TMX na Baadhi ya Makatibu wa Vyama vya Ushirika (AMCOs) wanaigombanisha Serikali yetu kwa Wanachi kwa kutolipa pesa ya ufuta msimu 2020

Mkoko2020

New Member
Aug 17, 2020
1
0
Habari wakuu.

TMX ni moja ya shirika lililopewa dhamana ya kuwaingizia wakulima pesa zao baada ya mnada kufanyika na wafanya biashara kulipa pesa husika.

Ila tangu mnada wa mwezi July mpaka leo hii wakulima wengi wa mkoa wa Lindi na Mtwara hawajalipwa pesa zao na majibu hakuna. Hawa jamaa ni JIPU.

Makatibu wa AMCOs nao pia hushirikiana na TMX kuwadanganya wakulima. Hawa hawatoi taarifa sahihi muda wote. Pia hutoa data (idadi ya kilo) pungufu tofauti na uhalisia

Wenye dhamana shughulieni hali ni mbaya na wakulima wanateseka badala ya kunufaika na jasho lao.
 
Back
Top Bottom