Tofauti ya elimu kati ya wanasiasa na wanataaluma,je inatuathiri vipi ?

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,491
8,301
Wanajamvi nianze kwa kuwasalimia.
Ni hivi juzi tumepokea taarifa ya ndugu zetu kukosa sifa za utumishi serikalini. Naamini kwa namna moja ama nyingine wote tumeguswa maana kile kishindo mwangwi wake ni mkubwa.
Tumemsikia waziri pia akisema sifa za wanasiasa ni kujua kusoma na kuandika,sina tatizo na hilo maana ndiyo sheria inavyotaka,
Tunajua kuwa wanasiasa ndiyo wanaopanga nakusimamia sera zote za taifa hili. Hapo ndipo ninaposhawishika kuanzisha mjadala huru usio wa kisiasa kwa mustakabali wetu wenyewe ambao ndiyo tunaowapigia kura wanasiasa,(unaweza kusema ma DC na RC hawachaguliwi na sisi) lakini anaewachagua tunamchagua. Jamani tunataka kuendelea na hii hali? Kama hatutaki nini kifanyike na kifanyike vipi.
Karibuni tujadili.
 
Back
Top Bottom