Mkikimkiki: Mdahalo wa Utaifa(Sera za vyama) leo Agosti 30, 2015

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Habari wakuu,
Kuelekea uchaguzi mkuu October 25, leo kuna mdahalo kwa vyama vya siasa juu ya utaifa(Ilani za vyama). Mdahalo huu utakuwa na wawakilishi wa vyama vya siasa nchini ambapo Samson Mwigamba atawakilisha ACT wazalendo, Ndelakindo Kessy atawakilisha NCCR-Mageuzi, Jacob Samuel atawakilisha ADC na Rajab Hozza atawakilisha UPDP. Mdahalo huu pia utarushwa na kituo cha televisheni cha Star TV na kusikika radio free Africa. Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojadiliwa ukumbi wa JNICC Dar es Salaam.
==========

Maria Sarungi .jpg

Wameanza na wameonyesha uchambuzi kwa ujumla, sasa mdahalo unaanza na kila mshiriki anapewa dakika nne kujibu swali la kwanza na baadae ya dakika mbili kila mmoja.

Hozza(UPDP): Mimi ni mjumbe wa halmashauri kuu UPDP, sehemu alipozaliwa mtu ndio asili ya taifa hilo. Mtu wa wa Kenya anaweza kuchukua uraia wa Tanzania lakini akawa si mtaifa wa taifa hilo. Utaifa ni asili ya ulipozaliwa au wzazi wako walipozaliwa.

Ndelakindo Kessy(NCCR):
Mtanzania linatokana na neno Tanzania, Tanzania ni eneo lenye watu, ardhi na mamlaka, ni eneo linalotokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Raia wa Tanzania kulingana na katiba aidha amezaliwa au amejiandikisha.

Mwakatobe(ACT): Ni mojawapo ya swali jepesi, ni mwananchi mwenye uraia wa Tanzania. Eneo la kijigrafia linaitwa nchi na kwa Tanzania ni ndani ya mipka ya iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar. Mtanzania ni raia au mwananchi anaetokea Tanzania.

Jacob Samwel(ADC): Mtanzania ni mtu ambae anakaa ndani ya mipaka ya nchi ambazo zamani zilikuwa zinaitwa Tanganyika na Zanzibar, unapokuwa mtanzania unaunganishwa na sheria. Mwananchi wakati huohuo atakuwa na wajibu wa kuilinda nchi yake. Leo tunaishi katika mfumo wa kijamaa wa kisasa na vinakwenda pamoja na mfumo wa kijamaa. Hili limesababisha baadhi ya watu kuishi maisha ya kijamaa na wengine kibebari, hii imesababisha kujenga chuki kwa wanaishi maisha ya kijamaa dhidi ya wanaoishi maisha ya kibepari.

SWALI: Watanzania tunajivunia umoja na mshikamano, hakuna pengo kubwa kati ya masikini na matajiri, tunajivunia hatuna mpasuko. Hii ni kweli?

ADC: Hili si kweli kwa sababu kuna ukandamizaji ndani ya nchi, hata maji ya kunywa ni matatizo, kila kitu nchi hii ni matatizo. Wakiingia viongozi kwa mfumo huu huu kutatokea mpasuko.

Ndelakindo: Itikadi ni utu, utu ni umuhimu wake. Misingi ya utu kuna imani, mahali popote kwenye matabaka ya watu, katika umasikini ule utu haupo, kutogawana keki sawa.

Mwakatobe: Sasa hivi hatupo kwenye dalili, tupo kwenye hali halisi ya mpasuko, watanzania ni wavumilivu mno. Kuna nchi hata wakiongeza hata shilingi 50 kwenye mkate, hawataki. Hofu yangu ni pale watakapokoma na kuvumilia zaidi, dola inapaswa na wananchi na sisi ACT Wazalendo tunasema utaifa kwanza, vyama na ubinafsi baadae.

ADC: Katika chama chetu tuna itikadi ya haki kwa maana ya haki sawa kwa wote, kugawana fursa sawa, upendeleo sawa, kugawana mzigo wa taifa sawa. Mfano unaweza kuingia katika ofisi na kukuta kabila moja 30 na kabila jingine hakuna hata mmoja. Tugawane rasilimali za nchi sawa ili kulinda umoja wetu.

Tanzania ni muungano wa TZ na Zanzibar, na katika bunge la katiba kulikuwa na mpasuko, Je chama chako kina maoni gani kuhusu muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar.

UPDP: Ulianza vizuri kwa sababu ulianza na vitu flani, lakini baadae mambo yakaongezeka. Mzee Warioba alikusanya maoni na kupeleka bungeni, chama cha UPDP ulisamama katika serikali tatu, UPDP mwakilishi wetu Dovutwa alibaki baada vyama vikubwa kutoka, nyani akaachiwa shamba na kurudi kwa serikali mbili.

NCCR: Kulikuwa na mchakato wa kutengeneza rasimu ya pili ya katiba, kuna process huwezi kurudi nyuma. Kwa hivyo swala hili halipo tena kwa chama cha NCCR mageuzi kinasimami nini maana ipo chini ya mikono ya wananchi.

Mwaktobe: Kama mwenzangu alivyotangulia, muundo unaendelea uleule wa serikali mbili kwa katiba ya 1977. Ninachoamini mimi ni mahusiano mazuri iwe serikali moja au mbili, ningependa nchi yetu iwe na Afrika moja. Ukiunganisha vitu viwili huwezi kupata tena vitu viwili, ama kimoja au zaidi ya viwili.

ADC: Huu si muungano wa haki, Zanzibar uhuru wake ni nusu lakini Tanganyika haionekani popote, Tanzania ana uhuru wake asilimia 100 na Zanzibar inao wake asilimia 50%

Swali
Dr. Mlaga: Je swala la maadili limepewa uzito unaostahili katika bunge maalum la katiba?

Ndelakindo: Haya yalikuwa maamuzi ya waliokuwa mle tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha, limetupwa katika rasimu iliyowakilishwa kwa rais

Mwakatobe: Nilipinga sana, haiwezekini zaidi ya nusu ya wajumbe wawe wabunge halafu wakajitungie maadili, huu ni mgongano wa kimaslahi. Maana ya maadili ni matendo mema, ukitaka kuwa kiongozi lazima uwekewe mipaka.

Jacob: Utaifa wetu unatengenezwa na katiba, katiba tuliyokuwa tunaitumia haitokani na watu.

Rajab: Bunge la katiba, lilikuwa wabunge wasiwepo, wawe watu wapya, walivyokuwepo wale wabunge ndio mambo yote yaliyotokea. Wamevibakiza vitu vyenye maslahi yao. Maadili ya kumwajibisha mbunge ilikuwa ni sahihi, hii katiba iliyokuwepo ni nadharia hivi sasa, ikipita ni ileile maana hamna mabadiliko makubwa. Rais atakaechaguliwa aanze mchakato upya.

Msosa(Mwanafunzi): Kwa kuwa Tanzania ni taifa la vyama vingi, kwenye vyama kuna watu wenye dini mbalimbali, haitaleta madhara yoyote?

Mwakatobe: Mimi ni mkristo, nimesoma na waislamu. Mtu unamweka mbele mwenzako kuliko imani yako. Niwapongeze waislamu, wakristo na dini nyingine. Katiba yetu inatupa uhuru wa mawazo, taifa letu kwanza ndilo linalotuunganisha. Taifa kwanza, mwenzako kuliko imani zetu, imani pia zinajali wengine

Jacob: Chochote unachokifanya lazima ukitenganishe na dini

Ndelakindo: Katika katiba kuna uhuru wa kuabudu, chama cha siasa hakiwezi kukubalika kama hakijasajiliwa. Hakuna chama cha siasa kinachoweza kusajiliwa kama kinafata udini. Sioni kama kuna tatizo lolote.

Rajab: Udini katiaka taifa letu, wakristo na waislam tumekaa muda mrefu. Kuna tatizo hilo kwa watawala, waislamu waliomba kwa baba mahakama ya kadhi lakini upande wa pili walikuwa wanajibu kuliko baba, naomba serikali inayokuja isifumbie macho, kama mtu anamuomba baba, wewe hauna mamlaka ya kuingilia, hii ni tahadhari muifanyie kazi.

Swali
Erick Edward: Vyama pinzani vimependekeza serikali tatu, je vikiingia madarakani je kutakuwa na marekebisho katika katiba iliyopendekezwa.

Joel: Kwa sababu Tanzania inatokana na muungano wa nchi mbili, Bara ni unitary state. Muungano utakaofaa kabisa ni wa serikali tatu kwa maana ya federation, huu ndio muundo ambao nafikiria kwa chama chetu cha ADC unafaa.

Mwakatobe: Kulingana na katiba, mpaka sasa hakuna muungana wa chama cha siasa lakini unaweza kumuunga mwenzako mkono. Hakuna mseto kama walivyo Kenya kwa hio tunalo hilo tatizo, ningependa sana tuwe na serikali moja tu. N avyote tuvifute hata Afrika ningependa iwe moja, hata hivyo serikali tatu zina uwazi zaidi.

Ndelakindo: Kila chama ni chama pinzani, hakuna chama chenye mamlaka ya kubadili katiba, katiba ni mamlaka ya wananchi. Hata serikali wenyewe hwana mamlaka ya kubadili katiba.

UPDP: Kma itaingia madarakani, lazima ifanye mchakato wa kuwauliza wananchi te, hii iliyokuwepo ina malalamiko mengi, kama ikiingia madarakani itaanza mchakato wa kuwauliza wananchi upya.


Swali
Lusako: Waumini wa serikali tatu, TZ ni muungano wa Tanganyika na Znz, Je Tanganyiaka yetu inatetewa na mwanasheria gani

Mwakatobe: Ndio mkanganyiko mkubwa kama nilivyosema awali, huwezi kuunganisha vitu viwili upate viwili. Malalamiko ya wazanzibar wanasema Tanganyika imejificha nyuma ya Tanzania. Waziri mkuu anashughulika na Tanzania bara tu, hawezi kuvuka Zanzibar hata Rais huwa havuki kule na sisi chama chetu kinatetea Zanzibar.

Rajab: Mwanasheria wa Tanganyika hayupo kwa sababu wamefunikwa na shuka la Tanzania, watu wanataka serikali tatu ili kila mtu ajitegemee alafu kuwepo na kitu cha kutuunganisha. Hawa wanaozaliwa hawajui mambo ya muunganiko, sehemu inayostahili ifanyiwe kazi kuliko kusubiri watu wawe wengi.

Kessy: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa ni muungano wa maridhiano hivyo muungano uliopo ulifikiwa kwa maridhiano, lakini sasa una dosari, tukaona itasuluhishwa na katiba mpya.

Samwel: Nilisema aina hii ya muungano ni mbaya kwa sababu haitendi haki kwa sababu inaifanya Zanzibar kuwa koloni la Tanganyika, Zanzibar ianpoteza uhuru wake kwa sababu haina mambo yake ya nje, imechukuliwa na Tanganyika

Swali
Suleyman: Mkataa kwao ni mtupwa, je uraia wa nchi mbili utaua uzalendo?

Rajab: Mimi siafiki uraia wa nchi mbili kwa sababu kila kitu kina asili yake, mtu atakuja kufanya kazi hapa, atafanya mambo flani atakimbili uingereza, wewe huwezi kumrudisha kwa sababu ana uraia wa Uingereza. Utakuaja kutudhoofisha kwa mambo yetu ya kinchi

Ndelakindo: Kulikuwa kuan mchakato wa katiba, inaonekana wazo hilo japo lilitolewa halikukubalika. Ukitazama katika dunia yetu kuna mataifa machache ambayo yanahesabika developed, itapofikia hamna tofauti sana kati ya mataifa labda itakuwa na umuhimu.

Mwkatobe: Nzalendo hata kama hana uraia ana mapenzi kwa nchi yake ya asili, raia wa nchi moja tunaona wanavyokufa kwenye bahari ya nchi ya mediteraniani, nchi inajengwa na wenye nchi yetu. Baadhi wanahitaji uraia wa nchi mbili ili watumie fursa, sioni tatizo.

Jacob: Tumesaini mkataba wa kimataifa, uraia wa nchi mbili au tatu hauzuiliki.

Swali
Makuka(Mwanza): Utafanya nini kuhahakikisha kila mtanzania anakua mzalendo na kujivua kuwa mtanzania kama huko nyuma

Jacob: Kwanza haki ni kitu cha msingi, kwa mfano hatugawani rasilimali sawa, siku zote atakuwa na malalamiko, tunatakiwa tupate sawa rasilimali.

Mwakatobe: ACT tunapigania kurudisha misingi aliyoiasisi Nyerere, azimio la Arusha lilikuwa na misingi ya nchi. Watu waliletwa pamoja na azimio la Arusha. Sasa kuna mpasuko kwa baadhi ya watu kujiona wenye nchi, lazima tuwe na haki sawa. Vipi mkulima anaelima kuanzia kijana mpaka kuzeeka kuilisha nchi.

Kessy: Jambo hilo haliwezekani kwa kila raia kuwa nzalendo, ndani ya Marekani hawataki watu hata kuitwa wamerakani, ni kumuelimisha mtanzania kujua yeye ni mtu gani. Hili ni swala la binafsi ila kwa ujumla lazima tuelimishane.

Rajab: Uzaledo umevunjika hivi sasa kwa sababu ya uonevu, weka haki.


Rajab: Katiba iiyopendekezwa, kama watu wanataka ukweli. Kama itatumika nguvu kura ya maoni, naomba wananchi tuipigie hapana, malalamiko bado yako palepale ukipita.

Kessy: Katiba kutengeneza ni mchakato, kwa muda waliojiweka lazima tungaeenda kwenye kura ya maoni, bunge lijalo lipiteshe kani jinsi gani watamalizia jambo lile. Naamini bunge lijalo litaendeleza pale palipokuwa pamefikiwa kwa sababu kuanza mchakato upya huo ni gharama kubwa.

Mwakatobe: Mimi niliona ile rasimu ni lumbesa kweli, katiba hata ingikuwa na page 20 zinatosha tu, ule ni muongozo tu. Maamuzi ya wengi ndiyo tunayokwenda nayo hata kama sio kama mnavyofahamu demokrasia.

Jacob: Msimamo wa chama changu upo katika ilani, tumeeleza namna ya kufanya marekebisha yote. Watanzania wengi huwa hawaangalii walipojikwaa, wanaangalia walipodondokea, marekibisho makubwa yatakuwa kwenye serikali.

Tanzania ni nchi yenye rasilimiali nyingi, Je ni jitihada gani mtazifanya watanzania kunufaika na rasimali hizo

Kessy: Sio kwamba hazitumii, sisi sote hatuwezi kwenda kwenye machimbo, kama hatuwezi kuona tumejaaliwa tumekosa maarifa, hivyo tatizo ni rasilimali watu pia rushwa na ufisadi. Hatujaweza kuweka mfumo wa kushirikiana na nchi nyingine kupambana na ufisadi mkubw.

Mwakatobe: Rasilimali za nchi yetu zinatumika kutajirisha watu wengine badala ya nchi yetu, inauma. Katika ilani yetu kuna uchumi shirikishi, lazima kila mtanzania hata wa chini ashiriki, sisi tuna watu wasomi, kuna watu tunawaita ni wawekezaji, si wawekezaji, ni waporaji.

Rajab: UPDP sera yake ni ardhi na hizi rasilimali nyingi zipo kwenye ardhi na sera ya ardhi haijakaa vizuri. UPDP ikipata madaraka aradhi itatoka kwa serikali na kumilikiwa na mwananchi. Serikali haifanyi biashara, mwekezaji akija atakuwa na mkutano na wananchi, itakuwa mkataba maalum kati ya wawekezaji na wananchi.

Samwel: Katika ilani yetu tutafanya marekebisho katika serikali,mfumo umefanya mali zote za umma na mikataba yake kuwa siri yake yenyewe.

Rwegasira: Ili kudumisha uzalendo unadhani kuna haja ya kuwa na chama kimoja?

Samwel: Mfumo wa chama kimoja ni mfumo wa kukomunist, ukitoka katika mfumo huo, mifumo mingine yote inaruhusu vyama vingi. Vinampa mwananchi uwezo wa kuchagua.

Mwakatobe: Uhuru wa mawazo ni jambo muhimu sana kwenye katiba, unaweza kuwa na watu wenye fikra tofauti lakini wafanye kazi moja, sisi tunaunganishwa na vitu vingi tukiwa watanzania kuliko vinavyotutengenisha.

Kessy: Hatujaweza kufafanua uzalendo maana yake nini, sisi tunafata demokrasia ya vyama vingi, maamuzi ya kuchagua vyama vingi yalikuwa maamuzi ya wengi. NCCR na UKAWA tunakubaliana katika utu.

Rajab: Haina haja ya kuwa na chama kimoja, uzalendo ni watawala kuwawekea watu misingi.

Swali: Historia haijafundishwa kwa uwazi na ukweli, mtaboreshaje ufundishaji wa historia ya nchi yetu

Rajab:
Hata mimi nashangaa historia inaanzia 1961, kuna vitu vimefichwa kuanzia 61 kurudi nyuma. UPDP ingiingia madarakani lazima ianzie nyuma.

Kessy: Wamafunzi wanajifunza si kwa ajili ya kupenda, kumtakana baba wa taifa au mwingine yoyote ni swala la maadili. Kumtukana mtu mwengine sio utu.

Mwakatobe: Tuna mambo mengi mazuru, je vimeingizwa kwenye mtaala, kwa niaba ya chama changu tutaiweka misingi katika mtaala hata familia.

Swali: Vyama vya upinzani vumebomoa utaifa kwa kutafuta madaraka yoyote, uzalendo wao uko wapi

Samwel: Tatizo lipo kwenye dola, vyombo vya dola vinajenga uadui na wananchi, chama ambacho kinatawala kizangatie haki.

Mwakatobe: Uzalendo ni kwa ajili ya watu wa nchi yako, mtu anaweza kuwa na maoni mazuri sana lakini kwa sababu tu ni CCM anapingwa, mtu anaweza kuwa na hoja nzrui sana lakini akapingwa kwa sababu tu ni upinzani. ACT wazalendo tutasimamia haki hata tukibaki wachache.

Kessy: Hatujaweza kuweka sawa maana ya uzalendo, maana ya chama pinzani! Serikali ina mamlaka kwa vyama vinavyoharibu uzalendo kufutwa.

Rajab: Chama kilichopo madarakani kinajaza watu hofu, tuondoke kuwa wanachama wa kadi na kuwa wanachama wa maendeleo na chama chochote kipo kisheria kushika madaraka.

Sarungi: Niwashukuru watazamaji na wasikilizaji wote kwa kuwa pamoja nasi na naomba kuwakumbusha kwamba wiki ijao mdahalo wetu utakuwa unaendelea Zanzibar ambapo tumeshaomba vyama hivi vitano viweze kutoa wagombea wao wa Urais kwa upande wa Zanzibar, hivyo tunawakaribisha muendelee pia kutuma maswali yenu kwa wagombea hawa ili tuweze kuwauliza.

Tuwahoji, tuwapime, tuwachuje.
 

Attachments

  • DSC03045.JPG
    DSC03045.JPG
    1.2 MB · Views: 32
  • Washiriki wa mdahalo huo.jpg
    Washiriki wa mdahalo huo.jpg
    54.7 KB · Views: 31
Back
Top Bottom