To Mbowe and Slaa: Mtwara magamba mmewashika pabaya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

To Mbowe and Slaa: Mtwara magamba mmewashika pabaya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ebaeban, Jun 4, 2012.

 1. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Huko kusini hususani Mtwara ndio ufisadi ulikojaa, kwa hiyo magamba mmewakamata kweli kweli k.m Newala ndiko kuna magodowm ya korosho alishauziwa Kalamagi siku nyingi, viwanda vidogovidogo vya kubangua korosho vilivyopo Mtwara mjini waliisha wahi wajanja nashindwa hata kuwataja na mashine wamehamishia sehemu nyingine, wakati Murji akiwa mbunge Newala na mwenzie Dr Alex Khalid walijaribu kulizungumzia hili la kuhujumu miundo mbinu ya korosho matokeo yake Murji akapigwa ban na magamba wenzie amesota weeee ndio mwisho akahamia kugombea Mtwara mjini nako amehonga karibu miaka miwili. Mbaya zaidi bandari ambayo ilikuwa imeajiri wamakonde wengi nayo imeuzwa kwa hio huko magamba hawana ujanja mmewakamata pabaya. Kielelezo cha umaskini wa Mtwara wambieni waende Mtwara maeneo ya magalani kuna kiwanda cha kubangua korosho cha wahindi lile jingo lilikuwa la mamlaka ya korosho ndani yake akina mama kama 2000 wameajiriwa wanabangua korosho kwa kutumia mikono na vimashine Fulani vya miguu sasa kawaangalie mikono ilivyoliwa na mafuta makali ya korosho lazima yeyote mwenye huruma atawahurumia sana kwa sababu risk ni kubwa malipo ni kichekesho niliacha wanapewa elfu 4000 kwa siku na wanalipwa jumamosi sh 28,000 elfu Kazi hiyo akina mama a Mtwara mjini hawaitaki kabisa wanachofanya wale wahindi wameweka mawakala kuwatafutia nguvu kazi toka vijiji jirani kama Ziwani, Msangamkuu, Naliendele , Moma nk kwa hakika mpaka uwe maskini wa kutupwa ndo kazi ile utafanya. Ninachowaombeni makamanda wakati mnawajuza wananchi au mnapowafungua macho msiseme kwa ukali na kuonyesha hali ya jazba kwani kufanya hivyo magamba wataogopa kwa hiyo hata mkishinda hawatawapeni nchi maana wataogopa mtawakamata watasema tu wacha liwe litakavyokuwa inaweza kuishia kama ya BAGBO wa Ivory Coast, punguzeni ile hali ya munkali. Ushauri wangu ndio huo. CHADEMA KAMATA MWIZI MEEEEN.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nuru ndio hivyo imeingia inabidi tuilinde kwa nguvu zote ili tusirudi gizani tena.
   
 3. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  upo sahìhi mkulu wane naheshimu sana vichwa vyenye kuangalia matatizo yetu kwa karibu respect to yo. Na yale ya ivory kost aina haja ya kuyaogopa hakuna haki iliyosimama hapa duniani bila ya damu yetu sisi wanadamu kumwagika sisi ndo Mungu alituumba tuwe juu ya viumbe wote isipokuwa yeye na akatupa utashi haya mambo yafanywayo na sisiem sio kwamba hawezi kuyageuza lah ila ametuachia sisi sababu ametupa akili ili sio kila kitu tumlaumu yeye kwahiyo kazi ya kuyapiga magamba chini bila ya kuogopa sijui ya Gagbo ni yetu wale wachache ambao wamepewa akili lemavu kidogo zimepungua ndo utawaona wanashobokea magamba. Eeh MUNGU tunaomba msaada wako ili haya mapambano yaishe salama ameen
   
 4. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Teh teh teh!
   
 5. m

  mtukwao2 Senior Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :evil::evil::evil::crazy:
   
 6. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Si Mtwara pekee yake wafikie mpka Tunduru kuangali jinsi siasa inavyofanya kazi kuchezea maisha ya watu.Suala la kutokuuzwa kwa korosho ni maamuzi ya kisiasa.Wananchi wanataabika korosho zimehifadhiwa kwenye maghala.Alikwenda MMarekani mmoja akaahidi kununu akorosho za Tunduru lakini naye ameingia mitini.

  CDM msiishiye kuwa elimu ya uraia tu,ongeni na wanunuzi wakubwa wa korosho duniani kuinusuru hali iliyo wakumba wenzet toka kusini,hapo mtakuwa mmegusa na kukonga nyoyo za wanyonge.Kwan wananchi wanaamini ninyi ndio pambazuko jipya wenye kukerwa na matatizo ya wananchi yaliyosababishwa kwa makusudi kwa maaamuzi ya kisiasa zaidi.
   
 7. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Mimi kuna picha nimeona kwenye tanzania daima uk wa mbele mwenye ujuzi atuwekee humu,mbowe akila ugali na raia nimeipenda sn.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hawa ndugu zetu lazima twende nao pamoja maana wameteseka sana na blah blah za viongozi wetu
   
Loading...