Tohara yaua wavulana 20 kwa mpigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tohara yaua wavulana 20 kwa mpigo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Friday, 18 June 2010 22:58

  EASTERN CAPE, Afrika Kusini

  WAVULANA 20 wamefariki dunia baada ya kufanyiwa tohara katika eneo la jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini.

  Idadi hiyo ni miongoni mwa wavulana 60 waliofanyiwa tohara, mila ambayo ni muhimu kwa wavulana wanapoingia katika utu uzima kwa karibu jamii zote nchini nchini Afrika Kusini.

  “Vifo hivyo vimetokea katika siku 12 zilizopita, ambapo tisa kati ya hivyo vimetokea ndani ya masaa 24 yaliyopita,” alieleza Sizwe Kupelo, msemaji wa Wizara ya Afya wa jimbo hilo.

  Wavulana waliookolewa walipelekwa haraka katika hospitali ya Nelson Mandela huko Mthatha.

  “Wavulana wote 60 waliotahiriwa wana majeraha ambayo yamelazimika kufanyiwa utaratibu wa kitaalamu,” alisema Kupelo.

  “Wavulana wanne kati ya hao watalazimika kuondolewa kabisa viungo vyao vya uzazi, kwa kuwa bila hivyo hawawezi kupona. Tunasubiri kupata ridhaa ya wazazi wao ili tuendelee na utaratibu huo,” aliongeza.

  Mwanzoni mwa wiki hii, wavulana saba wa umri mdogo walinusurika katika tohara haramu iliyopangwa kufanyika katika shule moja, chini ta mtaalamu wa kijadi asiyesajiliwa mwenye umri wa miaka 55 ambaye pia amewahi kukamatwa mara kadhaa kwa makosa ya aina hiyo.

  “Tayari alishahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa lakini amekuwa akiendelea kufanya makosa hayo hayo. Miaka mitano iliyopita, karibu wavulana 20 walifariki dunia katika shule yake na 15 walilazimika kuondolewa uume,” ilieleza taarifa ya idara maalum ya afya ya Eastern Cape.

  Idara hiyo ya afya ilieleza kwamba inaendelea kuwasiliana na polisi, wanasheria na waendesha mashtaka kwa ajili ya kujaduili kwa kina kuhusu sheria ya tohara ya jadi, ambayo husimamia utamaduni huo kwenye jimbo hilo.

  “Tatizo kubwa hapa ni kwamba wazazi wanaona vyema kuwatumia wataalamu hao wa kijadi ambao muda mwingine huwalazimihsa watoto wao kufanyiwa tohara hiyo kijadi katika umri mdogo sana,” Kupelo alisema.

  “Tumeshawakamata baadhi na tunaendelea kuwatafuta wahusika, lakini iwapo wazazi wakionekana kutokuwa na nia ya kuwafungulia kesi, mara nyingi wamekuwa wakiachiwa huru na hurejea katika kazi yao, huku wakisababisha vifo hivyo vya watoto,” aliongeza.

  Mara nyingi, madhara hayo hutokea aidha mwezi Juni hadi Julai, au Novemba hadi Desemba.

  Mwaka uliopita, wavulana 91 walifariki dunia kutokana na aina hiyo ya tohara na wengine kwa mamia walilazwa hospitali kwa matibabu.

  BBC
  Chanzo Tohara yaua wavulana 20 kwa mpigo

  Hizi Tohara za Kienyeji jamani Zimepitwa na wakati watoto zetu Tukitaka kuwafanya Tohara tuende Hospitalini jamani sio kutumia Utalaam wa Kienyeji umeshapitwa na Wakati Wakuu.
   
 2. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii pia itakuwa ni fundisho kwetu hapa kuna mambo kama hayo ya Tohara za Kienyeji, ningependa Serikali ipige marufuku tohara za kienyeji kuepusha Vifo. Wahusika wa suala hilo wanaliona ila je utekelezaji upo?
   
Loading...