Tofauti ya Uzinzi na Uasherati

Tofauti ya Uzinzi na Uasherati

iMind

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,232
Reaction score
5,534
Wengi hawajui tofauti ya haya maneno mawili. Ili kuwa mzinzi lazima uwe umeoa au kuolewa au una mtu ambaye unaishi naye kama mke na mme au mmekubaliana kuwa pamoja hata kama hamjaoana. Mtu anakua mzinzi au anazini pale ambapo anafanya mapenzi na mtu mwingine ambaye si yule ambaye hajaoana naye au yule ambaye siye aliyekubaliana naye kuwa katika uhusiano wa kimapenzi. Maana ndoa siyo lazima ifungwe kanisani au msikitini au kwa mkuu wa wilaya, ila pale unapokiri kwa kinywa chako kuwa umempenda mwenza wako na umekubali ukiwa na akili timamu kuwa utakuwa naye kama mpenzi bf gf n.k tayari unakuwa umefunga ndoa. Kanisani au msikitini au kwa mkuu wa wilaya hiyo ni formalities tu za kidunia.

Uasherati ni kitendo cha mtu asiye na ndoa wala uhusiano wowote wa kimapenzi kufanya mapenzi na mtu yeyote. If u a single unapofanya one night stand unafanya uasherati.

Uzinzi ni dhambi, ingawa uasherati siyo dhambi kwa mijibu wa dini ya kikristo. I hope nimeeleweka.

Kwa mfano kama hujaoa au kuolewa na huma mtu ambaye umefanya commitment naye. Ukiruka na changudoa pale corner bar unafanya uasherati na hii siyo dhambi. Kwa sababu hujamsaliti mtu na wala hakuna uvunjifu wowote wa amani au upendo unaweza kutokea.
 
news3.gif%3Fw%3D360%26h%3D360
church-of-satan-logo-black.png
 
Acha kujifariji kwa Uasherati wako. Uzinzi ni tendo linalomhusisha mmojawapo aliyeko kwenye ndoa, hapa unahusika usaliti wa ndoa na uasherati ni kitendo kinachomhusisha kijana ambaye hajaoa na binti ambaye hajaolewa na YOTE MAWILI YAANI UZINZI na UASHERATI ni DHAMBI KATIKA UKRISTO. Kama hujui biblia inakataza uasherati sehemu gani, soma hapa usaidike. WAGALATIA 5:19-21, Waefeso 5:3-7.
 
Back
Top Bottom