Toa sababu za kwanini mbunge wako unataka aendelee au ang'oke mwaka 2015

TRIPLE H

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
651
349
Kila mtanzania popote alipo anaye mbunge anayemwakilisha ndani ya bunge;awe amemchagua au la.Hata wewe mtanzania mwenzangu popote pale ulipo unaye mbunge anayekuwakilisha!
Je,unazo sababu za kwa nn aendelee kuwa mwakilishi wako? na je,ungetaka asichaguliwe tena ktk uchaguzi mkuu ujao? toa sababu.
ANGALIZO: Uruhusiwi kushambulia kwa matusi mbunge asiye wa jimbo lako kwa kuwa hakuhusu.
 
Mbunge wangu ningependa aendelee kwani ni bonge jembe. Ni yule wa ZIMBABWE iliungana na ZANZIBAR. Namkubali sana.
 
mbunge wangu namshauri apishe kiti kwan amekaa vya kutosha, tunataka mtu mbunifu na mtetezi wa kweli kwa wananchi. aliyepo anawatisha wanachi kwa kuweka vibarakawake kuanzia kitongoji ad tarafa ili wasimamie na kulinda kitichake na kudhibiti changamoto za vyama vya upinzani. ni Mnadhim wa serikali (Lukuvi)
 
Akiendelea ni vizuri ila anatajwa anataka kuongoza nchi. Nampenda sio mzungumzaji Sana ni mtendaji . Kila la heri mbunge (EL)
 
mbunge wangu mnyika ameshindwa kila kitu namshauri arudi uds akasome jimbo awaachie ccm
 
Wee unaemkataa Mnyika mbona yule mbunge wenu aliyeiba kura kipindi kilichopita hakufaya chochote jimbo la ubungo?? alpokwenda ensile bado Manispaa hazijagawanywa ndio sifuri kabisa.
 
ni vzr kuwa wazi,taja jina lake na uelezee sababu za kumkubali au kumkataa na siyo kuhemka.
 
Deo Sanga! jah people ameshaandika historia yake kwa kuingia bungen na elimu ya drs la pili. Hakuna alichofanya Njombe kaskazini aende kwa amani
 
mbunge wangu sitaki hata kusikia jina lake maana tangu tumchgue amekuwa na kazi ya kuitetea serikali tu hajawahi hata siku moja kututetea sisi tuliomchagua. Halifu mbaya zaidi hata akitokea mbunge mwingine akatutetea yeye husimama na kuomba mwongozo na kuomba hoja ya mtetezi huyo iondolewe huwa simwelewi kabisa MBUNGE WANGU NI LUKUVI LIWALO NA LIWE:lock1:
 
Sisi wakwetu Anna kilango malechela ashatuaga tangu alipo rudi kushukuru wapigakura wake walio msaidia kuiba kura kasema harudi tena namnukuu kwa watu walio karibu naye"Hapa sigombei tena kama nitashidwa kutekeleza haya mambo nilio waahidi."Ametudanganya kwa miaka 10 kwa saund ya kiwanda cha tangawizi feki ambacho ninyumba ya mtu ambayo ndani haina hata mashine moja hilo amesanukiwa halisemi tena.Tuka tegemea ahadi ya Jk ya kutengeneza barabara ya Same kisiwani gonja mpaka mkomazi hili ndo watu waliamini wakampa kura mpaka leo hakuna lami wala moramu ni mahandaki kwa kwenda mbele hivyo kutokana na mambo hayo ana kilango kwaheri yakuonana.
 
Mbunge wangu asiendelee tena,ni mtendaji mzr lkn hana nguvu tena ya kuhimili siasa ya kishindani.ni muda wa kupisha wengine
SABABU:
Umri wake umesogea sana(mzee) Huyo ni Ndesamburo
 
Mbunge wa Bukoba vijijini Mh Rweikiza hajawafanyia lolote wapiga kura wake,anachowakirisha bungeni anakiju mwenyewe,hakuna wilaya yenye matatizo kama hiyo,njaa imeikumba sababu ya mnayuko na udongo kuchoka,vijana jobless wameongezeka kwa kasi sana na wengi wamekata tamaa ya maisha hakuna anayewasaidia kuwawezesha angalau waigie kwenye kilimo chenye tija au biashara,wilaya aina hata kisima kimoja,mito mingi ya asili imekauka,maeneo mengi ndoo ya maji ni kati ya sh 400 na 500 kutegemeana na kama yameletwa na pikipiki,baiskeli au kichwa,wakina mama na vijana wanatumia muda mrefu kwenda kutafuta maji na hivyo kuathri shughuli za maendeleo,sasa hivi wanaomba mvua inayoendelea isiishe kwani imewapunguzia gharama za maji.
Yote hayo mbunge hayajui,yuko anakula nchi Dar na Dodoma na akija mara chache ni kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya shule yake na kuwanunulia wazee walafi Rubisi huku wakimuhakikishia kuwa mpinzani wake bado hajazaliwa.Lakini asisahau kwa Bukoba vijijini ni nadra sana mbunge ku serve terms mbili.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom