafu jk analia namuuliza rais kama yeye analia cc walalahoi tufanyeje
 
Dictatorship is the only type of leadership which could make TZ be where we dream.....
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom