Tips kwa Mawaziri wa Tanzania

Tips kwa Mawaziri wa Tanzania

winnerian

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
407
Reaction score
638
1. Unda timu ya kijasusi kwa ajili ya ukusanyaji wa data, uchambuzi, na mapendekezo mbadala kwa maeneo yote yenye matatizo

2. Wawezeshe wakuu wote wa vitengo kuanzia Watendaji Wakuu hadi viongozi wa chini. Wape uhuru wa kutenda katika sehemu zao bila kuingiliwa ili kukupa matokeo.

3. Epuka kuwaunganisha Wakurugenzi wakuu na utaratibu wako wa kila siku wa siasa. Waache kwenye ofisi zao ili waweze kutoa matokeo unayohitaji. Kuwa na Wakurugenzi Wakuu karibu nawe kila siku, siku baada ya siku, hatimaye kutadhoofisha uwezo wao wa kukupa matokeo unayotaka

4. Mwisho kabisa, tembelea miradi yako kwa lengo la kutatua changamoto na sio kujipromote kisiasa wala kutafuta umaarufu haitakusaidia na pia haitakufanya uendelee kubaki kwenye nafasi yako milele kwani ufanye vibaya au vizuri ipo siku utaachia ngazi.
 
Back
Top Bottom