Tofauti ya jiji la Dar na jiji la Nairobi

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,015
4,982
Hello guys,
Naomba Leo niwaletee tofauti niliyoona Kati ya jiji la Dar na la Nairobi.

Nairobi: Lugha kubwa inayotumika pale Ni English wengi hawajui kiswahili vizuri., ijapo huzungumza lugha zao kama kikuyu lakini English ndo lugha unayowaunganisha wengi, lakini Dar hata msomi WA Chuo English ya kuandika Ni shigida.

Nairobi: Bara bara zao Ni pana na Kuna hadi zenye njia 5 za magari kupita kwa wakati mmoja na ijapo Kuna foleni lakini inatembea tofauti na foleni ya Dar inaganda sehemu mmoja.pili madereva WA Nairobi wanajua kuendesha magari vizuri Sana kutokana na wingi WA magari na watu barabarani, Dereva WA Dar Nairobi hawezi kitu.

Nairobi: Wanawake Ni wengi Sana kuliko wanaume , kila baada nusu hatua utakutana na wanawake na wadada wengi kuliko wanaume . Idadi ya wanawake WA Nairobi haiwafiki WA Dar

Nairobi: Wanawake WA kule Wako very smart na huvaa short dress and skirt utafikir ulaya, na wanaume WA kule hawana ushabiki WA kijinga kama WA Dar WA kuwashangaa na kupiga yowe utafikiri wameona kakakuona.
Kila mtu tupo fee kuvaa na kwenda popote.

Nairobi: Jiji lilichangamka(busy)kuliko yote EA. Saa tisa usiku bara barani pako busy kutokana na wingi WA watu kwa ujumla kila mtu akiwahi sehemu ya shughuli yake.


Nairobi; mirungi huuzwa kama mchicha bara barani Yan kule Ni ruksa na Ni halali kufanya biashara hiyo.
Machinga hupanga kwenye Meza mirungi Yao .

Nairobi: Hakuna masista duh mavi kama ilivo Dar hapo mtu anakaa home anasubiri achune mibuzi mbwa ili siku iende wadada WA Nairobi Ni hard working mbaya kabisa na kwa kiasi kikubwa wanawake WA pale wameubeba uchumi WA nchi.

Nairobi: Hands craft, wakenya Ni watundu na watu wenye akili Sana katika mambo mengi.
Hutengeneza bidhaa nyingi za kiafrika kwa mikono na hupeleka nje ya nchi,eg.ulaya, America etc.
Asilimia kubwa ya wafanyabiashara WA Arusha huagiza mizigo Yao Nairobi.

Nairobi: Viwanda ndo usiseme.
Nairobi; kilimo ndo usiseme.

Na mengine mengi Tu ambayo sikundika hapa, lakini kiukweli wakenya wapo vizuri katika sekta zote.

Nairobi:elimu ya pale ipo vizuri Sana, watanzania wengi na waganda pamoja na nchi nyingine hupeleka watoto WA pale kupata elimu, hadi chekechea boarding Wako vizuri kwenye kuangalia watoto vizuri.


Nb: Wanaume WA kule Ni wanaume kweli Yan wapo kiume haswa sio wambea na wapashkunaku au wala chipsi Yai kama WA Dar.
Wanaume WA Nairobi wamesimama
 
kwa vitu vingi nakubaliana nawe labda kwa sababu ni EAC city hub, wamejiahidi to some extent
 
Kuvaa vimini na wanawake wenu walivyo na vipaja vimekomaa kama wakimbiaji wa marathon hawaoni hata aibu, vipi kuhusu uchafu mwaka huu East African limeongoza.
Na kuhusu lugha mna lugha gani nyie ya kusema spaki badala ya spika, mna poor pronunciation..!
 
Bushland bhana.. Kwahyo usmart nj kuvaa vimini..
Then kuhusu madereva usidanganye... Hakuna madereva wazembe kama wa nairobi..
Dereva WA Dar kupaki gari pembeni Nairobi na kutembea kwa ngoko panakuhusu.
 
Bado tuko nyuma Sana, hard working man ndo njia ya kutusua, viwanda ndo usiseme kilimo ndo usiseme

Maendeleo yako yataletwa na wewe mwenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii wala sio nchi ya viwanda. Hayo uliyoyasema kuhusu Nairobi wala hayawasaidii wakazi wa Nairobi, kama Kibera, Kawangwale, Kawangeme, Matopeni n.k...
 
Madereva daladala wa huk wakienda huko mbna watanyooka
Alf acha kufananisha wakikuyu na madem wa bongo ww
Wanaume wa huko si ndo wanaoongoz kupigwa na waume zao
 
Maendeleo ya Nairobi yameletwa na
Maendeleo yako yataletwa na wewe mwenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii wala sio nchi ya viwanda. Hayo uliyoyasema kuhusu Nairobi wala hayawasaidii wakazi wa Nairobi, kama Kibera, Kawangwale, Kawangeme, Matopeni n.k...
Na wakenya wenyewe ndo mana Hapo juu nkazungumzia kuwa saa tisa ya usiku wao tayari wapo barabarani, nimezungumzia pia swala la hard working hapo juu, sasa wewe sijui unaongea nini tena jombaaa
 
Pumbaf zenu Nairobi ndo nn kenge nyie .Kila mji unapendeza kivyake kulingana na geogafia ya eneo husika na vilevile mambo mengine pia. Wakenya mpo busy kuandika ujinga
 
Maendeleo ya Nairobi yameletwa na
Na wakenya wenyewe ndo mana Hapo juu nkazungumzia kuwa saa tisa ya usiku wao tayari wapo barabarani, nimezungumzia pia swala la hard working hapo juu, sasa wewe sijui unaongea nini tena jombaaa
Basi ngoja waje watakaokuelewa, maana sijaona cha maana hapo...
 
Back
Top Bottom