TLP yaungana na CUF kuhusu Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TLP yaungana na CUF kuhusu Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 31, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  TLP yaungana na CUF kuhusu Katiba mpya

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 30th December 2010 @ 23:57 Imesomwa na watu: 86; Jumla ya maoni: 0
  JINAMIZI la kudai Katiba mpya limeendelea kutikisa ambapo sasa Chama cha Tanzania Labor (TLP), kimeungana na Chama cha Wananchi (CUF) kutaka kutokuwapo serikali mbili za Muungano na Zanzibar.

  Chama hicho kinataka Katiba mpya iruhusu serikali tatu badala ya mbili za sasa ambazo ni ya Tanzania Bara, Zanzibar na serikali ya tatu ya Muungano huku ikisema utaratibu wa sasa wa kutokuwa na serikali ya Tanzania Bara si haki.

  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Hamad Tao alisema chama chake pia kinataka Katiba hiyo iruhusu serikali ya mseto itakayoshirikisha vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi bungeni, kwa madai itasaidia kuondoa chuki kati ya vyama vya siasa na kujenga umoja na mshikamano ambao utaleta amani na maendeleo.

  Katika mapendekezo yao mengine, TLP inataka mawaziri wathibitishwe na Bunge lakini wasiwe wabunge, bali wataalamu katika fani zao ili kuondoa malalamiko kwamba mawaziri huteuliwa kirafiki.

  “Katika Katiba hiyo mpya, tunataka Tume huru ya Uchaguzi kwani iliyopo huteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama tawala na wakati wa uchaguzi hutokea pengine akawa mgombea,” alifafanua.

  Katika kuonesha kukerwa na ilivyo sasa, wagombea urais hawawezi kupinga matokeo ya kura za urais mahakamani, chama hicho kinataka hilo liruhusiwe endapo kama kuna utata sawa na ilivyo kwenye matokeo ya kura za wabunge.

  Tao alitaja mapendekezo mengine ya chama chake kuwa ni kuwapo mfumo wa uwakilishi wa uwiano bungeni na kwenye halmashauri za miji, hali itakayosaidia kuboresha demokrasia na kufikisha malengo ya uwakilishi wa asilimia 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume.

  Katiba hiyo mpya inatakiwa kuwa na kipengele cha kuruhusu mikataba mikubwa ithibitishwe na Bunge, ili kuepuka kashfa na ardhi isimilikiwe na Serikali Kuu, bali iwe mali ya wananchi wa eneo husika kupitia serikali zao za vijiji na vitongoji.

  Tao alifafanua “hii itaondoa uporwaji wa ardhi unaofanywa na wawekezaji na kuwafanya wananchi wakose ardhi kwa shughuli za kilimo na nyinginezo”.

  Katika kukosoa Katiba ya sasa iliyoundwa mwaka 1977, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema tangu kuingia mfumo wa vyama vingi, hakujafanyika mkutano wa Katiba kama ilivyo katika nchi nyingi ambao hushirikisha wadau wote na kuandaa Katiba mpya.

  Baadaye mkutano huo wa Katiba huunda Bunge la Katiba linalokuwa na wawakilishi kutoka kwa wadau wote na Bunge hilo ndilo hupitisha Katiba mpya.

  Vuguvugu la kutaka Katiba mpya lilianza mwaka 2000 baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kutaka Katiba iliyopo sasa ibadilishwe, lakini matakwa hayo yameshika kasi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hasa baada ya Chadema na viongozi wa dini ‘kushika bango’ huku wakiungwa mkono na wanaharakati mbalimbali.

  Vuguvugu hilo lilikwenda mbali zaidi baada ya juzi, CUF kuwasilishwa rasimu ya Katiba mpya kwa Wizara ya Katiba na Sheria iliyodai iliwachukua miaka minne kuikamilisha kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 130. Katika rasimu yao wamependekeza kuwapo serikali ya shirikisho ambayo itakuwa na rais mmoja.

  Tayari Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameshatoa tamko akisema atamshauri Rais Jakaya Kikwete juu ya kuundwa kwa Katiba mpya.

  Hata hivyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, alisema kwa maoni yake haoni sababu ya kuandikwa kwa Katiba mpya isipokuwa iliyopo sasa inaweza kufanyiwa marekebisho.

  Naye John Mhala anaripoti kutoka Arusha, kuwa Mbunge wa Kahama mkoani Shinyanga, James Lembeli, amesema anaunga mkono kuundwa kwa Katiba mpya yenye kukidhi matakwa ya wananchi wa matabaka yote, lakini nguvu ielekezwe kupambana na watuhumiwa wa ufisadi
  ikiwezekana wafungwe.

  Lembeli alisema hayo jana katika kikao na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa iwapo watuhumiwa hao hawatafikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua, suala la Katiba mpya linaweza “kuchakachuliwa’’ kwani watu hao wana nguvu sana ndani ya chama na serikali.

  Alisema Katiba ya sasa iliandikwa enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati huo viongozi wa chama na serikali wakiwa waaminifu na waadilifu kupita kiasi tofauti na hali ilivyo sasa.

  Lembeli alifafanua kuwa tofauti ya viongozi wa sasa na wa zamani katika uaminifu, ndiyo inayosababisha Katiba ionekane kuwa na upungufu mkubwa unaohitaji marekebisho ambayo kwa namna fulani inalinda watuhumiwa hao.

  Mbunge huyo aliendelea kuitaka serikali kusikiliza kilio alichokiita kuwa ni cha Watanzania wengi na kukifanyia kazi badala ya kuwabeza, kwa kuwa kwa madai ya mbunge huyo, kufanya hivyo ni kutaka kuleta vurugu zisizo na msingi.

  Lembeli alisema anasikitishwa na kauli za baadhi ya viongozi wa serikali kupingana wenyewe kuhusu hoja ya kuwa na Katiba mpya au kufanyiwa marekebisho Katiba ya sasa na kudai kuwa hali hiyo inaonesha jinsi wasivyojua mipaka na maadili ya uongozi.

  Alisema Waziri Mkuu alishatoa maoni yake kama kiongozi wa serikali, lakini akadai kuwa wengine wanakurupuka na kusema yao bila kujua mipaka jambo alilolieleza kuwa hatari kwa nchi ya demokrasia.

  “Jamani mimi nawajua mafisadi na dawa yao ni mahakamani na jela, vinginevyo hilo la Katiba mpya litakuwa ndoto,’’ alisema.

  Alipoulizwa mbona alikuwa kimya kwa muda mrefu, Mbunge huyo alisema alikuwa akitafakari mustakabali wa kura za maoni na uchaguzi mkuu na nini atawafanyia wananchi wa Kahama kwa kumkubali na kumrudisha bungeni kwa kishindo pamoja na alichokiita mafisadi kupiga kambi jimboni humo.

  Lembeli alisema pamoja na kukaa kimya, kaulimbiu yake ni ileile ya kupiga vita ufisadi na hataiacha mpaka dakika ya mwisho, kwani huo ndio msimamo wake kabla ya kuwa mbunge na baada ya kuwa mbunge.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Vuguvugu la kudai Katiba Mpya ndani ya CCM linazidi kupamba moto.....na itakuwa vigumu sana kwa vibaraka wa mafisadi ndani ya chama hicho kuendelea kutetea hoja ya viraka kwenye katiba iliyopo...................
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sirikali moja tosha na kutuimarisha zaidi umoja wetu wa kitaifa.

  Tufuate federal system ambapo visiwani tutakua na state of pemba na gavana wake na counties zake, unguja state hivo hivo na bara nako tukaunde states mbalimbali lakini chini ya rais mmoja kama ambavyo mfumo wa marekani ulivyo.

  Huu mfumo utaimarisha zaidi umoja wa kitaifa, gharama nafuu, kuharakisha maendeleo kwa wananchi na wapemba na wa-unguja kutokumezwa.
   
Loading...