Tofauti ya uwekezaji wa hati fungani na masoko mengine ya mitaji kama Hisa

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,915
3,407
Hatifungani ni tofauti kabisa na masoko mengine ya mitaji kwa mfumo wake na hata faida zake.

> Kwenye hatifungani unapata faida bila ya kujali uchumi unakwendaje. Kwa sababu unaponunua hati fungani unajua kabisa ni riba kiasi gani unapata kwa mwaka. Lakini kwenye hisa hujui ni faida kiasi gani unapata kwenye uwekezaji wako. Faida inategemea na halinya uchumi, uimara wa soko.

> Kwenye hisa unapata faida pale hisa zinapofanya vizuri na unapata hasara pale hisa zinapofanya vizuri. Kwenye hatifungani unapewa riba uliyoambiwa bila ya kujali fedha ulizowekeza zimezalisha au la.

> Kwenye hisa unaweza kupata faida kubwa sana pale uchumi unapokwenda vizuri. Kwenye hatifungani utapata riba ile ile.

> Hatifungani zina kipindi maalumu baada ya hapo zinakomaa na hivyo kurudishiwa fedha zako. Hisa hazina ukomo wa kipindi, kadiri kampuni inavyoendelea kuwepo unaweza kuendelea kumiliki hisa zake.

> Kwenye hisa unaweza kushiriki kwenye vikao mbalimbali vya kampuni, kwenye hatifungani hupati nafasi hiyo. Wewe unawekeza fedha na kuchukua riba mpaka pale inapokomaa.
 
Asante sana kwa hili sababu kubwa nilipata nafasi ya kwenda hadi BOT kupata ufafanuzi lakini nika toka kapa . Je una weza ni sadia namna ya kufanya calculation zake , kwa mifano rahisi pamoja na malipo ya Tax kwa uwekezaji ?
Mfano kama nikiamua kuweza sh 10,000,000 kwenye Hati fungani , Je una calculate vipi ? na pia kama utatapata na fasi pia kama utaweze nielekeza nama ya ku calculat Tresuary Bills pia , Asante
 
Asante sana kwa hili sababu kubwa nilipata nafasi ya kwenda hadi BOT kupata ufafanuzi lakini nika toka kapa . Je una weza ni sadia namna ya kufanya calculation zake , kwa mifano rahisi pamoja na malipo ya Tax kwa uwekezaji ?
Mfano kama nikiamua kuweza sh 10,000,000 kwenye Hati fungani , Je una calculate vipi ? na pia kama utatapata na fasi pia kama utaweze nielekeza nama ya ku calculat Tresuary Bills pia , Asante
Habari mkuu,
Nimefafanua vizuri hili kwenye darasa nililotoa.
Labda nikufafanulie kidogo kwa mfano uliotoa hapa wa tsh milioni kumi.
Kwa mfano umeamua kununua bonds za NMB ambazo ndiyo zinatolewa sasa,
Bond hizi zinatolewa kwa miaka mitatu na riba yake ni asilimia 13 kwa mwaka na inalipwa mara mbili kwa mwaka.
Kwa hiyo kwa milioni kumi kwa mwaka utalipwa milioni moja na laki tatu (1,300,000/=) na hii itagawanywa mara mbili na kulipwa kwa kipindi cha miezi sita, hivyo utalipwa kama ifuatavyo;
Baada ya miezi sita tangu unumue bond utapewa tsh 650,000
Mwezi wa 12 utapewa tsh 650,000
Mwezi wa 18 utapewa tsh 650,000
Mwezi wa 24 utapewa tsh 650,000
Mwezi wa 30 utapewa tsh 650,000
Na mwezi wa 36 ambapo ni mwaka wa tatu utapewa tsh 650,000 pamoja na kurejeshewa ile milioni 10 yako.
Hivyo kwa ujumla unakuwa umevuna tsh 3,900,000/= kwa kipindi cha miaka 3 kutoka kwenye milioni 10 yako.
 
Asante sana , now nimeelewa vizuri kuhusu bonds ,Kama utapata na fasi tena tuta shukuru kama uta tueleza kuhusu treasury bills na kwa mifano rahisi haswa zile za 35 days , najua zinakua auctioned, je nazo zina kuwa calculated vipi ? tuki weka mfano huo huyo wa sh 10 million .Sorry kwa usumbufu wa ma swali mengi .asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom