Tofauti ya CCM na CHADEMA ni majina tu ila mfumo ule ule

Tofauti ya CCM na CHADEMA ni majina tu ila mfumo ule ule

Wiston Mogha

Senior Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
168
Reaction score
141
-
1 .CONFLICT OF INTEREST ikumbukwe kuwa kufuatia uchaguzi wa 2005 Fisadi Mbowe asiyekuwa na nguvu ya Dola alikidaichama kiasi cha USD 181,949.00 sawa na kiasi cha sh TZS 300,215,850 kitu ambacho alifanikiwa kujilipa nusu ya pesa hizo ambazo marehemu Chacha- Zakayo wangwe alihoji akidai kuwa fisadi huyu hakustahili kujilipa pesa hizo kwani hazikuingia kwenye account ya chama na hazikuwahi kuonekana na mtu yeyote isipokuwa mbowe Mwenyewe na baba mkwe wake Mzee Mtei.
Ukiangalia mwenendo wa chama hauridhishi kabisa,wakati hali ya ofisi za mikoa ikiwa ni ya kusua sua huku mikoa mingine ikiwa haina hata ofisi kutokana na kushindwa kulipa kodi za mapango na hivyo kufukuzwa na wamiliki wa majengo- hali ya kuchekesha na kusikitisha inakuja pale ambapo Mtendaji mkuu wa chama hiki Dr willibrod Slaa anapoamua yeye na genge lake kumkubalia kujilipa kiasi cha sh million 13.5 kwa mwezi,huku makatibu wa Mikoa,Wilaya,Kata na wengine wakiwa hawalipwi hata senti moja.
-
2.MIUNGU WATU Wanachama wa chama hiki hawana ruksa ya kuzungumza wala kuwakosoa viongozi na endapo mtu yeyote atajaribu kuwarekebisha basi mtu huyo ataitwa msaliti,na hivyo kunyang’anywa madaraka aliyonayo au kuvuliwa kabisa uanachama wake,hali hii haikuanza leo, hata wakati marehemu Chacha zakayo wangwe alipokuwa hai na kujaribu kukemea juu ya matumizi mabovu ya ruzuku ya chama,alinyang”anywa wadhifa wake,vivyo hivyo kwa Kafulila ambaye ni Mbunge wa chama cha CUF kwa sasa naye alifukuzwa baada ya kuonekana anajaribu kuwa rekebisha,pia wapo vijana wengi ambao wamekumbwa na kimbunga cha kufukuzwa na kuitwa wasaliti eti kwa vile tu hawakukubaliana na matakwa ya viongozi hawa.Imefika hatua mbowe hataki kuachaia madaraka na kudiriki kutamka bila woga kuwa HAJAONA MTU MAKINI WA KUONGOZA CHAMA HIki,kimsingi kauli hii ni ya kuwadharirisha wanachama -wote.

3. UBABE Chadema ni chama kilichonjia panda kwa sasa kutokana na ubabe alionao Mwenyekiti wa chama hiki ambaye ikibainika kuwa kuna viongozi ambao hawapendezwi na mwenendo wake,basi viongozi hao watachukuliwa hatua mara moja,pia kama kiongozi wa chama amekuwa akiahirisha uchaguzi mkuu wa chama hicho kwa vipindi vitatu sasa akidai kuwa chama hakijajipanga vizuri,huku akiwavua madaraka viongozi wasiokubaliana nae na kusimiki viongozi wamuda,pia amebadili katiba ya chama bila ya kuwashirikisha wanachama wake,kimsingi amekuwa ni kiongozi ambaye ukomo wake wa uongozi haujulikani kwani pamoja na kukifikisha chama hiki katika hatua hii mbaya bado anaendelea na jitihada za kuhakikisha anaweka mgombea hafifu ili eti ionekane kuwa kashinda kwa kishindo,kwakweli kwa mwenendo huu watanzania tumeshawashtukia watu hawa na hatuna budi kujitenga mbali nao.

4.UFUJUAJI WA PESA ZA CHAMA- mnamo mwaka 2008 chama hiki kilipata msaada wa fedha wa kiasi cha Sh million 78,000,000 kutoka kwa chama cha conservative cha uingereza kwa ajili ya kununua baiskeli na piki piki ambazo hazikununuliwa na badala yake zilitafutwa pikipiki zilizokwisha tumika.kilichofanyika baada ya kutapeli pesa hizo jamaa hawa walitafuta risiti za kughushi ili kuficha madhambi yao,hata hivyo utapeli wao umewapa uoga kiasi kwamba wanaona aibu kiasi cha kukwepa hata kushiriki katika vikao vya DEMOCRATIC UNION OF AFRICA{DUA} Muungano wa vyama vya upinzani kwa kuofia kukutana na wafadhili ambao ni Conservative party na Republican ya Marekani.Pia viongozi hawa wamekuwa wakijiamulia wenyewe juu ya matumizi ya fedha,wamekuwa wakisafiri nchi nzima kwa kutumia helkopta na Magari wakiidai wanajenga chama mwisho wa yote baada ya ziara zao wamekuwa wakijilipa gharama zote kuanzia kula,kulala,kunywa pamoja na hawala zao na kibaya zaidi kila helkopta inaporuka wamiliki wa helkopta hizo hudai wamekikodisha chama hivyo fedha zote za chama huishia kujilipa wenyewe.
Chama hiki kwa sasa kinapata ruzuku ya kiasi cha Sh million 200 kila mwezi ,cha kusikitisha ni kuwa badala ya fedha hizi- kutumika vizuri ili kujenga chama, mgawanyo wake umekuwa ni wa kifisadi kwani kila jimbo linapaswa kupokea ruzuku kila mwezi kitu ambacho hakifanyiki kikamilifu,viongozi hawa wamekuwa wakipeleka ruzuku majimboni mara moja kwa miezi mitatu au miezi sita,ukiangalia Kadi za Chama kila mwanachama hununua kadi yake na sio kupewa bure,Uniform za Chama kila mtu hujinunulia uniform,kadhalika bendera za chama Hugawiwa kipindi cha kampeni pekeake na ikitokea jimbolikapewa Bendera basi Ruzuku ya mwezi ya jimbo hilo hukatwa,kwa maana ya kwamba bendera hizo watakuwa wameuziwa,hali hii inaonyesha wazi kuwa hizi pesa ni kwa ajili ya wao na familia zao,kwani mbali na viongozi wa juu hakuna binadamu yeyote wa chadema anayelipwa chochote

5.UBAGUZI chama hiki kimeonekana kuwa na ubaguzi kwani imefika hatua mwanachama wa CDM akionekana katika kundi la wanachama wa CCM anaonekana kuwa ni msaliti na kushukiwa kutoa siri za chama,Kwa upande wa dada zetu ambao eidha wanawachumba wa vyama vingine au waume wa vyama vingine wamekuwa wakibaguliwa na kutoshirikishwa kikamilifu katika shughuli za chama.Mtu yeyote ambaye alishafukuzwa au kukosana na viongozi wa chama hutengwa na wanachama kupewa onyo kali kwa kutakiwa kutokuonekana naye mahali popote,Mfano Mzuri ni Hivikaribuni ambapo wasanii wa bongoflaver walipojiunga na CCM bila aibu wala woga kiongozi anayejidai kuwa na huruma kwa watanzania Freeman Mbowe,alidiriki kutangaza hadharani katikia mikutano ya hadhara kwamba watanzania wasinunue kazi za wasanii hao,Viongozi hao wamekuwa wakieneza dhana ya ubaguzi kwani imefika hatua wanawafundisha -watanzania kuvibagua vyombo vya habari kama TBC,UHURU,STAR TV,RAIA MWEMA,MTANZANIA na JAMBO LEO kwa madai ya kuwa vyombo hivi havikitendei haki chama chao,Viongozi hawa pia ilifika hatua wakatufundisha watanzania kumbagua Rais wetu na kumporomoshea matusi na kumuita majina ya kila aina,kama haitoshi wamewafundisha hata wabunge wa chama hiki kuwabaguwa wabunge wa vyama vingine bungeni,kwa mwenendo huu chama hiki kikikamata dola wananchi tutajuta.
-
6.UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUMU swala hili halifichiki na halihitaji hata elimu ya Chekechea ili kulielewa,chama hiki kimeonekana kuwa kipo kwa ajili ya kuwawezesha,Mbowe na genge lake kuwa patia,Mabibi zao na dada zao ubunge wa viti maalumu,mwaka 2010 Mbowe kwa makusudi mazima akishirikiana na wahuni wenzake walivuruga uchaguzi wa wanawake ambao- ulikuwa ufanyike kwa haki ,baada ya mbowe kuona mabibi zake na mabibi wa rafiki zake pamoja na dada zao hawajakubalika na wanawake wenzao walivuruga uchaguzi huo na kutoa tamko la kuwataka wanawake kugombea majimboni.wakatangaza kuwa wanawake wanaogombea katika majimbo watapewa kipaumbele,bila ya huruma yeyote viongozi hawa waliwahujumu dada zetu na mama zetu, ambao walifanya kazi kubwa na kuishia kupoteza fedha nyingi majimboni huku ubunge huo wakipewa dada wa Tundu lisu,Mkwe wa Slaa ukiacha Mchumba wake wa sasa,Hawara wa Mbowe Joyce Mukya,Mtoto wa Ndesamburo,ndugu wa Mtei na waliopata wachache kwa lengo la kufunika uovu wao
 
Kama hamuwaogopi chadema,mbona mnawatajataja..
Adui kama akupi shida wala HUMUWAZI
 
Mkuu nakubaliana na kichwa cha mada yako ila ndani hujatuonesha usawa wa CCM NA CHADEMA umeikosoa CHADEMA ila CCM Umeiacha
 
Madhara ya kukubali kuwa mtumwa wa kusafirisha sembe la riz 1 beijing na mexico ilisha kuathiri medula oblangata!
-ujipime na ujitafakari kwa uelewa wako wa kufananisha matukio kwa msingi sote tuko sawa umeshafeli kitambo.
 

Attachments

  • TMPSNAPSHOT1429819801119.jpg
    TMPSNAPSHOT1429819801119.jpg
    30.2 KB · Views: 125
Sijui baada ya october mwaka huu atajilipa kiasi gani maana Zitto anazidi kuharibu kuna khofu ya kukosa ruzuku kabisa
 
Chadema ni saccos ya wapiga dili na kutafuna ruzuku

Haya uliyoandika yote yalikuwa yakindikwa zamani na Id ya Tuntemeke, ila baada ya nyinyi kufukuzwa hakuna siri za chama tena zinavuja, na kiwango kikubwa post inakuwa kama imeandikwa na kiongozi mkuu wa chama.kilichobeep juzi kwa hisan ya watu wa Lumumba na lile fisadi linalousaka urais. Ni hici hamna siasa za kistaarabu wala nini zaidi ya kujifanya wasomi huku mkiamini kishirikina zaidi. Juzi mlikuwa mnajigamba cdm imevunjika kwa propaganda mfu eti huyo superstar kaondoka na.yeye ndio ilikuwa injini, lakini baada ya taasisi makini kuingia field imebidi mtoke na habari za kwenye archieve. Yaani mna mambo ya watoto wa shule ile mbaya. Hivi kweli mnaweza kusimama mbele ya wanaume mmjigambe kwa mbinu za kiccm eti nyinyi ndio mlioendesha taasisi makini kwa elimu zenu wakati mnaamini ushirikina wa kipuuzi. Aibu imewapata baada ya mbinu yenu ya kizee kujibiwa ontime. Na kama kweli nyinyi sio kikundi cha wapenda madaraka.chini ya kiongozi wenu mwenye uchu wa madaraka, fanyeni mikutano kama taasisi muone kama aibu haitawapata., wengine znz, wengine musoma kwa mpigo. Nyie ni macheckbob tu mmepata hela.za mafisadi mnazila kiujanja kwani mmewaongopea eti mnaweza kupambana taasisi makini kama.cdm.
 
Back
Top Bottom