Tigo yawapa wateja wake huduma ya Whatsapp bure

paulivo

Member
Jan 22, 2016
15
2
Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini.

Akitangaza upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez alisema kuwa wateja wote wa Tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.

Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe kwa njia ya simu, ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania na duniani inatumiwa na watu wapatao milioni 900. WhatsApp inawezesha watumiaji kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.

“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia WhatsApp BURE. Hili linawezekana kama mteja ana smartphone.

"Huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wetu inaonesha jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.

Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na kifurushi cha intaneti cha wiki au mwezi ambacho anaweza kukipata kupitia *148*00# à Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.

WhatsApp ni huduma dada na huduma ya Facebook ambayo iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.
 
ubure upo wapi wakati mpaka ujiunge kifurushi cha wiki au cha mwezi

means kama hujajiunga hupati whatsapp bure

Tigo ni wajinga
tigo wanakula hela za watu
tigo wanakata muda wa vifurushi
tigo hawawajali wananchi wa kawaida


USIWE KAMA TIGO
 
ubure upo wapi wakati mpaka ujiunge kifurushi cha wiki au cha mwezi

means kama hujajiunga hupati whatsapp bure

Tigo ni wajinga
tigo wanakula hela za watu
tigo wanakata muda wa vifurushi
tigo hawawajali wananchi wa kawaida


USIWE KAMA TIGO
ukinunua dawa ya meno unapewa mswaki bure.
huna pesa ya kujiunga na vifurushi au una stress??
 
Nimeipenda speed ya halotel kwenye internet. Napenda kuwashauri tigo waboreshe internet. Wachache wanaotaka vya bure
 
Hivi wanaposema huduma ya whatsapp ni bure ina maana hata kama umetumiwa picha za kawaida na pia video za ukubwa wowote kwa whatsapp zitafunguka kama kawaida bila kuwa na gharama yoyote ya ziada ili mradi uwe umejiunga na vifurushi vya wiki/mwezi? Au bure ni kwenye text pekee yake zitakazotumwa kwa njia ya whatsapp?
 
Ninamashaka na uwezo wa kufikiri wa huyo boss wa tigo, anachokisema hakina tofauti na mtu anayekuuzia muhindi halafu anakwambia nimekupa gunzi bure kwa ajili ya kushikilia punje za mahindi unazotafuna
Hahahahaha aisee
 
maaana ya watsap bure iko wapi hapo
Tigo wazushi tu hakuna whatsapp ya bure. Nimejaribu kujiunga na kifurushi cha wiki cha 2,000/= nikapata dakika 22 kupiga mitandao yote, sms 200 na 10 MB. Kweli nimepokea sms, picha na video kwa whatsapp lakini baada ya muda mfupi nikapokea meseji ikionyesha kuwa nimebakiwa na 5 MB. Baada ya muda kidogo tena MB zote kumi zikawa zimeisha. Baada ya hapo ni sms tu ndiyo naweza kupokea kwenye whatsapp huku picha za kawaida au video hata zenye ukubwa mdogo tu zinazotumwa kwangu hazikubali kufunguka na pia siwezi kuzituma kwa wengine.

Inavyoonekana whatsapp ya bure wanayomaanisha hawa Tigo ni hizo 10 MB na hivyo vimeseji unavyoweza kutuma kwa njia ya whatsapp ambavyo sioni kama vina tofauti na sms za kawaida zisizohitaji whatsapp na siyo bure kwenye kutuma picha za kawaida na video.
 
Ninamashaka na uwezo wa kufikiri wa huyo boss wa tigo, anachokisema hakina tofauti na mtu anayekuuzia muhindi halafu anakwambia nimekupa gunzi bure kwa ajili ya kushikilia punje za mahindi unazotafuna

uwiiii asante kwa kuniongezea siku, au amekuuzia shati na vifungo vya bure
 
Back
Top Bottom