Tiketi za mechi ya 'mtani jembe' zachakachuliwa!

Tiketi za mechi ya 'mtani jembe' zachakachuliwa!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,900
Reaction score
29,433
Mimi sio mshabiki wa mpira wa mchangani lakini nimehudhunishwa mno na mafisadi wachache walioamua kununua tiketi zote za Tsh 5000, zinazotegemewa na makabwela, na kisha kuziuza mtaani katika soko jeusi (black market) kwa bei ya kuruka kuanzia Tsh 7000 mpaka 10000!

Leo nimeshuhudia vijana wakihaha huku na kule kusaka tiketi hizo bila mafanikio. Kuna mshabiki mmoja alienda hadi tff kufuatilia hizo tiketi za makabwela lakini alikuta zimeishaingia kwenye mikono ya mabwanyenye ambao walikuwa wakiziuza kwa Tsh 7000 badala ya Tsh 5000 za halali.

Naomba tff walichukulie suala hili kwa umakini mkubwa kwani linarudisha nyuma maendeleo ya mpira na kuwanufaisha mafisadi wachache wenye matumbo mapana na yasiyojaa katu!
 
Back
Top Bottom