Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,319
- 72,747
Huyu mtoto ni shujaa, tena shujaa kuliko maelfu ya watu wazima waliopo humu JF na mamilioni ya Watanzania mitaani. Ni shujaa pengine kuliko hata watumishi wengi wa vyombo vya uokoaji ndani ya nchi yetu.
Kwa wasio mtambua, Huyu ndio yule mtoto huko visiwani Geita ambaye yeye na wenzie wakati wakienda shule asubuhi mtumbwi ulio wabeba ulipinduka na kuzama.
Pamoja na umri wake wa miaka 16, alijitahidi kuogelea na kuokoa mtoto mmoja mmoja hadi akafikisha wenzake 9 ila watatu wakawa wamechoka na kuzama na kufa Maji.
Huyu sio wa kawaida, nimemsikiliza Clouds 360 hakika nimejiuliza mengi. Jee mie rafiki zangu wangezama ningeweza kurudi mara tisa majini na kuwaokoa? Sijapata jibu nadhani kwa vile sina ushujaa wa mtoto huyu.
Naomba nasi JF tumtangaze kuwa ni shujaa wa 2017 na kuishinikiza serikali kijana huyu apewe ile nishani ya Rais ya ushujaa.