Tigo watoa Basi kwa Shule ya Sinza Maalum. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tigo watoa Basi kwa Shule ya Sinza Maalum.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BabuK, Oct 9, 2010.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  SERIKALI imeshauriwa kuongeza juhudi katika kutoa mafunzo, kwa walimu maalumu wa kufundisha watu wenye ulemavu.

  Rai hiyo ilitolea juzi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sinza Maalum,jijini Dar es Salaam, Charles Katage, alipokuwa akipokea msaada wa basi la wanafunzi wa shule hiyo, lilitolewa na Kampuni ya Simu za mikononi ya Tigo.

  "Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, inapaswa kuongeza nguvu katika kutoa mafunzo kwa walimu ambao ni maalumu katika kufundisha watoto wenye mahitaji maalum (walemavu)," alisema Katage.


  Alisema hatua hiyo ni ya muhimu hasa kwa kuzingatia kuwa bila ubunifu wa kufundisha watoto hawa, kazi itakuwa ngumu zaidi.

  Akipokea basi hilo lenye thamani ya Sh106 milioni, Katage alisema kwa muda mrefu sasa, shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na tatizo la usafiri, jambo lililosababisha watoto wengi kushindwa kuhudhuria shuleni.

  Alisema tatizo hilo pia lilisababisha wanafunzi kushindwa kufanya ziara za kimasomo na kwamba kitendo cha Tigo kutoa basi hilo, kimesaidia mno kupunguza ukubwa wa tatizo.
  "Tumekuwa tukishindwa kwenda katika ziara mbalimbali za kielimu kwa sababu ya kukosa usafiri, naona sasa tumepata mkombozi na watoto wetu wamefurahi sana,"alisema Katage.

  Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Benjamini Kulwa, alisema serikali iko katika mchakato wa kuongeza mishahara kwa walimu wanaofundisha watoto walemavu.

  "Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kuwaongezea mshahara walimu wanaofundisha elimu maalumu kwani wana kazi kubwa sana,"alisema Kulwa.
  Ofias Rasilimali Watu wa Tigo, Bennet Kakorozya,alisema msaada huo kwa shule hiyo, unalenga katika kukuza kiwango cha elimu kwa watoto wenye ulemavu.
  Chanzo: Mwananchi
   
 2. K

  Kudadadeki Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa, bus lenyewe aina ya TATA- upatikanaji wa spea na gharama za kumiliki TATA ni TATA kweli kweli. Hiyo shule hawatakuwa na uwezo wa running cost za ilo bus in 6months. Anayebisha, afuatilie hali ya bus hilo by mid 2011. Ni kama VODACOM walivyotoa Bus la model ya ajabu kwa Marie Stoppes Hospital ya Mwenge. Lilitumika miezi kadhaa then parked for good. Lilikuwa pale nje ya mwenge marie stops hospital mpaka majuzi. I hope limeuzwa kama chuma chakavu- scraper...
   
Loading...