Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,148
- 10,571
Hivi karibu katika ulimwengu wa kidijitali, imekuwa ni kawaida watu kuzungumza kama bile wamekatwa vichwa. Mitandao imekuwa ji mahali ambapo ukweli unapigwa kwa sababu ya kulinda hisia za mtu na ambapo mantiki inaonekana kama ni adui.
Hivi sasa, ukiingia TikTok au Instagram, hutakutana tu na picha za chakula na densi; utakutana na mijadala ambayo inakufanya ujiulize je kwanini shule hazikujengwa kwa ajili ya kufugia kuku na sio tena kuelimisha watu.
Mwaka jana mjadala mmoja uliopamba moto ni ule wa "Gorilla mmoja dhidi ya wanaume 100." Kuna watu, wakiwa wamejinyoosha kwenye makochi yao huku wakila kachori na Pepsi ya baridi, wanadai kwa dhati kabisa kuwa binadamu wanaweza kumpa kichapo Silverback Gorilla.
Hebu tuchambue ukweli kidogo: Gorilla mmoja ana nguvu mara tisa kuliko mwanadamu mwenye nguvu zaidi. Ana uwezo wa kunyanyua uzito wa kilo 800! Hawa wanaume 100 wa dar?, ambao wengi wao hupata "stress" wakikosa chaji ya simu au mpaka alikasusu?!, watafanya nini mbele ya mnyama anayeweza kupasua tairi la gari kwa meno yake pekee?
Hapa ndipo maoni yanapojaribu kupigana mwereka na uhalisia ambao upo wazi. Watu 100 dhidi ya Silver back gorilla mmoja inaonekana kama idadi kubwa, lakini kwenye msitu, hiyo ni sawa na kumpa Gorilla karanga 100 za vitafunio. Watu 30 wa kwanza watafanyiwa jambo ambalo Guinness World Records watachapisha rekodi zenu.
Kisha mwaka jana huo huo kukaja mjadala mwingine wa ajabu: "Dubu au Mwanaume msituni?" Wanawake wengi walichagua kukutana na dubu (Bear) porini badala ya mtu mwenye jinsia ya kiume wakidai dubu anaeleweka kihisia kuliko binadamu, SERIOUSLY?
Hapa, hisia za kijamii zimefunika kabisa, huku wale watetezi wa haki za wanawake wakiropoka kama walevi, kuwa ni salama kuwa karibu na Dubu. Yaani ni heri mtoto wako wa kike akutane na Dubu porini kuliko mwamba, kwa sababu dubu yeye ataishia kukutafuna pekee ila mwanaume atafanya vitu vibaya zaidi.
Ukweli wa kisayansi ni kwamba Dubu (hasa Grizzly au Poral Bear) hakuangalii kama kiumbe mwenye matatizo ya kisaikolojia; anakuangalia kama "msosi.", Ingawa tunaelewa hofu za kijamii, kutaka kupiga picha na dubu msituni kwa sababu "wanaume ni watu wabaya".
Tatizo la mijadala hii ni nini? Ni kile tunachokiita "Online Echo Chambers"—mahali ambapo watu wanatafuta kutetea mihemko na hisia zao badala ya kutamani kufahamu na kukubali ukweli. Tunapuuza kanuni na uhalisia wa maisha ili tuonekane "tuna hoja" mtandaoni.
Tunahitaji kurudi kwenye misingi. Ukweli haubadiliki kwa sababu umepata likes elfu kumi. Gorilla atabaki kuwa jitu lenye maguvu, na dubu hatakuuliza mdada kama una msongo wa mawazo ama umeachwa na boyfriend.
Tuache kutumia maoni yetu kupinga uhalisia; vinginevyo, tutaishia kuwa kizazi kinachojua kutumia sana filter za picha lakini hakijui tofauti kati ya kufa kishujaa na kifo cha mende.