Kwenye ndoa unahitajika UAMINIFU. Uaminifu wenyewe ni pamoja na kumweleza mwenzio UKWELI (unavyouona wewe) ili kuboresha ndoa yenuKwa hiyo sasa,kwenye ndoa tunahitaji Ukweli au Uaminifu? Jibu moja Tafadhali...
Ukweli ni truth na uaminifu ni Faithfulness
nmekupata mkuuKatika context ya kuelezea jambo
Ukweli ni ile Hali (situation) ya kueleza kile anachokijua/alicho sikia kuhusu jambo fulani
Kwa maana hiyo ukweli sio universal ukweli wa kwako kuhusu magufuli sio lazima ukawa sawa na ukweli wa kwangu kuhusu huyo magufuli
Mengine wataongeza wengine
Ahadi za mwanaTANU mojawapo niUkweli ni zaidi ya uaminifu maana kuwa mkweli ni kuzungumza na kutenda yale yanayopaswa bali kua muaminifu nikutenda kwakuhakikisha hutoki nje ya makubaliano.
Kwamaana nyingine nikwamba mnaweza mkakubaliana kutotenda haki na atakaye to a siri ya makubaliano hayo sio muaminifu
Ndio maana watu hali viapo vya ukweli bali wanakula vya uaminifu kwamaana ya makubaliano
Ukweli ni kusema kwa usahihi kile kilichotendeka! Na uaminifu ni kitendo cha kuwa muungwana na kutokuwa mswahili!
Kiufupi uaminifu ni zaidi ya ukweli wenyewe kwa sababu ukweli huusemea sana uaminifu ingawa uaminifu nao unayo tabia ya kuujenga ukweli.
Kwa hiyo uaminifu na ukweli ni kama sarafu yenye pande kuu mbili zinazotegemeana.
thanks for your contribution, nimepata kituKuwa. Mkweli ni kujizuia kufanya mabaya au maovu au kufanya mambo kinyume na utaratibu au kusema ukweli na sio uongo iwe kweny mapenz au maisha ya kawaida kuwa mwaminifu ni kutokuwa na njia za kando na mkato au za pembeni au mchepuko.

Thanks zee la hekima nmejifunza kitu kikubwa Sana hapoUaminifu ni ile hali ya kutenda jambo ambalo mmekubaliana liwe zuri au baya. Uaminifu SIO KWA MTU bali ni kwa jambo fulani. Mtu aliye MWAMINIFU KWA NDOA YAKE hawezi kuchepuka. Mtu aliye mwaminifu kwa kiapo cha kazi yake atafuata maadili na maelekezo ya utendaji wake kwa ukamilifu. Ukweli maana yake ni tofauti kabisa na uaminifu. Unaweza ukawa MKWELI KWA NAFSI YAKO ukamwambia mwenza wako wa ndoa mambo yake yanayokukera. Ukifanya hivyo kwa nia ya kuboresha ndoa yako, hapo umekuwa mwaminifu kwa ndoa yako. Lakini lazima utambue kwamba wewe unachoona ni ukweli, kwa watu wengine kinaweza kuonekana kama uongo mtupu. Mara zote UKWELI unahusisha mawazo nafsini mwako kulingana na uzoefu au kile unachoamini. Kwenye nafsi yako, unaweza kuwa unadhani mwenza wako wa ndoa hakupendi na ukaamini ndio ukweli kumbe anakupenda lakini hafanyi matendo ya kudhihirisha hivyo. Lakini kama wewe ni mwaminifu kwa ndoa yako hutamwacha japo unadhani ukweli ni kwamba hakupendi (japo huo sio ukweli)
Ina uhusiano gani na uaminifu katika context hiyohyo ya kuwa kinyume na neno Uaminifu?Udhalimu ni kuwanyima watu “HAKI” zao.
Na mtu ambae ni dhalimu huwa na cheo/mamlaka fulani.
Na anakuwa mtu katili fulani asiye na huruma wala kujali utu !