Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,865
- 730,438
Ni kitu kinachoshangaza mno kwamba mzazi mmoja anaweza kuzaa mtoto mzuri wa sura na mwingine akazaa mtoto mwenye sura ya kutisha(sio ulemavu ).
Je kuna nguvu ya giza?
Je ni kizalia?
Je kuna mahusiano siku saa na dakika ya kushika mimba? Kwamba wazazi walikuwa kwenye mood gani? Hasira uchungu kisirani furaha au amani?
Je hawa wenye sura za kutisha ni binadamu kamili ama?
Inawezekana kabisa ni mazoea lakini sura ya mtu MARA NYINGI huelezea tabia na matendo yake....japo si wote lakini mara nyingi sura ngumu huwa na roho ngumu/mbaya pia.
Hapa sizungumzii ulemavu, kila mzazi hupenda kuzaa mtoto mwenye sura nzuri , ni mazoea tu ya kibinadamu ambayo yamepelekea kuleta hata mashindano mbalimbali ya urembo.
Mazoea haya ya kibinadamu yamepelekea utengano wa kimatendo katika jamii, kwamba eti ile sio sura ya kufanya kazi bank au ile sio sura ya kuroga nk nk
Tusichopenda kukubali ni kwamba SURA SIO ROHO kuna watu wana sura za kuvutia mno (kwa vigezo vya kibinadamu) lakini wana roho mbaya wamepiliza na kuna watu hawana sura nzuri kwa vigezo vile vile vya kibinadamu lakini ni watu wema kabisa
Hebu chukua kioo ujiangalie