TOL Gases Limited inaliwa wenye hisa zenu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TOL Gases Limited inaliwa wenye hisa zenu....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuntui, Jun 7, 2011.

 1. T

  Tuntui New Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niliweke wazi kwenu kampuni ya gas ya tanzania TOL Gases LTD iliyoko pugu road imekuwa shamba la bibi kwa muda mrefu na hii yote inasababishwa na Uongozi mbove chini mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mr. H.Temu, huyu jamaa amekuwa akifanya kila kitu kama anavyotaka .juzi katangaza nafasi za kazi kwa ma director watu tumeenda kufanya interview kumbe tayari nafasi zote wamepewa wakenya, wanahisa mnalalamika kampuni haipati faida wakati wakenya 4 wanalipwa 500mil kwa mwaka hii kwa sababu MD analipwa 20mil, na madirector 10mil kila mmoja wakati ukiuliza kazi zao ni utumbo mtupu huyo MD kajaza wakenya wenzie na anafanya finita za kufukuza waswahili wote subirini muone.Mr Temu amefanya fitina mpaka mzee Anorld akajiuzulu kisa kampuni ilishaanza kupunguza hasara.

  Kuna wabongo mainjia wa ukweli pale TOL wenye elimu ya kweli na uzoefu ndio maana unaona ile mitambo mpaka leo inafanya kazi lakini mishaahara yao ni aibu wanalipwa sio zaidi ya 3m kwa mwezi, pale watu wanaajiliwa kwa memo naomba Uhamiaji muhamie pale muone vituko wahindi na wakenya .

  Napata tabu kupata uwezo wa mwenyekiti wa Board waswahili amkeni ile kampuni hawezi kupata hasara mnaliwa...........................................WENYE HISA KATAENI UPUUZI

  NAWASIRISHA
  MIMI MWENYE HISA ZILIZOCHOKA --TUNTU
   
 2. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Sio hiyo tu mbona hizi zinazoitwa multi - national zote zina wageni wanaitwa ma-expat ambao wanafanya manegerial job za kawaida ambazo hazihitaji any special skills, wapo hata mafundi wengi tu wa kihindi, kifilipino kwenye migodi na bigger industries ambao wapo kwa ajili ya kujiendeleza wenyewe at the expense of locals, hao jamaa wa uhamiaji wakitoka hapo TOL wafanye ziara kwenye haya makampuni na wasiishie tu kwa ma HR wetu kwa sababu ndio wanasifika kwa short-cuts,
  mimi nipo mining napo mchezo ni ule ule wapo ma expat drivers, drillers, operator, supervisors, very foolish in deed...nao wana zaidi ya miaka mitatu..ina maana wabongo ni bongo lala kiasi kwamba wameshindwa kujifunza kutoka kwao so ina justify kuwepo kwao muda kama huo....:shut-mouth:
   
 3. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Pole Mkuu, jana tu wametimua wafanyakazi zaidi ya 27 bila sababu yeyote............Lakini TOL Gases LTD ilionyesha tangu mwanzo kuwa ingefika hapo ilipo kwani Uongozi wa mwanzo walimwachisha kazi kijana mmoja ambae alikuwa ROHO ya kiwanda..........Kuanzia hapo wiki moja baadae menejimenti ikafukuzwa kazi........miezi mitatu mkurugezi akasitaafu..........takribani miezi sita mkurugezi mpya akaachishwa kazi.......Wakaja sasa wakenya lakini bado hapajatulia......Damu ya Mwana KONDOO ilimwagwa kwa mtindo huo nadhani hatabaki mtu wazawa wote wataondolewa.......Wanawadanganya Viongozi ya kuwa eti MTAMBO WA KUZALISHA GESI ni Mkubwa hivyo uuzwe awnunue Mdogo kulingana na Mahitaji wakati Gesi haitoshi kwa kutoweka miundo mizuri ya kuuza gesi tu kuna mikoa mpaka leo wanachome na kuwatoza wateja wao kwa kila sentimita waliyochomea kwa sababu gasi hakuna.........Tuna nini waTZ?.............Serikali iko wapi..........?

  Ningekuwa mimi ningewaita wafanyakazi wote wa zamani kubadilishana mawazo bila kujali nini kilitokea.......


  MATUNDA YA L. MASHA Mbunge wa zamani NYAMAGANA
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  tatizo liko kwa wenye hisa kutojua nguvu yao kisheria na kuchekacheka na kutowawajibisha viongozi wao, ngoja muibiwe mpaka mtapojanjaluka
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  nikipita hili jukwaa lazima nipate hasira.....
   
 6. m

  mdawi Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe Mjini Chai, mimi ni mteja mkubwa saaana wa TOL ila nafikiria kutafuta supplier mwingine wa Gas, kuna Mainjinia Vichwa wametolewa kwa ajili ya FITNA na Majungu mfano G. Lyatuu alikuwa production Manager, A. Magai alikuwa Fundi Mkuu Mzee Matilya woote hawa ni vifaa wameamua kuleta wakenya na kuwaacha wazawa, nawaonea huruma wao walio na hisa pale.
  Immigration/Labour tafadhalini okoeni hili taifa linaangamia kwa kukosa MAARIFA Jamani.

  Any way mi napita kwa aliye na muda apite pale TOL awaulizie hao waliotajwa hapo juu ndio watakubaliana nami.

  Nawasilisha
   
 7. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2013
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Washikaji eee, vp huku nasikia wanauza hisa. Kuna matangazo wametoa kuhusu uuzaji hisa. Please mi nataka nijitose nikanunue, mnanishaurije ndugu zangu? Au bado kuna magumashi. Pia mlio na uzoefu tujuuzeni faida anazopata mwanahisa. Asante sana, si mnajua gas itakuwa njenje so kama vipi huu ndo mpango mzima kuwahi.
   
 8. K

  Kajunjumele BA JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2013
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 674
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu usifikiri hao unaowambia hawajui, Lahasha hata Wizara husika zinajua lakini hawa ndo wachangiaji wa sherehe zakitaifa Kanga na Kofia pamoja na Fulana hapo jumlisha na michango ya kuchangia mbiyo za mwenge. Watendaji hawana ujasiri ten wa kufanya kazi.

  Nchi hii kama ni gari basi halihitaji engine service bali injini iwe overhauled yote.Kila sehemu ni hivyohivyo ajira nyingi zinatangazwa kwa geresha kwa hiyo Ufalme wa kipepo hauwezi kupingana wenyewe tunachotakiwa ni kufanya uaamuzi Mgumu wa kuikataa serikali iliyopo madarakani na hata hiyo tutakayo iweka madarakani kwa kura ikileta uzembe ipigwe chini hapo ndo watakuwa na adabu.
   
 9. A

  Asamwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2013
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 2,546
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Kwa muda mrefu sana Kampuni ya TOL ilikuwa ina-operate kwa hasara ndiyo maana hisa zake zilibaki kwenye kiwango cha chini sana, nadhani sh. 145 kwa hisa moja katika soko la hisa la Dar es Salaam.

  Miezi ya karibuni hapa naona hisa zake zimeanza kupanda kwenye soko la hisa, na sasa hivi kiwango chake ni Tsh. 310 kwa hisa; hii ina maana kuwa hali ya kifedha ya kampuni imeanza kuimarika, na mahitaji ya hisa zake na wanaotaka kuwekeza yameongezeka.

  Natofautiana na mtoa mada kuwa wanahisa wako hatarini kuingia hasara. Badala yake naona kama mwelekeo wa kampuni ni mzuri kwa sasa.

  Uzuri wa kampuni ambazo zimeandikishwa katika soko la hisa Dar es Salaam (DSE) ni kwamba ripoti za utendaji wa kampuni zinawekwa wazi, na ikifikia mahali kwamba kampuni haikidhi masharti ya soko la hisa, basi inaweza kufutwa.

  Ambacho siwezi kuzungumzia ni swala la upendeleo au unyanyasaji wa wafanyakazi!
   
 10. H

  Helios JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2015
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 396
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  TOL hisa imefika 750 now
   
Loading...