Timu yako EPL haichezi, unajua kwanini?

poppah

JF-Expert Member
Dec 19, 2014
630
547
Wikendi hii ya Februari 8 (jana) na 9 (leo) ambayo Ligi Kuu ya England, EPL, inaingia raundi ya 26, kutakuwa na mechi 4 tu huku mechi zingine 6 zikichezwa wikendi ijayo, kati ya Februari 14 hadi 17.

Hii inatokana na makubaliano yaliyofikiwa Juni 2018 kati ya Bodi ya Ligi Kuu (EPL), chama cha soka (FA) na na Bodi ya Ligi za chini (EFL) kwamba Februari ya kila mwaka, ni lazima timu zote zipate wikendi moja ya mapumziko.

Mapumziko haya ambayo yanaitwa Winter Break au Mid-season Player Break, yamekuja ili kupumzisha miili ya wachezaji hasa baada ya ratiba ngumu ya Disemba na Januari.

Ujio wake kwa kiasi kikubwa umechagizwa na kelele za makocha wageni ambao katika nchi zao mapumziko haya yapo na huwa hakuna ratiba ngumu ya Disemba - Januari.

Hoja yao ilikuwa mapumziko haya huwafaidisha wachezaji kwa kukabiliana na pilika pilika za nusu ya pili ya msimu, hasa timu zinazosonga mbele kwenye mashindano ya Ulaya.

Pia iliaminika kwamba itawasaidia wachezaji wa England kuelekea msimu wa mashindano ya kimataifa, kama Euro 2020.

Mapumziko haya yameanza rasmi Februari hii ambapo mechi 4 za wikendi hii ni

Feb. 8
Everton v Crystal Palace na Brighton v Watford.

Feb. 9:
Sheffield United v Bournemouth na Manchester City v West Ham.

Hata hivyo, mechi ya Manchester City na West Ham imeahirishwa kutokana na kimbunga Ciara kilichoikumba Uingerera.

Mechi 6 za wikendi ijayo ni

Feb. 14:
Wolves v Leicester

Feb. 15:
Southampton v Burnley na Norwich v Liverpool.

Feb. 16:
Aston Villa v Tottenham na Newcastle v Arsenal.

Feb. 17:
Chelsea v Manchester United.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom