Tulipo anza miaka ya 60/70 kozi nyingi za chuo zilikuwa miaka 3. Kwenye 1980s kukaingia kidudu mtu kukaja system ya miaka 4- nakumbuka SUA walibadilisha course nyingi kwenda miaka 4. Ilipokuja swala la mikopo kama mikopo uhalisia ukatuingia na course nyingi ziliangaliwa kwa jicho la miaka 3 kama miundo mbinu inaruhusu. UDSM na SAUT nafikiri wao wamekwama kwa miaka 4 na wengine kama Mzumbe ni 3. Labda watu wa Law School wanaweza kutuambia kama kuna tofauti kubwa kati ya wale wa miaka 3 na wale wa miaka 4. Nadhani kama program imepangwa vizuri hakutakuwa na tofauti.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.