Timu inamsubiri nahodha tu

Timu inamsubiri nahodha tu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Alianza kuchaguliwa Hashim Juma Issa kutoka Zanzibar kama Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA. Akafuata Paschal Patrobas kama Mwenyekiti wa BAVICHA. Jana, Halima Mdee amekabidhiwa BAWACHA kama Mwenyekiti wao. Hawa wote wana viongozi wenzao katika mabaraza yao. Kiujumla ,wanatengeneza timu. Kukamlika kwatimu hii,lazima nahodha achaguliwe.Ni tarehe 14/9/2014.

Mwenyekiti wa chama atakayechaguliwa ataitumia timu hii mpya ya uongozi ya CHADEMA kusonga mbele. Kwa mastaa waliopo katika timu hii, ni lazima kuchaguliwe nahodha imara. Anayeheshimika na kusikilizwa. Anayewea kusemea na kukemea.

Safu safi imeshapatikana. Bado nahodha tu.Wajumbe husika kazi kwenu...
 
Last edited by a moderator:
Magamba hawana hamu kabisa na huu uchaguzi.
Kuanzia mwenyekiti wa taifa wa CCM mpaka balozi wa nyumba kumi wanafuatilia uchaguzi huu hatua kwa hatua.
Hawataki kabisa hata kujua wapuuzi wenzao kule Dodoma wanaendeleaje;wote wapo bize na uchaguzi wa CHADEMA.
pipoooooooooooooooooooooooooooooooz.
 
Magamba hawana hamu kabisa na huu uchaguzi.
Kuanzia mwenyekiti wa taifa wa CCM mpaka balozi wa nyumba kumi wanafuatilia uchaguzi huu hatua kwa hatua.
Hawataki kabisa hata kujua wapuuzi wenzao kule Dodoma wanaendeleaje;wote wapo bize na uchaguzi wa CHADEMA.
pipoooooooooooooooooooooooooooooooz.

Wanaofuatilia kama vile wa kwao teh teh
 
mdee ni jembe la ukweli unakumbuka alivyompelekesha prof Tibaijuka kuhusu ufisadi wa ardhi cha simba
 
Na team captain ni Freeman Aikael Mbowe.
CCM wanatamani kumkodi mh. Mbowe akawarekebishie na kuokoa chama chao!
 
Kwa kikosi hicho, kocha aliyestahili ni Zitto Kabwe
 
Wakuu,
Kansa Mbarouk akipata hata kura yake Mwenyewe nahamia MAGAMABA
 
Back
Top Bottom