TIGO wapingana na taarifa ya TCRA kuwa wao ndio mtandao ghali zaidi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Kampuni hiyo imesema gharama zake zilizonukuliwa kutoka TCRA zimejumuisha kodi ya ongezeko la thamani (Vat) ambayo kwa kampuni nyingine washindani hazijawekwa.

Dar es Salaam. Baada ya taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuonyesha wateja wa Tigo hulipa fedha nyingi zaidi kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi, kampuni hiyo imesema tafsiri iliyotolewa si sahihi.

Akifafanua kuhusu gharama hizo, Ofisa Mkuu wa Ufundi na Mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou alisema wateja wengi wa kampuni hiyo wanatumia vifurushi tofauti vinavyotolewa na kwa mwaka mmoja uliopita wamekuwa wakifanya utafiti wa tabia za wateja kabla ya kubaini hilo. “Zaidi ya asilimia 80 ya wateja wetu wanapendelea kununua vifurushi kuliko kutumia fedha zao kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi wa maneno moja kwa moja. Kwa sababu hiyo, tumeanzisha promosheni ya vifurushi mbalimbali ambavyo vinawapa unafuu wateja kuwasiliana,” alisema Albou.

Kwa maelezo hayo, ina maana takriban wateja milioni 2.2 ambao ni sawa na asilimia 20 ndio wanaolipa gharama za juu kulingana na taarifa ya TCRA, ingawa Albou alisisitiza kwamba kampuni yake imejikita kuboresha huduma na kwamba gharama zao ni rahisi zaidi ndiyo maana wateja wanazikimbilia na kufurahia wakati wote wanapotaka kufanya mawasiliano.

Ripoti ya TCRA kwa robo iliyoishia Septemba inaonyesha wateja wa Tigo hutozwa Sh360 kupiga simu kwenda kwa wenzao wanaotumia mtandao huo kwa dakika moja, hivyo kuufanya kuwa mtandao ghali ikilinganishwa na mingine nchini kwa kuwa tozo hiyo ipo juu ya wastani wa gharama za kupiga simu ambazo ni Sh278 kwa dakika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wateja wa Vodacom wanalipa Sh270 kwa dakika wakifuatiwa na wale wa Halotel wanaolipa Sh228 wakati watumiaji wa Airtel wakilipa Sh219 kwa kila sekunde 60.

Ripoti hiyo inaonyesha wateja wa TTCL, Zantel na Benson ndio wanaolipa gharama ndogo zaidi kuwasiliana, ambapo wale wa TTCL wanatozwa Sh154 kwa kila dakika wakati Zantel ni Sh157 na Benson Sh60 kupiga simu kwa muda huo.

Ripoti hiyo inaonyesha pia kuwa Tigo ni ghali hata kupiga simu kwenda mitandao mingine ambapo hutoza Sh480 kwa dakika wakati wateja wa Airtel hulipa Sh361, ilhali wa Vodacom wakilipa Sh330 na TTCL Sh274. Wale wa Benson hulipa Sh150 wakifuatiwa na wa Halotel wanaolipa Sh228 na Zantel Sh249.
 
tigo hawapo serious kwn mpaka sasa ukifuatilia hata vifurushi vyao vingi ni vya kizushi
 
Tigo wanatapatapa kama mtu anae zama majini.

Huduma zao aghali sana. Hata voda kuna wakati wanazingua.

Mimi nina line za mitandao karibu yote lakini Airtel nawakubali sana. Gharama zao ni chini iwe ndani ya mtandao au kwenda mtandao mwingine. Internet wako vizuri pia.

Halotel mwanzo walikuwa vizuri sana gharama ndogo na mtandao wenye kasi lakini sasa majanga.
Wamepunguza muda na volume ya data bundles, na speed imekuwa mbovu sana.
 
Tigo majizi bundle zao tu majanga ukifungua page utasikia bundle lako limekwisha
 
Sasa njoo kwenye bando linavyoisha kw speed plus vocha kukatwa bila ya taarifa,plus meseji zisizokuwa za msingi na simu zinazopigwa eti usikilize hadithi tamu za mapenzi
I conclude kuwa tigo si tu ni mtandao ghali bali mtandao wa kipuuzi
 
Mbwa anapewa jina baya kwanza then ndio anapigwa risasi;wenye akili tulishaelewa
 
Back
Top Bottom