Mama yangu alikuwa
akinipenda sana, labda hii kwa
sababu nilikuwa ni mtoto
pekee katika maisha yake.
Baba yangu hakuwepo
duniani, tayari alikuwa
amekwishafariki kitambo
sana. Pamoja na mapenzi
makubwa ambayo alikuwa
akinipa, kiukweli sikumpenda
kabisa mama yangu.
Nilimchukia sana tena naweza
kusema kwamba nilikuwa
nikimchukia kuliko hata
nilivyokuwa nikimchukia
shetani. Mama yangu
hakulijali hilo, kama mtoto
wake bado alikuwa akinipa
mapenzi ya dhati kama mtoto
wake.
Mama yangu alikuwa na
kasoro moja mwilini mwake,
hakuwa na macho yote
mawili, alikuwa akitumia jicho
moja tu kuonea. Katika
upande ambao haukuwa na
jicho, sehemu hiyo ilikuwa
ikijaa uhafu sana jambo
ambalo lilinifanya hata
kumuogopa kumuangalia.
Mama alikuwa akipenda
kuniona nikipata kila
nilichokuwa nikikitaka, kuna
siku akaamua kuniuliza ni kitu
gani ambacho angependa
kitokee ili niwe na furaha
zaidi, nilichokijibu,
nikamwambia kwamba kama
angekufa basi ningekuwa na
furaha kubwa maishani
mwangu.
SIKUMPENDA mama yangu,
nilimchukia sana japokuwa
alikuwa amenisomesha sana.
Nilipomaliza chuo,
nikabahatika kuhamia nchini
Kenya huku nikimuachia
nyumba ambayo tulikuwa
tunakaa. Toka nilipohama
ndani ya nyumba hiyo,
sikuwahi kuwasiliana nae hata
siku moja ingawa miaka
mitano ilikuwa imepita.
Ningewasiliana nae vipi na
wakati sikuwa nikimpenda?
Kuna siku akaamua kuja
kunitembelea Kenya.
Alipogonga mlango, mtoto
wwangu wa kwanza, Keneth
akaenda kufungua mlango,
mara nikasikia akianza kulia
kwa sauti kubwa, alipokuja
mtoto wangu wa pili, nae
akaanza kulia.
Kwa haraka haraka nikatoka
chumbani na kwenda kuona
kitu gani kimetokea,
nilipoufungua mlango,
nikamkuta mama yangu
ambaye akaachia tabasamu
pana baada ya kuniona.
"Umefuata nini?" Nilimuuliza
mama yangu na kuendelea.
"ONDOKA. Unawatisha
watoto wangu" Nilimwambia
mama yangu kwa ukali huku
nikifunga mlango. Tundu la
jicho lake lile ambalo lilikuwa
wazi ndilo ambalo lilionekana
kuwa kama kinyago.
Kwa sababu mvua ilikuwa
ikinyesha, mama yangu
akaondoka. Sikujua
angekwenda wapi, sikujua
angelala wapi na wakati
kipindi hicho kilikuwa ni usiku
wa saa tatu. Alichokifanya,
akaondoka na kupotelea
ndani ya jiji kubwa la Nairobi.
Baada ya mwaka kuisha
nikapewa taarifa kwamba
mama yangu alikuwa
amefariki dunia. Huku
nikijifanya kuwa na mapenzi
ya kinafiki nikaelekea Dar es
Salaam tena huku nikiwa
nimechelewa makusudi ili
nisiuzike mwili wake.
Nilipofika, majirani
wakanigawia barua ambayo
alikuwa ameiacha mama
yangu kwao, barua hiyo
iliandikwa hivi.
Kwako mwanangu mpendwa,
Antony.
Najua kwamba ulikuwa
haunipendi kabisa lakini mimi
kama mzazi niliamua
kukupenda kwa moyo wa
dhati. Ulikuwa ukipenda sana
nife na ninaamini kwamba
kwa sasa utakuwa
umefurahia. Nilikujali na
kukupenda kama mwanangu
mpaka siku ya mwisho kuingia
kaburini.
Nilipokuja nchini Kenya
kukutembelea, ukanifukuza
kwa sababu tu nilikuwa
nikiwatisha watoto wako
kutokana na jicho moja
ambalo nilikuwa nalo.
Nikaondoka nyumbani kwako
huku mvua ikinyesha, sikutaka
kutamka neno lolote baya
kwako, niliondoka nikiwa
ninatabasamu tu.
Ila naomba nikuambie kitu
kimoja Antony. Katika kipindi
ambacho ulikuwa mdogo,
ulipata ajali ambayo ililifanya
jicho lako kutoboka. Sikutaka
ukue na kuiona dunia kwa
jicho moja, nilichokifanya ni
kulitoa jicho langu na kisha
kuwekewa wewe hospitalini.
Nilitamani sana ukue na
uweze kuuona ulimwengu
huu kwa macho mawili,
sikujua ni kitu gani ambacho
kingenikuta baadae kitu
ambacho nilikijali kwa wakati
huo ni kukuona ukiwa na
macho mawili tu.
Ninakupenda Antony, na kila
siku nitaendelea kukupenda.
Baki salama na uwapende
zaidi watoto wako kama
nilivyokupenda.
Regina.
akinipenda sana, labda hii kwa
sababu nilikuwa ni mtoto
pekee katika maisha yake.
Baba yangu hakuwepo
duniani, tayari alikuwa
amekwishafariki kitambo
sana. Pamoja na mapenzi
makubwa ambayo alikuwa
akinipa, kiukweli sikumpenda
kabisa mama yangu.
Nilimchukia sana tena naweza
kusema kwamba nilikuwa
nikimchukia kuliko hata
nilivyokuwa nikimchukia
shetani. Mama yangu
hakulijali hilo, kama mtoto
wake bado alikuwa akinipa
mapenzi ya dhati kama mtoto
wake.
Mama yangu alikuwa na
kasoro moja mwilini mwake,
hakuwa na macho yote
mawili, alikuwa akitumia jicho
moja tu kuonea. Katika
upande ambao haukuwa na
jicho, sehemu hiyo ilikuwa
ikijaa uhafu sana jambo
ambalo lilinifanya hata
kumuogopa kumuangalia.
Mama alikuwa akipenda
kuniona nikipata kila
nilichokuwa nikikitaka, kuna
siku akaamua kuniuliza ni kitu
gani ambacho angependa
kitokee ili niwe na furaha
zaidi, nilichokijibu,
nikamwambia kwamba kama
angekufa basi ningekuwa na
furaha kubwa maishani
mwangu.
SIKUMPENDA mama yangu,
nilimchukia sana japokuwa
alikuwa amenisomesha sana.
Nilipomaliza chuo,
nikabahatika kuhamia nchini
Kenya huku nikimuachia
nyumba ambayo tulikuwa
tunakaa. Toka nilipohama
ndani ya nyumba hiyo,
sikuwahi kuwasiliana nae hata
siku moja ingawa miaka
mitano ilikuwa imepita.
Ningewasiliana nae vipi na
wakati sikuwa nikimpenda?
Kuna siku akaamua kuja
kunitembelea Kenya.
Alipogonga mlango, mtoto
wwangu wa kwanza, Keneth
akaenda kufungua mlango,
mara nikasikia akianza kulia
kwa sauti kubwa, alipokuja
mtoto wangu wa pili, nae
akaanza kulia.
Kwa haraka haraka nikatoka
chumbani na kwenda kuona
kitu gani kimetokea,
nilipoufungua mlango,
nikamkuta mama yangu
ambaye akaachia tabasamu
pana baada ya kuniona.
"Umefuata nini?" Nilimuuliza
mama yangu na kuendelea.
"ONDOKA. Unawatisha
watoto wangu" Nilimwambia
mama yangu kwa ukali huku
nikifunga mlango. Tundu la
jicho lake lile ambalo lilikuwa
wazi ndilo ambalo lilionekana
kuwa kama kinyago.
Kwa sababu mvua ilikuwa
ikinyesha, mama yangu
akaondoka. Sikujua
angekwenda wapi, sikujua
angelala wapi na wakati
kipindi hicho kilikuwa ni usiku
wa saa tatu. Alichokifanya,
akaondoka na kupotelea
ndani ya jiji kubwa la Nairobi.
Baada ya mwaka kuisha
nikapewa taarifa kwamba
mama yangu alikuwa
amefariki dunia. Huku
nikijifanya kuwa na mapenzi
ya kinafiki nikaelekea Dar es
Salaam tena huku nikiwa
nimechelewa makusudi ili
nisiuzike mwili wake.
Nilipofika, majirani
wakanigawia barua ambayo
alikuwa ameiacha mama
yangu kwao, barua hiyo
iliandikwa hivi.
Kwako mwanangu mpendwa,
Antony.
Najua kwamba ulikuwa
haunipendi kabisa lakini mimi
kama mzazi niliamua
kukupenda kwa moyo wa
dhati. Ulikuwa ukipenda sana
nife na ninaamini kwamba
kwa sasa utakuwa
umefurahia. Nilikujali na
kukupenda kama mwanangu
mpaka siku ya mwisho kuingia
kaburini.
Nilipokuja nchini Kenya
kukutembelea, ukanifukuza
kwa sababu tu nilikuwa
nikiwatisha watoto wako
kutokana na jicho moja
ambalo nilikuwa nalo.
Nikaondoka nyumbani kwako
huku mvua ikinyesha, sikutaka
kutamka neno lolote baya
kwako, niliondoka nikiwa
ninatabasamu tu.
Ila naomba nikuambie kitu
kimoja Antony. Katika kipindi
ambacho ulikuwa mdogo,
ulipata ajali ambayo ililifanya
jicho lako kutoboka. Sikutaka
ukue na kuiona dunia kwa
jicho moja, nilichokifanya ni
kulitoa jicho langu na kisha
kuwekewa wewe hospitalini.
Nilitamani sana ukue na
uweze kuuona ulimwengu
huu kwa macho mawili,
sikujua ni kitu gani ambacho
kingenikuta baadae kitu
ambacho nilikijali kwa wakati
huo ni kukuona ukiwa na
macho mawili tu.
Ninakupenda Antony, na kila
siku nitaendelea kukupenda.
Baki salama na uwapende
zaidi watoto wako kama
nilivyokupenda.
Regina.