Tofauti ya hamahama ya 2015 na hii ya Leo ni nini?

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,346
Reaction score
9,846
Wananchi wa Tanzania,hususani wapinzani wako katika taharuki kubwa sana kwa sasa juu ya hatima ya nchi yao na hatima ya siasa za Tanzania kwa ujumla.
Matukio yanakuja kwa kasi mno mpaka kubashiri kesho itakuwaje linakuwa zoezi gumu kabisa!
Viongozi wanahama chama, watu wanatekwa, miili inaokotwa kwenye viroba, watu wanapigwa risasi, biashara zinafungwa ....
Halafu viongozi WANAUNGA MKONO JUHUDI ZA MHESHIMIWA RAIS.
Sawa na kuona mkristu akimsifia myahudi siku ya kukumbuka kifo cha Yesu!

Hii hamahama ukijiuliza maswali huwezi kuyajibu.
1.Kuna wanaosema Mbowe amekuwa kiongozi kwa muda mrefu.
Nafikiri Mwalimu Nyerere anayeenziwa leo alikuwa kiongozi wa chama kwa muda mrefu kuliko mtu yeyote ndani ya nchi hii.Wanaoisifia CCM kuwa taasisi imara hawaangalii umuhimu wa kitendo hiki cha Mwalimu kuwa mwenyekiti kwa muda mrefu. Hawajiulizi kuwa ingekuwaje kama wakati wa harakati za Uhuru au mara tu baada ya kupata Uhuru, mwalimu angeachia nafasi ya mwenyekiti, nini kingeweza kuwa hatima ya CCM Leo?
Watu wanalinganisha CCM na CHADEMA moja kwa moja.
Huwezi kufanya hivi, kila chama kinatembea kwenye kalenda ya peke yake kiharakati. CCM ni chama dola na kimekuwa hivyo kwa miaka mpaka watanzania wanataka kuzoea umasikini wao na kuamini ni sehemu ya maisha.
CHADEMA iko katika mpito kutoka chama cha harakati kwenda chama dola. Matukio ya nyumba ya jirani hayawezi fanana na yetu.
Wenzetu wana ndoa ya zaidi ya miaka 40,wameshajenga, wanavitegauchumi, wamemaliza kusomesha....
Sisi ndoa yetu ya juzi, mtoto hata kitovu hakijaanguka na bado watu wanataka style ya maisha yetu ifanane na jirani??? Wapi na wapi??
2.Kuna wanaosema ruzuku ya chama inatumika visivyo!!
Hawasemi inatumikaje isivyo pasi na kuwa matumizi yanaainishwa wazi.
Hivi kama mimi mwanachama wa kawaida nachangia chama, wewe kiongozi uliyewezeshwa kupata nafasi na chama unaona shida gani ukichangia?

Anyway ndipo tulipo, natamaani iwe ndoto niamke nikute mambo yako sawa lakini hakuna namna, lazima kikombe hichi tukinywe!

Kwa wanachama wa CHADEMA!
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi hata kidogo kwaajili ya viongozi kuhama!
Tuwe na wasiwasi juu ya wale wanaotaka kuiua demokrasia ya nchi yetu,wanaouvunja umoja wetu kwa nguvu, wanaotuteka, kutupiga risasi na kutuua.Kwa hawa tufanye jambo, kila mtu kwa nafsi yake kwa uwezo wake kwa jinsi Mungu atakavyompa nafasi!

Hawa viongozi wanaohama tumewaweka sisi wenyewe na hawahami na mawazo yetu wala mapenzi yetu kwa demokrasia na chama.

Hamahama ya 2015 ilitanguliwa na kashfa mbalimbali za chama tawala na uongozi kwa wakati ule.
Viongozi walihama kwasababu wanachama walishatangulia kuhama. Kwao kuendelea kubaki kwenye chama kusingekuwa na maana yeyote. Wangemuongoza nani?
Kwahivyo CHADEMA haina tatizo la uongozi au vipaji vya kuongoza. Mtashangaa mtakapoona sura mpya kwenye majukwaa siku Mungu atakapoulegeza moyo wa Farao.

Sitaki kusema kama wote wanaohama wananunuliwa ila ukiona mtu anakwambia anakupenda huku anatetemeka na kujikunja baridi basi ujue huyu anakuogopa.
Viongozi wanaohama wengi wana hofu kuu!
Je, nini kinawaogofya?
Labda usalama wao? Labda usalama wa watoto wao au wapendwa wao au usalama wa familia uko mashakani!
Ndugu zangu, tunaweza kuwananga kumbe wengine ni mateka wa kisiasa!

Kesho ni siku nyingine, Mungu ataleta mwanga!
Nawapenda sana.
 
Hio ndio tofauti pekee kati ya hamahama ya 2015 na hii ya sasa...
Watu wanasahau kama dhana ya uongozi wa kuchaguliwa/demokrasia ni uwakilishi.
Sasa kama hakuna unaowaakilisha, umaana wa kuhama unakosekana.

Korongoni-Moshi wamerudia uchaguzi wa diwani juzi.Wapigakura waliojiandikisha kwenye daftari ni karibu watu 5000, waliopiga kura juzi ni kama watu 1000. Hata robo ya waliojiandikisha haijafika.
Bado hizi kura 1000 CCM wamezigawana na vyama vingine kama ACT na SAU.
Halafu unakuta mtu anajipongeza kwa ushindi???
 
Kweli umedhihirisha kuwa Chadema ina watu ambao upeo wao wa kufikiri na kuchambua mambo ni mdogo sana. Kichwa cha habari na mambo uliyoyaandika ni vitu viwili tofauti kabisa. Umeleta hisia na mihemuko yako bila kutofautisha mambo. Nyerere kuwepo kwa muda mrefu wakati wa mfumo wa chama kimoja unataka kulinganisha na kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi na kukua kwa demokrasia. Pia umesahau kuwa chama chako kinaitwa chama cha demokrasia, lakini unataka kiongozi abakie madarakani mpaka mungu atakapompumzisha. Watu wakihoji, mnataka kuwafukuza chama. Pole sana Mbowe, kama hao ndiyo washauri ulio nao, wewe endelea kutafuna ruzuku na kuwafukuza wale wote wanaohoji. Ila kumbuka kuwa, kadri idadi ya wabunge inavyopungua, inakula kwako kwa kupungua ruzuku.
 
Nataka twende pamoja ili hapa hapa, kabla jogoo hajawika mara tatu,mimi na wewe tukubaliane kuwa nani kati yetu mwenye upeo mdogo wa kuchambua mambo!

Swali:
Mbowe amekula kiasi gani katika ruzuku ya chama mpaka sasa?
 
Kweli umedhihirisha kuwa Chadema ina watu ambao upeo wao wa kufikiri na kuchambua mambo ni mdogo sana. Kichwa cha habari na mambo uliyoyaandika ni vitu viwili tofauti kabisa. Umeleta hisia na mihemuko yako bila kutofautisha mambo. Nyerere kuwepo kwa muda mrefu wakati wa mfumo wa chama kimoja unataka kulinganisha na kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi na kukua kwa demokrasia. Pia umesahau kuwa chama chako kinaitwa chama cha demokrasia, lakini unataka kiongozi abakie madarakani mpaka mungu atakapompumzisha. Watu wakihoji, mnataka kuwafukuza chama. Pole sana Mbowe, kama hao ndiyo washauri ulio nao, wewe endelea kutafuna ruzuku na kuwafukuza wale wote wanaohoji. Ila kumbuka kuwa, kadri idadi ya wabunge inavyopungua, inakula kwako kwa kupungua ruzuku.
Umekimbia jumla boss!
Nakusubiri
 
Korongoni-Moshi wamerudia uchaguzi wa diwani juzi.Wapigakura waliojiandikisha kwenye daftari ni karibu watu 5000, waliopiga kura juzi ni kama watu 1000. Hata robo ya waliojiandikisha haijafika.
Bado hizi kura 1000 CCM wamezigawana na vyama vingine kama ACT na SAU.
Halafu unakuta mtu anajipongeza kwa ushindi???

ndio tanzania mkuu, time will tell
 
Wananchi wa Tanzania,hususani wapinzani wako katika taharuki kubwa sana kwa sasa juu ya hatima ya nchi yao na hatima ya siasa za Tanzania kwa ujumla.
Matukio yanakuja kwa kasi mno mpaka kubashiri kesho itakuwaje linakuwa zoezi gumu kabisa!
Viongozi wanahama chama, watu wanatekwa, miili inaokotwa kwenye viroba, watu wanapigwa risasi, biashara zinafungwa ....
Halafu viongozi WANAUNGA MKONO JUHUDI ZA MHESHIMIWA RAIS.
Sawa na kuona mkristu akimsifia myahudi siku ya kukumbuka kifo cha Yesu!

Hii hamahama ukijiuliza maswali huwezi kuyajibu.
1.Kuna wanaosema Mbowe amekuwa kiongozi kwa muda mrefu.
Nafikiri Mwalimu Nyerere anayeenziwa leo alikuwa kiongozi wa chama kwa muda mrefu kuliko mtu yeyote ndani ya nchi hii.Wanaoisifia CCM kuwa taasisi imara hawaangalii umuhimu wa kitendo hiki cha Mwalimu kuwa mwenyekiti kwa muda mrefu. Hawajiulizi kuwa ingekuwaje kama wakati wa harakati za Uhuru au mara tu baada ya kupata Uhuru, mwalimu angeachia nafasi ya mwenyekiti, nini kingeweza kuwa hatima ya CCM Leo?
Watu wanalinganisha CCM na CHADEMA moja kwa moja.
Huwezi kufanya hivi, kila chama kinatembea kwenye kalenda ya peke yake kiharakati. CCM ni chama dola na kimekuwa hivyo kwa miaka mpaka watanzania wanataka kuzoea umasikini wao na kuamini ni sehemu ya maisha.
CHADEMA iko katika mpito kutoka chama cha harakati kwenda chama dola. Matukio ya nyumba ya jirani hayawezi fanana na yetu.
Wenzetu wana ndoa ya zaidi ya miaka 40,wameshajenga, wanavitegauchumi, wamemaliza kusomesha....
Sisi ndoa yetu ya juzi, mtoto hata kitovu hakijaanguka na bado watu wanataka style ya maisha yetu ifanane na jirani??? Wapi na wapi??
2.Kuna wanaosema ruzuku ya chama inatumika visivyo!!
Hawasemi inatumikaje isivyo pasi na kuwa matumizi yanaainishwa wazi.
Hivi kama mimi mwanachama wa kawaida nachangia chama, wewe kiongozi uliyewezeshwa kupata nafasi na chama unaona shida gani ukichangia?

Anyway ndipo tulipo, natamaani iwe ndoto niamke nikute mambo yako sawa lakini hakuna namna, lazima kikombe hichi tukinywe!

Kwa wanachama wa CHADEMA!
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi hata kidogo kwaajili ya viongozi kuhama!
Tuwe na wasiwasi juu ya wale wanaotaka kuiua demokrasia ya nchi yetu,wanaouvunja umoja wetu kwa nguvu, wanaotuteka, kutupiga risasi na kutuua.Kwa hawa tufanye jambo, kila mtu kwa nafsi yake kwa uwezo wake kwa jinsi Mungu atakavyompa nafasi!

Hawa viongozi wanaohama tumewaweka sisi wenyewe na hawahami na mawazo yetu wala mapenzi yetu kwa demokrasia na chama.

Hamahama ya 2015 ilitanguliwa na kashfa mbalimbali za chama tawala na uongozi kwa wakati ule.
Viongozi walihama kwasababu wanachama walishatangulia kuhama. Kwao kuendelea kubaki kwenye chama kusingekuwa na maana yeyote. Wangemuongoza nani?
Kwahivyo CHADEMA haina tatizo la uongozi au vipaji vya kuongoza. Mtashangaa mtakapoona sura mpya kwenye majukwaa siku Mungu atakapoulegeza moyo wa Farao.

Sitaki kusema kama wote wanaohama wananunuliwa ila ukiona mtu anakwambia anakupenda huku anatetemeka na kujikunja baridi basi ujue huyu anakuogopa.
Viongozi wanaohama wengi wana hofu kuu!
Je, nini kinawaogofya?
Labda usalama wao? Labda usalama wa watoto wao au wapendwa wao au usalama wa familia uko mashakani!
Ndugu zangu, tunaweza kuwananga kumbe wengine ni mateka wa kisiasa!

Kesho ni siku nyingine, Mungu ataleta mwanga!
Nawapenda sana.

Hama hama ya sasa toka Upinzani kwenda CCM ni biashara kubwa ya polepole na wapambe wake akina Le mutuz, wanavuna pesa nyingi kupitia 10% kila kichwa wanachofanikisha kiunge mkono juhudi za kudhoofisha chadema na kuua upinzani kwa ujumla, zamani kidogo wapinzani walihama kwa hiali ingawa Slaa yeye alihamishwa na Benard membe kwa dola milion 2 na kununuliwa nyumba canada, Uhamiaji wa zamani ingawa uligubikwa na fitna na rushwa lakini haufanani na Uhamiaji wa sasa ambao umegeuzwa biashara wa wajanja wachache hukp CCM.
 
Back
Top Bottom