Mbunge wa Bukoba vijijini Mh Rweikiza hajawafanyia lolote wapiga kura wake,anachowakirisha bungeni anakiju mwenyewe,hakuna wilaya yenye matatizo kama hiyo,njaa imeikumba sababu ya mnayuko na udongo kuchoka,vijana jobless wameongezeka kwa kasi sana na wengi wamekata tamaa ya maisha hakuna anayewasaidia kuwawezesha angalau waigie kwenye kilimo chenye tija au biashara,wilaya aina hata kisima kimoja,mito mingi ya asili imekauka,maeneo mengi ndoo ya maji ni kati ya sh 400 na 500 kutegemeana na kama yameletwa na pikipiki,baiskeli au kichwa,wakina mama na vijana wanatumia muda mrefu kwenda kutafuta maji na hivyo kuathri shughuli za maendeleo,sasa hivi wanaomba mvua inayoendelea isiishe kwani imewapunguzia gharama za maji.
Yote hayo mbunge hayajui,yuko anakula nchi Dar na Dodoma na akija mara chache ni kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya shule yake na kuwanunulia wazee walafi Rubisi huku wakimuhakikishia kuwa mpinzani wake bado hajazaliwa.Lakini asisahau kwa Bukoba vijijini ni nadra sana mbunge ku serve terms mbili.