Tofauti kati ya kufunga na kuahirisha kikao.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,678
Ndugu...Ni tofauti gani ya haya maneno mawili Kufunga kikao na kuahirisha kikao?
 
kuahirisha, maana yake, hakifanyiki kama ilivyopangwa, badala yake kitafanyika wakati/siku nyingine.

kufunga kikao, maana yake kuhitimisha baada ya kumaliza.
kilianza kwa kufunguliwa ili kuruhusu utaratibu wa mijadala rasmi, sasa mijadala imefikishwa mwisho na mwenye dhamana.
 
Tafuta kamusi ya kiswahili kisha tafuta maana ya kufunga na kuhairisha mkuu
 
Kuahirisha kikao ina maana kuna
Maazimio au muafaka haujafikiwa au kufanikiwa hivyo mpaka kiitishwe tena wajadili
Kufunga kikao ina maana muafaka
Na maazimio yamefikiwa hivyo
Kinachobaki ni utekelezaji tu
 
Neno halali la kutumia hapo ni kufunga kikao lln watu wamezoea kusema kuahirisha half wanaona ndio ujanja
 
Back
Top Bottom