Tigo_Zantel: Je kampuni ya Zantel imeuzwa kwa tigo?

decomm

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
726
660
Habari wana jamvi?

Laini yangu ya Zantel (simcard), ilikuwa haipati network kwa takribani wiki mbili (maeneo ya Tanga), line ipo kwenye simu inayokubaliwa na TCRA, na simu ilikuwa imewashwa siku zote, wakati huohuo laini nyingine ya kampuni nyingine ya simu ilikuwa ipo hewani kama kawaida.

Kuanzia jana mchana nikaona mnara wa laini ya Zantel kwenye simu umepanda lakini cha ajabu imeandika tiGo_Zantel ilhali katika simu hiyo hakuna laini ya kampuni ya tiGo.

Je kampuni ya Zantel imeuzwa kwa kwa kampuni ya tiGo au nini maana yake?

Mwenye kujuwa hili tafadhali anifahamishe.

Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom