Timu ya FC Bayern München ya Ujerumani yatoa shukrani kwa mashabiki wake wa Tanzania

Mtamba wa Panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2017
695
1,712
Klabu maarufu ya soka duniani yenye maskani yake katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani, FC Bayern München E.V, Leo tarehe 31/12/2017 mnamo mida ya SAA Nane mchana ( kama masaa mawili yaliyopita Wakati naanza kuandika Uzi huu ) , kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Facebook, wamewashukuru mashabiki wao kutoka Tanzania kwa support yao kwa mwaka huu wa 2017, unaotarajiwa kuisha Masaa machache yajayo.

Ujumbe huo wa shukurani ulisema "Dear FC Bayern fans in Tanzania, thank you very much for your great support in 2017!
1f64f.png
[HASHTAG]#MiaSanMia[/HASHTAG]
1f1f9_1f1ff.png
"
huku wakiambatanisha picha yenye backgroud ya Wachezaji wa bayern wakishukuru mashabiki ambayo walizidi "kunogesha pilau" kwa kuandika "Asante" iliyoambatanishwa na Bendera ya Tanzania na logo ya "manunda" hao.

26230478_1802679443136455_8359444851262262160_n.jpg


Watanzania wapokea kwa furaha shukrani hizo
1802679443136455


Watanzania wengi walipokea kwa mshangao na furaha pia shukurani hizo, ambapo baadhi waliambatanisha hashtah ya [HASHTAG]#MiaSanMia[/HASHTAG] ambayo ni club motto ya
klabu hiyo ambayo ni kama vile "Daima Mbele, Nyuma Mwiko" kwa timu ya Yanga, ama "Nguvu Moja" kwa Simba SC, wazee wa Msimbazi.

Kama kawaida ya "Wabongo" hawakuacha kuonyesha vituko vyao kwenye ukurasa wa "vigogo" hao wa Ulaya. Maneno maarufu kama "Vyuma vimekaza" pia
hayakukosekana kwenye "Comments" za wachangiaji wa "Post" hiyo ya ukurasa wa "wazee" hao wa Bavaria.

Kama haitoshi, Shabiki mmoja wa klabu ya Arsenal ya Uingereza "aliniacha hoi" mimi mwandishi wa uzi huu pale alipoonyesha kukerwa kwake na "vipigo"
vya mara kwa mara kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE akionesha kukerwa zaidi na "dhahama" a.k.a "Kuchenjuliwa Makinikia" jumla ya magoli 10-2 pale timu hizo zilipokutana mara ya mwisho kwenye UCL.

Utani uliendelea kwenye eneo la maoni, ambapo baadhi ya mashabiki wa wapinzani wa klabu ya Arsenal ya Uingereza walipowashukuru "wababe" hao kutoka
jiji la Munich, Ujerumani juu ya "Kuwatembezewa vitasa" mara kwa mara "washika bunduki" hao kutoka jiji la London.

Katika hali ya kushangaza, shabiki mmoja aliandika ujumbe ambao uliwakera wachangiaji wengine pia, pale alipoandika kuwaonya bayern kuhusu "kutia
maguu" hapa "bongo" akidai kwamba hapafai na Bayern wajiepushe na hilo. Baadhi ya "Wabongo" walimjibu vibaya na wengine kuhoji uraia wake.

Raia mmoja wa Rwanda pia aliwashukuru Bayern kwa shukrani hizo, lakini katika hali isiyokuwa ya kistaarabu ambayo mwandishi wa uzi anaikemea, baadhi ya wachangiaji wakitumia lugha ya Kiswahili, "walimshukia" na "Kumsemea sivyo" jamaa huyo kutoka "Ardhi ya Kagame" huku wakimwambia "asiishobokee" nchi yao.

Pamoja na yote, baadhi ya "Wabongo" walionesha kutoamini kwao kuhusu hilo huku baadhi wakidhani ni Uongo a.k.a "Utapeli". Mimi mwandishi wa uzi huu nimejiridhisha vya kutosha kwamba si "Utapeli" bali ni kweli Bayern wametuma salamu hizo kwetu sisi "Wabongo" kupitia ukurasa wao rasmi wa klabu ambao ni huu hapa. Wewe mwanaJf waweza pia kuingia sasa hivi kwenye ukurasa wa "mabingwa hao mara 5 wa Ulaya" na kujiridhisha.



Niite Mtamba wa Panya a.k.a Mzee wa Tuna
 
Back
Top Bottom