Background Check
JF-Expert Member
- Jun 28, 2019
- 378
- 578
Ndugu zangu watanzania,
Nafahamu mifumo imetutenga katika makundi tofauti ili mifumo hiyo iweze kututawala 'DEVIDE AND RULE'.
Nafahamu kuwa tulikuwa wamoja hadi pale vyama vya siasa vilipo tutenganisha. Utasikia "Wewe ni mwanachama wa Chama gani?" Huyu atasema ni 'CCM damu damu', na yule atasema 'CHADEMA kindakindaki' na mwingine atasema hana Chama Ilimradi tu asikose upande.
Tulikuwa wamoja hadi pale dini na mitazamo ya kiimani ilipotugawa katika makundi. Wale wanaamini katika kuoshwa kwa damu ya Muisraeli ama wale wanaoenda kusimama katika uwanja wa Arafa, mmoja akisema Asalam Alekmu, mwingine atasema Bwana Yesu asifiwe.
Tulikuwa wamoja hadi pale elimu ilipotugawanya (si unakumbuka marafiki zako mliosoma wote shule ya msingi, shule ya upili hata chuo), bila shaka mmepotezana kitambo kirefu hata kujuliana hali kwa simu, hilo halipo. Shahada na Stashahada zimetugawa pia. Ujinga na welevu.
Tukaendelea kuwa wamoja hadi pale makabila, ukanda ulipochukua jukumu la kutugawanya. Mimi mkwere ni mjanja wa kuzaliwa na kukulia mjini, utanambia nini wewe musukuma mshamba wa kijijini. Mara mimi ni mtu wa bara wewe ni mtu wa visiwani, utasikia ukanda wa pwani umetoa mawaziri wengi kuliko ukanda fulani.
Bado hadi michezo nayo ikaona tukiendelea kuwa wamoja tutafaidika saaana! ikatugawa, utasikia: "Wewe ni shabiki wa timu gani", yule atasema ni Simba na yule atasema ni Yanga kila mtu atachagua upande anao amua kusimama nao, ukifungwa unanuna.
Pesa hapa sasa usisema, pesa imetugawanya hadi mbele ya ndugu zetu ya damu bado imeonesha tofauti zetu. Umasikini na utajiri umetuchambua tukachambuka.
Yote hayo nimeeleza kuonesha tofauti zetu zilipo, sijasema tofauti hiyo ni mbaya laaahasha!. Nimeandika ili tuweke tofauti zetu kando, hasa imani kwa vyama vyetu, ukanda na mitazamo yetu tuziweke kando, hasa katika kipindi hiki kuelekea chaguzi za serikali za mitaa, na mwaka ujao katika uchaguzi mkuu 2025 wa Diwani, Mbunge na Rais.
1. Naomba tuchangie ni kwa namna gani serikali iboreshe huduma za jamii na kuleta mabadiliko na maendeleo chanya?.
2. Ni taasisi gani, au shirika la umma linahitaji maboresho, na ni maboresho ya namna gan?
3. Ni mambo gani unapendekeza yawekwe kwenye Ilani ya chama chochote kina hitaji kuwani kuongoza dola? (Ni imani yangu wanaoandika ILANI huwa wanapita na kwenye jukwaa hili la siasa.
Tuweke tofauti zetu zote pembeni, tuamue kuwa wamoja kwa mstakabali mpana wa taifa letu tukufu la Tanzania.
Naam,
Machepele Tanzania,
Dar es Salaam - Tanzania.
Agosti 26, 2024.