TMAA timizeni wajibu wenu, njoo huku Babati muone sheria zinavyokiukwa

Triple A

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
766
148
Wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania TMAA
linajukumu la kudhibiti uchimbaji haramu na utoroshwaji wa madini ili wahusika wafuate taratibu na sheria ya madini ya mwaka 2010,

Sisi wenye leseni za uchimbaji madini ujenzi tunawaomba TMAA mje hapa Babati muone sheria zinavyovunjwa mchana kweupeeeeeeee!

Msibakie kukagua Tanzanite na almasi peke yake, kuna madini mengine yanahitaji kukaguliwa kama madini ujenzi ikiwemo mchanga mawe kokoto na morom!
 
Hueleweki mkuu, hebu eleza kinagaubaga usaidiwe, sheria gani zinavunjwa,na nani anaezivunja
 
Hueleweki mkuu, hebu eleza kinagaubaga usaidiwe, sheria gani zinavunjwa,na nani anaezivunja

sheria ya madini ya mwaka 2010 kile kifungu cha 18 msatari wa 2 inaeleza wazi kuwa hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuchimba au kusafirisha madini isipokuwa mwenye leseni,mimi na wenzagu tuna leseni za uchimbaji wa madini ujenzi kama mchanga,mawe na morom.
Cha kushangaza ni kwamba kuna wachimbaji haram wengi sana wasiofuata sheria,serikali haipati mrabaha na sisi wenye leseni hatunufaiki na uchimbaji wa aina hii,tunaiomba chombo chenye dhamana hii imulike na huku babati.
 
Wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania TMAA
linajukumu la kudhibiti uchimbaji haramu na utoroshwaji wa madini ili wahusika wafuate taratibu na sheria ya madini ya mwaka 2010,

Sisi wenye leseni za uchimbaji madini ujenzi tunawaomba TMAA mje hapa Babati muone sheria zinavyovunjwa mchana kweupeeeeeeee!

Msibakie kukagua Tanzanite na almasi peke yake, kuna madini mengine yanahitaji kukaguliwa kama madini ujenzi ikiwemo mchanga mawe kokoto na morom!
Nadhani ingekuwa ni vyema ukatoa taarifa kwa wa husika naamini ni waelewa sana na watalishughulikia vizuri tu.
 
kwa jinsi hali ilivyo hivi sasa,hakuna sababu ya kuwa na sheria ya madini, ningeomba mh rais afute tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom