Toa ushauri kwa televison ya taifa TBC

Toa ushauri kwa televison ya taifa TBC

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,244
Tuna weza kuwa tunalalamika kwa upuuzi mkubwa ambao umekuwa sasa ni kero kubwa sana kwa watazamaji.
Na hasa ikitambulika kwamba kodi zetu ndizo kwa namna moja au nyingine zinaendesha TBC.
1- Je unafikiri ni nini hasa TBC wanashidwa kwenda na wakati uliopo.
2 - je viongozi waliopo TBC, uwezo wao umepitwa na wakati uliopo.
3 - je serikali kuingiza itikadi za kichama ndio sababu ya kukosa viongozi macreative
4 - je unafikiri kunauwezokano wa hiki kituo kuwa chombo huru kisicho ruhusu mikono ya serikali.
Naomba tutoe maoni ili waweze kuyachukua na kuyafanyia kazi. Kero zilizopo TBC zaweza kusababisha mtu kufa kwa kupata heart attack. Tuwasaidie watupunguzie maudhi.
Chombo cha Taifa aibu tupu.
 
382538_595292073836700_439303796_n.jpg
waendelee hivi hivi
 
Inaongozwa na watu wasio wazalendo bali wenye mrengo wa kichama
HII sio TV ya taifa ni Tv ya CCM au TBCCM1
alipaswa kujiuzulu mara moja Mkurugenzi wake kwa kashfa kubwa dhidi ya rais wetu.
Obama kawa lini rais wa Tanzania?
Hii ibinafsishwe tu wapewe wazalendo kuiendesha kwa manufaa ya Umma.
 
382538_595292073836700_439303796_n.jpg
waendelee hivi hivi

hahahaha mkuu niliona hii nikashindwa hata kushangaa nafkiri ukiondoa haya makosa ya kiufundi pia bajeti nafikiri ni ndogo sana halafu hakuna ubunifu katika vipindi na pia ni vipi shirika linaweza kuendeshwa kibiashara tido alijitahidi wakamuondoa sasa huyu jamaa wa sasa hivi naona bado
 
Mbona tangu zamani tbc washenzi! UDOM tuliwapga marufuku kuja kupata habari za migomo,wachakachuzi,to hell tbc
 
Wenye chama lao naona wamekaa kimya!!! jamani toeni ushauri kwa tv yenu iweje??
 
Wenye chama lao naona wamekaa kimya!!! jamani toeni ushauri kwa tv yenu iweje??
Sisi wenye CHAMA tunasema TBC1 endeleeni hivi hivi!
Rais wetu ni Obama maana ndiye anayeiendesha nchi tokea USA..
Hamuoni msaidizi wake anavyoenda mara kwa mara kuchukua maagizo?!
Sasa kaja mwenyewe kukagua ki-jimbo chake na kuondoka!
Tehe!
TBC1.
 
Wawe makini ili next time isije ikatokea tena slip of the keyboard halafu gabriel zakaria haupukane na maneno ya barabara ya morogoro road
 
tbc haiko huru na ndo tatizo kubwa!!
watafute viongozi wasioionea aibu serikali yan watakao kuwa na tayari kusema yote hata kama wamewekwa na serikali hiyihiyo
but ukweli ni kwamba Mrisho ni kivuli obama ndo anatoa order kama enzi zile za ukoloni
 
Kingine wakati wa ziara pia yule mama alikuw anatuunganisha live alijichanganya na kusema yamebaki masaa kadhaa ndege kutua badala ya dakika kadhaa pia alisema obama rais wa Tanzania huku ni kutojiamin na kutokuw makini kwa kwel alisikitisha sana.
 
Uhuru kwa wafanyakazi uongezwe ikiwepo wa kukosoa serikali pale inapokosea, Pia suala la uongozi liangaliwe vizuri maana naona kama ''nepotism'' imezidi.Mwisho, wafanyakazi wawe na uzalendo wakitambua kuwa sisi ndio tunaosaidia watoto wao waende ''msalani'' vinginevyo barabara ya kuelekea vyoo vyao itaota nyasi!!
 
Wakizunguka mitaani kutafuta maoni ya watu kuhusu jambo Fulani, yale yanayokosoa serikali wanayaedit wanaacha tu yale ya kusifu. Sijui hawajui kwamba wananchi wanapenda zaidi kuona serikali yao ikikosolewa ili iwajibike zaidi na sio kusifiwa tu, na kupigia chama tawala propaganda. Chama tawala si wawe na TV yao? Tutawapiga mawe mitaani msipobadilika, shauri yenu!
Uhuru kwa wafanyakazi uongezwe ikiwepo wa kukosoa serikali pale inapokosea, Pia suala la uongozi liangaliwe vizuri maana naona kama ''nepotism'' imezidi.Mwisho, wafanyakazi wawe na uzalendo wakitambua kuwa sisi ndio tunaosaidia watoto wao waende ''msalani'' vinginevyo barabara ya kuelekea vyoo vyao itaota nyasi!!
 
Yani hawa jamaa wapo wapo tu... Hawana ubunifu, hawawezi kupangilia vipindi...wanakera ile mbaya... Hv kuna tofauti gani kati ya kipindi cha bang na beat agenda
 
Sisi wenye CHAMA tunasema TBC1 endeleeni hivi hivi!
Rais wetu ni Obama maana ndiye anayeiendesha nchi tokea USA..
Hamuoni msaidizi wake anavyoenda mara kwa mara kuchukua maagizo?!
Sasa kaja mwenyewe kukagua ki-jimbo chake na kuondoka!
Tehe!
TBC1.

Yani umenichekesha ile mbaya.
 
Back
Top Bottom