Timu Maalim’ wasusa mjengo wa ‘Timu Lipumba’

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
SIKU, saa na dakika zinahesabika kwa Timu Maalim Seif Sharif Hamad kufungua ofisi mpya nje ya ile ya Buguruni jijini Dar es Salaam.

Wameamua kuachana na Ofisi Kuu ya chama hicho ambayo kwa sasa inatumiwa na Timu ya Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, Timu Maalim wamefikia uamuzi huo baada ya Timu Lipumba kung’ang’ania kutumia ofisi ya Buguruni huku mgogoro uliopo ukiwa haujapatiwa ufumbuzi.

Ofisi mpya za CUF Timu Maalim zinatarajiwa kuzinduliwa muda wowote kuanzia sasa katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma amethibitisha kuwa, Timu Maalim inatarajia kuzindua ofisi hiyo muda wowote kuanzia sasa ili chama hicho kiendelee na operesheni zake kama kawaida.
 
Namkubali sana Maalim Seif kwa Mikakati yake.Nadhani CUF inafaidika sana na Busara zake.
 
Prof Lipumba wewe ni mmoja wapo wa wasaliti wa mageuzi ya kisiasa kwenye Nchi hii.

Ukaribu wako na watawala na uharibifu wako katika kuvuruga CUF hausameheki asilani..!
 
Hapo hakuna cha pongezi, literally anakimbia chama. Anatambua ameshindwa na huenda chama kingine kitaibuka.
 
cha msing timu seif waimalisha 2 ushirikiano wao wa UKAWA il kuivunja timu liporopesa,na wabunge ambao walishnda kuptia UKAWA wasitegemee kurud tena mjengoni.hawajaona kabisa faida ya ukawa hasa dadangu Sakaya?
 
Yan Lipumba anazogoa sana asee kasahau kuna waarabu na wapemba wana hela hazinaga kazi kumpa Maalim mpunga akapange sio kesi kwao
 
SIKU, saa na dakika zinahesabika kwa Timu Maalim Seif Sharif Hamad kufungua ofisi mpya nje ya ile ya Buguruni jijini Dar es Salaam.

Wameamua kuachana na Ofisi Kuu ya chama hicho ambayo kwa sasa inatumiwa na Timu ya Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, Timu Maalim wamefikia uamuzi huo baada ya Timu Lipumba kung’ang’ania kutumia ofisi ya Buguruni huku mgogoro uliopo ukiwa haujapatiwa ufumbuzi.

Ofisi mpya za CUF Timu Maalim zinatarajiwa kuzinduliwa muda wowote kuanzia sasa katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma amethibitisha kuwa, Timu Maalim inatarajia kuzindua ofisi hiyo muda wowote kuanzia sasa ili chama hicho kiendelee na operesheni zake kama kawaida.
Ukawa ndo kwishilia mbali, ikiwa CUF vipande vipande,NLD Kama kimekufa Tu, NCCR imezimia. Imebaki CDM Tu nayo ipo ICU.
 
SIKU, saa na dakika zinahesabika kwa Timu Maalim Seif Sharif Hamad kufungua ofisi mpya nje ya ile ya Buguruni jijini Dar es Salaam.

Wameamua kuachana na Ofisi Kuu ya chama hicho ambayo kwa sasa inatumiwa na Timu ya Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa, Timu Maalim wamefikia uamuzi huo baada ya Timu Lipumba kung’ang’ania kutumia ofisi ya Buguruni huku mgogoro uliopo ukiwa haujapatiwa ufumbuzi.

Ofisi mpya za CUF Timu Maalim zinatarajiwa kuzinduliwa muda wowote kuanzia sasa katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma amethibitisha kuwa, Timu Maalim inatarajia kuzindua ofisi hiyo muda wowote kuanzia sasa ili chama hicho kiendelee na operesheni zake kama kawaida.
Hakuna tena chama hapo
 
Back
Top Bottom