TIGOPESA NA UBABAISHAJI WATEJA

TIGOPESA NA UBABAISHAJI WATEJA

Mr Sir1

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2018
Posts
1,787
Reaction score
8,123
Juzi Alhamisi saa tisa alfajiri nilifanya malipo ya Azam Tv kupitia tigopesa kwa kiasi cha fedha taslimu Tsh 28,000. Mpaka kunakucha huduma ya TV ilikuwa haijafunguliwa japo nilipata meseji ya ithibati kuwa pesa imekatwa toka kwenye akaunti yangu. Baada ya kuwapigia huduma kwa wateja walikiri kuwa pesa yangu itarejeshwa baada ya masaa 6 (Hiyo ilikuwa saa 2 asubuhi). Mpaka saa 12 jioni hakuna marejesho yaliyofanywa na nikawapigia tena safari hii stori ikabadilika na kudai watarejesha fedha baada ya masaa 12.
Mpaka jana Ijumaa hakuna marejesho yameliyofanywa. Baada ya kuwapigia tena imebadilika na sasa wanadai watarudisha pesa baada ya masaa 72. Huu ubabaishaji ni haki kweli? Kosa langu kama mtumiaji wa huduma liko wapi mpaka nitumikie adhabu yote hii? Na hao wanaopokea simu wana lugha za kebehi kama vile naomba msaada kwa fedha yangu mwenyewe.
Tigo Tanzania mnapaswa kujiangalia upya malalamiko juu yenu yamekithiri. Acheni utapeli wa kijinga.
 
Sio Tigopesa tu. Hata kujua salio la bando walikuwa hawatumi. Nadhani kuna vijana "wajanja" wamesha-hack hiyo system yao ili wachote. Si mmesikia kuna waliokamatwa? Nadhani watu watakaokuwa wamepoteza hela yao kwenye Tigopesa hiyo jana na juzi watakuwa wengi sana na amounts zitakuwa kubwa kubwa
 
Sio Tigopesa tu. Hata kujua salio la bando walikuwa hawatumi. Nadhani kuna vijana "wajanja" wamesha-hack hiyo system yao ili wachote. Si mmesikia kuna waliokamatwa? Nadhani watu watakaokuwa wamepoteza hela yao kwenye Tigopesa hiyo jana na juzi watakuwa wengi sana na amounts zitakuwa kubwa kubwa
Mbaya zaidi hawana lugha rafiki katika kumuelezea mteja. Wanachukulia urahisi tu kushikilia ama kupoteza pesa za watu. Kwangu mimi ni pesa ya king'amuzi kuna baadhi wanatuma pesa za matibabu. Hii ina maanisha wanacheza na uhai wa watu. Baada ya kuwaandikia facebook muda huu wanajibu kirahisi tu kuwa pesa itarudi baada ya masaa 72. Kwanini iwe masaa 72 kwa pesa yangu mwenyewe, hii kwa lugha nyingine wanakopa pesa za watu bila ya ridhaa yao. Kama wameshikilia pesa yangu masaa 72 kisheria inapaswa wanilipe fidia kwa hayo masaa 72.
Kwa kifupi tigo ni wezi.
 
Back
Top Bottom