Tofauti kati ya CCM na CHADEMA.

herikipaji

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
1,198
1,345
Hivi kuna tofauti gani kubwa kati ya vyama hivi vya siasa kati ya CCM na CHADEMA?
Hapa tuwapime kwa maneno na matendo yao wanachokiamini na kukisimamia kwa misingi ya itikadi, falsafa na ajenda kubwa wanazozifuata ili kutimiza malengo na kuhakikisha vyama hivyo vinaleta tija kwa jamii na taifa.
CCM wana ajenda ipi kwa sasa, na CHADEMA je?

Katiba za vyama hivi kuna mengi mazuri yameandikwa lakini je wanayasimamia na kuyaishi?

Mie binafsi nimejaribu kufanya uchunguzi wa kina na nikahitimisha kuwa hivi vyama CCM na CHADEMA ipo tofauti moja tu kubwa ni kuwa CCM wana tawala nchi kwa sasa tena utawala wa kidhalimu tu[Siyo kuongoza], na CHADEMA bado hawajafankiwa kupata nafasi ya madaraka makubwa.

Lakini CHADEMA ni kama CCM tu wanafanana wote ni WACHUMIA TUMBO tu.

Sasa raia wafanye nini kama wote ni wachumia tumbo!

Jibu: Mateso hayatoisha kwa watawaliwa hadi watawaliwa wenyewe waamue kuwadhibiti watawala dhalimu->hii haijalishi nani au chama gani kinatawala binadamu akipata mamlaka lazima adhibitiwe usipofanya hivyo utakiona cha mtema kuni.

Nini mtazamo wako na wewe?
 
Wote sawa tu hiyo ni kweli cha msingi ni wananchi kupevuka hata kama chama gani MTU akileta mizengwe ananapipiwa tu hakuna cha chadema wala mjukuu wa tanu au afroshirazi
 
Huo ndio uhalisia na wanachama na mashabiki wa vyama hivi vya Siasa ndio wanaotuharibia Nchi.
Mungu awape adhabu wanayostahili kwa unafiki wao
Na ni wanafiki wakubwa sana hawafai kwa lolote, huwa hawataki kuambiwa ukweli/kukosolewa nk ukifanya hivyo utaambulia matusi na vitu ka hivyo hufikiri.
 
Wote sawa tu hiyo ni kweli cha msingi ni wananchi kupevuka hata kama chama gani MTU akileta mizengwe ananapipiwa tu hakuna cha chadema wala mjukuu wa tanu au afroshirazi
Kweli yani inatakiwa akileta tu mizengwe aambiwe toka we utufai mchumia tumbo hapo mambo yataenda mkuu na wataacha kupigania madaraka sababu watajua kuna kuwajibika.
 
We hapa nimeandika uhalisia kama huamini basi nawe fanya uchunguzi wako utaamini nachoeleza
Sijabisha mkuu..ila ni namna ulivyo eleza na kwenda kwenye itimisho bila kutupa viashiri ilivyokutana navyo katika tafiti yako juu ya hili
 
Hivi kuna tofauti gani kubwa kati ya vyama hivi vya siasa kati ya CCM na CHADEMA?
Hapa tuwapime kwa maneno na matendo yao wanachokiamini na kukisimamia kwa misingi ya itikadi, falsafa na ajenda kubwa wanazozifuata ili kutimiza malengo na kuhakikisha vyama hivyo vinaleta tija kwa jamii na taifa.
CCM wana ajenda ipi kwa sasa, na CHADEMA je?

Katiba za vyama hivi kuna mengi mazuri yameandikwa lakini je wanayasimamia na kuyaishi?

Mie binafsi nimejaribu kufanya uchunguzi wa kina na nikahitimisha kuwa hivi vyama CCM na CHADEMA ipo tofauti moja tu kubwa ni kuwa CCM wana tawala nchi kwa sasa tena utawala wa kidhalimu tu[Siyo kuongoza], na CHADEMA bado hawajafankiwa kupata nafasi ya madaraka makubwa.

Lakini CHADEMA ni kama CCM tu wanafanana wote ni WACHUMIA TUMBO tu.

Sasa raia wafanye nini kama wote ni wachumia tumbo!

Jibu: Mateso hayatoisha kwa watawaliwa hadi watawaliwa wenyewe waamue kuwadhibiti watawala dhalimu->hii haijalishi nani au chama gani kinatawala binadamu akipata mamlaka lazima adhibitiwe usipofanya hivyo utakiona cha mtema kuni.

Nini mtazamo wako na wewe?
CHADEMA NI CHAMA NI BORA SANA KINA WATEA WALA UNGA, WALA MIRUNGI, GIROBA, PIA KINATETEA MAFISADI, PIA WANACHAMA WAKE NI WATUMIAJI WA VITU VILIVYLTAJWA HAPO, PIA WANATUMIA 75%YA SIKU WAKIJIFARIJI MITANDAONI. Upande wa CCM ni chama kikubwa KIMESHINDWA kutea wala madawa ya kulevya, viroba, bangi, mirungi, wala mafisadi, zamani wanachama wa ccm waliogopana kupeana KADI NYEKUNDU.
 
Ukitaka kujua chama kiko sawa na kipi hakiko sawa angalia wanaotoka ccm na kwenda cdm wengi wao hawatoki ccm kwa wema kwamba wanaondoka ccm kwenda kuleta mabadiliko wengi wanatoka skendo na wengine ulafi wa madaraka
 
Back
Top Bottom