Timu ya kampeni ya Mizengo Pinda hii hapa

Timu ya kampeni ya Mizengo Pinda hii hapa

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
Nadharia ya kambi au ufuasi ni jambo linalojotokeza pale mtu au kundi la watu wanapotofautiana falsafa, mawazo na hata matendo…. kwa mfano ukiwa unaamini katika utendaji bora na maamuzi magumu lazima utakuwa kambi ya Nyerere, Sokoine, Kawawa na Lowassa. Hiyo ndio nadharia nzima ya ufuasi au ukambi; kwaiyo kundi la Membe lazima litambua kuwa hata Lowassa kuwa na kambi sio haramu na dhambi na kama yeye alivyo pia na kambi, kama wassira alivyo na kambi, Pinda alivyo na kambi, Ngeleja, Magufuli hata na January pia. (Baada ya kumuelimisha chabruma na WAMA et al sasa naomba nije katika issues ya leo ambayo ni kambi ya Mheshimiwa Pinda).

1. Mheshimiwa Pinda
Huyu ndiye waziri mkuu wa sasa wa JMT. Hapa karibuni kajitokeza wazi wazi na kuonyesha nia ya kugombea urais wa 2015. Huyu mheshimiwa amekuwa akiratibu timu yake kwa usiri mkubwa sana ni miongoni mwa viongozi wachache ndani ya CCM walio na ushawishi hasa wa kuongea (one of the good orator). Mheshimiwa Pinda amekuwa akichukuliwa na jamii kama mtoto wa mkulima Pamoja na hizo sifa zote hapo juu, Mheshimiwa Pinda wachambuzi wamekuwa wakimchukua kama mtu dhaifu sana hasa katika kutoa maamuzi hata pale mamlaka yakiwa chini yake, hii ni tofauti na mtangulizi wake Lowassa ambaye watu uamini kuwa lowassa alikuwa mtu wa maamuzi magumu sana "kwa kweli hali ilivyo sasa Tanzania tunamtaka mtu kama Lowassa ambaye sio tu atatoa maamuzi bali pia usimamia maamuzi yake mpaka tone la mwisho ya damu yake"…….. Pinda amekuwa mtu wakulalamika na mbaya zaidi kupenda kulia, wachambuzi wanasema huyu mtu amekuwa wakupenda kulia lia, kwa mfano albino alipoouwawa jamaa alilia, Chadema walivyoo anzisha operation sangara jamaa alilia, na hata juzi alipoona waraka wa Lema hakujizuia kulia tena na wengine waliienda mbali sana na kusema "ili Pinda awe rais lazima kura ya maoni iitishwe kwanza (Referendum) ili kuwauliza watanzania kama kweli wanaitaji kiongozi anaependa kulia lia au hapana?"……. However jamaa amekuja kwenye gemu akiwa amejipanga san sana na hata kwa hali ilivyokuwa sasa hivi amepiku nafasi ya joka la mdimu na joka la mdimu ameanza kufikiria kumsapoti ili at the end awe PM.


2. Abdalla Bulembo
Huyu ni mwenyekiti wa wazazi wa CCM. Bwana Bulembo alikuwa kambi ya Lowassa kabla ya kuhamia katika hii kambi kwa sababu kuu tatu, mosi kutokana na elimu yake kuwa ndogo (darasa la saba) kila wazo alilikuwa anatoa katika hiyo kambi lilionekana kama pointless na kweli yalikuwa pointless ile mbaya, kwa hili hakuna ubishi nyie wenyewe mumeshuhudia hata katika uchangiaji wake katika bunge la katiba jamaa amekuwa akimwaga pumba ile mbaya…. Sababu ya pili kama tunavyokumbuka uchaguzi wake ulikuwa na doa la kutumia rushwa hivyo Mongula akamtisha kuwa matokeo yake yatafutwa kama asipomsapoti mheshimiwa PM., tatu kwa tamaa zake za kutafuta ela kwa ukwasi ilifikia kipindi akapeleka proposal kwa Lowassa bajeti ya million 300 ili kuanza kuzunguka kwa wajumbe ila Lowassa alimkatalia akasema kwa sasa kampeni hazijaanza na hata hivyo hana hiyo ela "kwa sasa sina kabisa hiyo ela mzee", Bulembo alitoka katika kikao hicho kwa hasira ya hali ya juu na ndio kisa cha yeye kuhama kambi….. Umuhimu wake ni kuwa cheo alichonacho ni dhahiri atakuwa na wafuasi wachache ndani ya jumuiya hiyo. Bulembo kwa sasa anatuhumiwa kuuza shule ya jumuiya ya wazazi ya CCM, shule ya ISANGO iliyopo Kinesi mkoa wa Mara (tena mbaya zaidi sehemu alikotoka baba wa Taifa ndiyo jamaa anauza shule wala haogopi laana ya baba wa Taifa). Shule hiyo ndiyo alisoma Mama Nyerere, Mama Sita na hata Mama Kabara(Waziri).


3. Didas Masaburi
Huyu ni meya wa jiji la Dar es Salaam. Huyu mtu sio mgeni katika masikio yenu hasa alipotoa ile kauli kali kuwa wabunge wanafikiria kwa kutumia makalio, ni mtu jasiri kutoka mkoa wa mara ila wachambuzi wanasema ujasiri wake anaupeleka mpaka kwenye kutafuta fedha kwa njia yoyote ile iwe mbaya au safi….. Ni huyu Masaburi aliyeshutumiwa sana sana katika uuzaji wa mradi wa mabasi ya UDA kwa bei cheeeeeeeee; bei ambayo hata Augustino Lyatonga Mrema kwa ile million 37 yake aliyonayo benki angeweza kuongeza kidogo na kununua UDA…… katika unununuzi huo hakuna shaka alilamba kitu kidogo (Rejea Hansad, kauli ya Mnyika na Mtemvu december 2013)… Awali alikuwa team Lowassa ila akahama kwa sababu kwamba Lowassa ana watu wengi sana sana sanaaaaaa hivyo awezi kupata cheo chochote… Amekuwa na tabia mbaya hata ya kumdanganya mkuu wa kaya kama mnakumbuka alifanya mpango then Jakaya akawa mgeni rasmi katika ufunguzi wa chuo chake cha ugavi kilichopo chanika, kumbe baadaye mheshiimiwa Mama Sita wakati huo ni waziri wa elimu akagudua kuwa chuo hicho hakijasajiliwa skendo iliyoingiza serikali katika matatizo makubwa sana, ndugu zangu always remember hakuna kitu kibaya kama short cut katika mambo ya msingi hasa elimu. Huyu ndiye Masaburi ambaye kapangiwa kuwa waziri wa elimu hiyo hiyo jamaa akishinda 2015. Natabiri elimu kufa kabisa katika nchi hii jamaa akipewa hiyo nafasi.



4. Janet Masaburi
Huyu ni moja wa wake wa mheshimiwa meya wa jiji wa Dar es Salaam. Ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM, kushinda kwake kulifanikishwa sana sana na Sophia Simba. Vikao vya Pinda vyote ufanyika nyumbani kwa mama Janet na ni shost mkubwa wa mama Tunu Pinda. Ukaribu wao umeongezeka hapa karibuni baada ya mama Tunu kufanikisha kumpa Janet tender ya kuingiza sukari nchini. Kama mnavyokumbuka hapa karibuni serikali iliisi kutokea upungufu wa sukari (Citizen, 22/3/2014) ndipo serikali iliamua kutoa vibali kwa watu wachache ili waruhusiwe kuingiza sukari kutokana na umuhimu wa jambo lenyewe likapelekwa chini ya ofisi ya waziri mkuu moja kwa moja na sio viwanda na biashara ndipo mama Janet akatumia hiyo fursa naomba nieleweke sio vibaya kutumia fursa ingawa kubebwa katika harakati hizo za kutafuta tender ndiyo sio halali na daima sio fair katika hali ya kawaida.


5. Sara Msafiri
Huyu ni mbunge wa viti maalumu kupitia kundi la vijana CCM. Ni binti ,ambaye yuko tayari kufanya lolote ilimradi afanikishe nia yake; aliwahi kunukuliwa akisema "yeye ni Machiavelli kwa maana yuko tayari kufanya na kutoa chochote kile ilimradi apate anachotaka na kutimiza nia yake". Kwake yeye the end justifies the means….. Katika hii kambi huyu ndiyo roho ya Pinda akiaminiwa kuwa anaushawishi miongoni mwa vijana kumbe hakuna kitu.. ukaribu wake huo umezua gumzo mpaka watu wengine wakaanza kufikiria vingenevyo. Ni sara na Masaburi walioyompa Pinda ushauri mbovu wa kuita wajumbe nusu kutoka kanda ya ziwa na kupelekea wengine kukasirika sana na kutoa siri za vikao hivi karibuni huko mwanza. Kumbuka mkutano ulifanyika kwa awamu awamu katika state lodge Mwanza. Ni sara akiwa na Munde majina yao yalisikika kwa mbali katika ile kesi ya ubadhirifu inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa Tanesco Ndugu Mhando (rejea kesi ya TAKUKURU chini ya vifungu namba 22, 28 na 31 PCCA). Umuhimu wake katika hili kambi ni kuwa mhimili mkuu (think tank) kwa kuwa dada kaenda shule, elimu yake ni ya Masters Degree ingawa dissertation aliandikiwa katika garden ya TAMAL mwenge, kuwa na hiyo elimu katika mambo ya jamii kinachomfanya kuwa msomi katika kundi hilo la Pinda, hivyo anachokisema ndicho kinachotendeka katika hiyo kambi.


6. Antony Dialo
Huyu ni darasa la saba ambaye mpaka sasa haijulikani ni jinsi gani aitwe Dr. Awali alikuwa katika kambi ya Membe ila alipoona Membe hauziki kabisa, hana mvuto wa kisiasa, Not Charismatic hata kidogo, hana ushawishi mzee Dialo akaona hakuna sehemu pa kwenda zaidi ya kwa Pinda, kumbuka kuwa halikuwa hawezi kwenda kwa Lowassa kwa sababu enzi za mkapa, Lowassa akiwa waziri wa mifugo na dialo akiwa naibu wake hawakuweza kuiva katika chungu kimoja na Lowassa kama kawaida yake hakumchelewesha bali alimlima barua kama tatu vile (Kesho nitaziweka humu ndani). Hili lilisababisha bifu kubwa sana ila lowassa hakumchelewesha tena akaenda kwa Mkapa na kumwambia chagua moja (kusuka au kunyoa) kuniacha mimi au kumuondoa Dialo kuwa naibu wangu kwa sababu uwezo wake ni mdogo sana na hana viwango kabisa. Dialo hana ushawishi kabisa wa kisiasa sema tu anapewa cheo kutokana na umiliki wake wa vyombo vya habari. Amekuwa akihusishwa na mambo mabaya kama yaliyomtokea Steven Kazi mbunge wa zamani wa Mwanza, amekuwa akihusishwa na kupotea kwa kijana moja katika uchaguzi wa 2005, na vile vile amekuwa akihusishwa na kilichomtokea mwenyekiti wa zamani wa mwanza kwa sasa ni marehemu. Ingawa kama ninavyopenda kusema zingine zaweza kuwa kama shutuma ila swali linakuja kwa nini ushutumiwe wewe tu na sii wengine? Hili ni swali ambalo mimi wala wewe hatuwezi kulijibu kwa haraka haraka. Huyu bwana nguvu yake katika hii kambi ni fedha kwa amejaliwa kuwa na fedha kwa kiasi fulani, hivyo maswala yote ya fedha katika hii kambi yeye uratibu.


7. Munde Tambwe
Huyu ni mbunge wa viti maalumu kupitia CCM. Katika kipindi kifupi huyu dada amekuwa haeleweki yuko kambi gani, amekuwa mtu wa kuhama hama kila kukicha na hii tabia yake utawaliwa na ukwasi wa kupata ela haraka haraka. Kwanza kabisa alikuwa kambi ya Lowassa hasa katika kipindi cha uchaguzi wa 2010 na 2012 uchaguzi wa chama, alipoona kwa lowassa hakuna mrija wa ela kwani ela zinapelekwa kwa (wajane, kusaidia yatima, kuboresha elimu, kusaidia wahitaji, masikini makanisani na misikitini) akaamua kukimbia kambi na kwenda penye fedha. Aliweza kukimbilia katika kambi ya Ngeleja na ndipo Ngeleja pasipokujua nia ya huyu dada alimpa takriban million 10 (Peackcook hotel, 14/2/2014) ili aanze kuorganize wanawake wa UWT mikoa yote kwa ajili ya kumsapoti Ngeleja. Munde kama Bulembo na Masaburi ni matapeli wakubwa na hata huyu Munde kama mnakumbuka yeye na dada yake wameweza kuhusishwa katika uuzaji wa unga. Mpaka naandika uzi huu dada yake yuko ndani kwani alikamatwa na unga katika uwanja wa JK nyerere tayari kwa kuipeleka Italy. Munde akuanza haya mamba leo kama mtakumbuka mnamo mwaka 2004 alikuwa moja wa washitakiwa wakubwa (Prime Suspects) katika halmashauri ya Tabora alipokuwa kama mhasibu msaidizi katika halmashauri hiyo (Rejea kesi maarufu kama Mama Khalfan). Kitu kilichopelekea kufukuzwa kazi katika halmashauri hiyo, vile vile watu walishangaa ni jinsi gani aliweza kuwa msaidizi uhasibu wakati elimu yake ni darasa la saba, ingawa kwa wakati ule labda tunaweza kusema wasomi walikuwa wachache.

8. Akaunti ya NYAU
Hili jina la akaunti ya Nyau, ni jina geni miongoni mwenu, ila ni akaunti mahususu kwa ajili ya wakurugenzi wa halmashauri kumchangia mzee tajwa hapo juu.. hii akaunti imeanza kazi rasmi mwezi huu wa nane unaweza kujenga picha mpaka mwakani mwezi wa tano hii akaunti itakuwa na kiasi ngapi… Wadau wakubwa katika akaunti hii ni wakurugenzi wa halmashauri na majiji ili kuweza kufanikisha jambo la mkubwa.. kiasi hakijawekwa wazi ila wanaweza kuchangia kuanzia 10ml and above kwa mwezi kwa kila mkurugenzi. So kama wakichangia wakurugenzi 80 tu (80X10 mln =80 million per month), unaleta mchezo wewe watu wanajipanga sio January Makamba kelele kelele tu kwenye facebook na tweeter wakati mkakati sifuri.

Mwisho:
Hili ndilo kambi lililochukua nafasi ya Membe baada ya kuona Membe hauziki, hana mvuto hata kidogo, uwezo wake ni mdogo sana pamoja na kupewa wizara nyepesi isiyokuwa na direct contact na mwananchi (pata picha Membe angepewa wizara ya Ardhi, maji, au Nishati hahahahahahaha sitaki kuimagine something like that).

Alhamisi nakuja na Wassira.

Asante
 

Umbea ni fani kama Art ya muziki vile, inabidi u practice kila mara iliufundi wako uwe endelevu

Tunasubiri Alhamisi ya Mzee wa Gombe
 
umbea mwingine ni hasara sana pole kwa umbea ambao hauna msaada kwa jamii.
 
pinda ni janga la taifa kundi limejaa matepeli Masaburi tapeli Bulembo tapeli Munde tapeli hahahaha
 
minding your own business is a full time employment!stay employed.
 
Hii kambi mbona haina uzito hata ukigombea Ubunge utashindwa haiba washawishi kabisa.
 
Haiitaji kuwa na elimu kama ya Bulembo ili kuweza kung'amua upo timu gani.
 
Unajua mimi nnapenda sana mki mjadili pinda kwasababu kukua kwa pinda ndio kifo cha membe,

membe anategemea viongozi serekalini na pinda naye anategemea serekaliini maana watu wana

taka fea na misaada ya kazi, kwahiyo wana pakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kwamba wanakubalika

ikifika mwenzi wa tano watajua papa lawasa ni nani.
 
Unajua mimi nnapenda sana mki mjadili pinda kwasababu kukua kwa pinda ndio kifo cha membe,

membe anategemea viongozi serekalini na pinda naye anategemea serekaliini maana watu wana

taka fea na misaada ya kazi, kwahiyo wana pakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kwamba wanakubalika




ikifika mwenzi wa tano watajua papa lawasa ni nani.

kaka we ni bonge la great thinker............kula like kubwa sana sana. Na ni jambo lililowazi kabisa kwamba Membe saizi hawezi gemu hata kidogo hata mkulu ameona wazi kuwa Membe hauziki hata umbebe vipi... hana mvuto wa kisiasa kabisa. ndio mana jk saizi kakaa pembeni amewachia mama salma na riz ndio wafe na membe.
 
Ya EL ni kambi nzuri lakini wasimu wa watu wake ni wapenda pesa na machoni mwa Watanzania hawaaminiki

sio kweli kaka, kupenda pesa ni hulka ya mtu binafsi na sio falsafa ya kambi....... kwa mfano hata humu kwa Pinda mtu kama Bulembo au Masaburi au sara msafiri utasemaje........
 
Back
Top Bottom