Tigopesa ni kwanini mnatunyanyasa hivyo?

Tigopesa ni kwanini mnatunyanyasa hivyo?

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Hivi nyie Tigo ni sisi ndio tuliwatuma mfanye marekebisho ya tigo pesa? Si nyie mlikuja kwa adabu kutafuta wateja? Naona sasa mnatunyanyasa.
Tangu mfanye marekebisho ya Tigo pesa hamtaki kurudisha pesa zetu.

Iko hivi wadau, nilikosea kutuma pesa bahati mbaya kwa mtu, nikawajulisha Tigo wakaizuia. Sasa ni wiki karibu ya tatu hawataki kurudisha pesa yangu. Ukipiga customer care hakuna cha maana zaidi ya kusema tatizo linashughulikiwa, Tigo shop nao wanasema tatizo linashughulikiwa muda mrefu sasa umepita, mara wanasema nitapigiwa simu toka makao makuu lakini kimya au mnataka rushwa? Semeni.

Jamani tumechoka rudisheni pesa zetu tunazihitaji na nitauacha rasmi mtandao wenu kwa kuwa hamjali wateja wenu.
 
Hivi nyie Tigo ni sisi ndio tuliwatuma mfanye marekebisho ya tigo pesa? Si nyie mlikuja kwa adabu kutafuta wateja? Naona sasa mnatunyanyasa.
Tangu mfanye marekebisho ya Tigo pesa hamtaki kurudisha pesa zetu.
Iko hivi wadau, nilikosea kutuma pesa bahati mbaya kwa mtu, nikawajulisha tigo wakaizuia. Sasa ni wiki karibu ya tatu hawataki kurudisha pesa yangu. Ukipiga customer care hakuna cha maana zaidi ya kusema tatizo linashughulikiwa, tigo shop nao wanasem a tatizo linashughulikiwa muda mrefu sasa umepita, mara wanasema nitapigiwa simu toka makao makuu lakini kimya au mnataka rushwa? Semeni. Jamani tumechoka rudisheni pesa zetu tunazihitaji na nitauacha rasmi mtandao wenu kw a kuwa hamjali wateja wenu.

Na bado hampokei simy za wateja!
 
Wairudisha mkuu,but watakapojicki.
 
Yaan kweli hawa shida! Yalishawahi kunikumba pia kwa kweli wanasumbua sana..
 
Tigo ndio walivyo...mimi nilishawahi kutuma 40k kwa mtu wakasema wameizuia..but hadi leo hawakuirudisha...yapata miezi 8 niliamua kuacha...usumbufu nilioupata sitousahau..
 
Kuna ndugu yangu amekosea kutoa pesa kwa wakala akaweka namba ya wakala wrong, akareport ikazuiliwa tangu tar 16.09.2015 hadi leo hii hajarudishiwa, japo akipiga simu tigo wanamwambia pesa inaonekana ipo ila wrong agent hapokei simu, sijui hawa watu Service Level Agreement (SLA) yao ikoje, hovyo sana.
 
Jambo la msingi ni sisi watumiaji wa Huduma tuwe makini, na pale inapotokea tumekosea tuwe wavumilivu na tusiwe wepesi wa kulaumu wakati sisi wenyewe ndiyo wazembe, huo ndio ukweli. Sasa Mimi ningewashauri muende Tigo makao makuu matatizo yenu yatapatiwa ufumbuzi haraka.
 
Aliyepo Tandahimba ataenda dar kwa ajili ya sh. 10,000 mkuu
 
Jambo la msingi ni sisi watumiaji wa Huduma tuwe makini, na pale inapotokea tumekosea tuwe wavumilivu na tusiwe wepesi wa kulaumu wakati sisi wenyewe ndiyo wazembe, huo ndio ukweli. Sasa Mimi ningewashauri muende Tigo makao makuu matatizo yenu yatapatiwa ufumbuzi haraka.
Tatizo hilo si kwa wanaokosea tu,nilituma pesa kwa mtu msg akaipata lakini pesa haikuingia,akawapigia tigo wakamwambia imerudishwa kwa aliyeituma.
Nimewapigia simu wananiambia itarudishwa kwangu,nimesubiri mpaka Nimechoka nikaenda kwenye ofc zao wakadai wamerudisha zitaingia baada ya 24 hrs,mpaka leo nimeamua kupumzika tu.
 
Nimewahi kupata tatizo hilo watakurudishia tu sema inachukua muda mpaka wajiridhishe kuwa ulituma kwa bahati mbaya kweli kwasababu kumekuwa na utapeli watu wanalipa halafu wanasema wamekosea.vumilia
 
Back
Top Bottom