Tishio la bomu Old Trafford

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Mechi ya mwisho katika ligi ya soka ya uingereza, EPL, kati ya Manchester united na Bournemouth imeahairishwa kufuatia wasiwasi wa bomu, uwanjani Old Trafford.

Kifurushi kinachoshukiwa kuwa na vilipuzi kilipatikana kimetegwa katika sehemu ya North West Quadrant.

Wachezaji wakiongozwa na kocha Louis Van Gaal walirudi kwenye chumba cha mabadiliko.

Tayari kikosi cha timu hiyo kilikuwa kinajiandaa kuingia uwanjani baada ya kutajwa. Maelfu ya mashabiki waliokuwa wanasubiri mchuano huo walilazimika kutoka nje.

Wataalam wa kutegua mabomu wameingia uwanjani kwa uchunguzi zaidi. Mchuano huo ulitarajiwa kuamua hatma ya Manchester United huku ikisaka nafasi ya kushiriki kwenye ligi ya vilabu bingwa barani ulaya.

Manchester United inashikilia nafasi ya saba ikiwa na alama 63 baada ya mechi 37. Awali Mashabiki wa klabu walionyesha kughadhabishwa na utendakazi wa kocha Van Gaal, wakitaka aachishwe kazi.

Hii ni baada ya Westham kuzamisha matumaini ya klabu hiyo kwa kuizaba 3-2 wiki iliyopita.
 
Habari zaidi zinasema Wanajeshi wa Uingereza watalaamu wa kulipua mabomu walifanikiwa kulilipua hilo bomu bila kuleta madhara.
Mechi hiyo itapangiwa siku nyingine ingawa hataitakuwa na faida yoyote kwa Man United kwani Man City baada ya kupata sare ya 1-1 ugenini kwa Swansea wamefikisha points 66 ambazo pia Man U itazifikia kama itashida mechi hiyo lakini Man City inayo uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa. Ili Man U iweze kuishisha Man City italazima kushinda zaidi ya magoli 10 , kitu ambacho hakiwezekani.
Jambo hilo linawezekana kwetu tu ambako Police Tabora na Geita United waliweza kufunga magoli 7 kila moja kwenye dakika 45 za kipindi cha pili cha mechi zao za mwisho ambazo zilikuwa zinaamua ni time ipi kati ya hizo mbili ingepanda daraja. K
Kwa Uingereza ni kama ndiyo basi. Masimamo top four utabakia kama ifuatavyo :Leister City, Arsenal, Tottenham Hotspur, Man City
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom