Tiketi haziuziki mechi ya Simba

Franky Samuel

JF-Expert Member
Oct 10, 2018
4,912
12,988
Kuelekea Simba day tiketi za Platinum ziliisha ndani ya siku moja, wiki moja kabla ya tukio. Simba SC ilitangaza tiketi zote zimeisha siku (2) kabla ya Mchezo.

Kuelekea African Football League tiketi za Platinum ziliisha ndani ya siku moja, wiki moja kabla ya tukio.

Michezo ya mwisho ya Simba :

◎ Simba 2 - 2 Al-Ahly Cairo
◎ Al-Ahly Cairo 1 - 1 Simba
◉ Simba 2 - 1 Ihefu
◎ Simba 1 - 5 Yanga
◉ Simba 1 - 1 Namungo

Zikiwa zimesalia saa kadhaa Kuelekea mchezo dhidi ya ASEC Mimosas mpaka sasa tiketi za Platinum ambazo huwa hazizidi (200) hazijaisha ikiwa tiketi zilianza kuuzwa wiki 1+ iliyopita. Hakuna sold out ya eneo lolote mpaka sasa.

Utaratibu wa Simba SC kuonesha graph ya mauzo ya tiketi awamu hii haupo kwa sababu ni tiketi chache sana zilizouzwa kiasi kwamba uongozi wa Simba kupitia kwa Mo Dewji umeamua kushusha bei ya tiketi za mzunguko ambapo ndipo hukaa mashabiki wengi. (Elfu 40) kutoka Tsh elfu (5) hadi elfu (3).

Bila shaka yoyote, hali ikienda hivi Jumamosi watu wataingia bure (Fungulia mbwa).

𝗜𝗻𝗮𝘁𝘂𝗳𝘂𝗻𝗱𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗻𝗶𝗻𝗶?
Hii inatufundisha viongozi, mashabiki na wadau wa soka kuwa, MATOKEO BORA UWANJANI ndio HAMASA kubwa inayoweza kuwaleta Watazamaji uwanjani...

Na sio kitu kingine.

Kutoka mtandao X/TWITTER

20231123_221744.jpg

Kuelekea Simba day tiketi za Platinum ziliisha ndani ya siku moja, wiki moja kabla ya tukio. Simba SC ilitangaza tiketi zote zimeisha siku (2) kabla ya Mchezo.

Kuelekea African Football League tiketi za Platinum ziliisha ndani ya siku moja, wiki moja kabla ya tukio.
Timu imemtimua kocha na imeshindwa kumleta mwingine, upuuzi mtupu
 
Back
Top Bottom