Tigo wanatuibia mb 500 za kifurushi cha chuo

chija

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
276
65
Mtandao wa tigo umeanza kutuibia mb 500 za kifurushi cha chuo nimejiunga jana eti leo kimeisha wakati Muda mwingi nilikuwa offline
 
Ndugu usije ukasema hivyo wakaviondoa maana wengine ndio huwa tunaponea hapo hapo japo sio wanachuo nadhani hata wewe sio mwanachuo....andika kmya kimya wasije wakasikia maana ile ni ofa tu..
 
Nakubaliana nawe...sio tigo tu.
Hata Halotel...nimejiunga na bundle ya mb 600 mara tatu in two days..imeisha kienyejienyeji tu wakati ni bundle ya wiki....sikua na matumizi makubwa kabisa....ila nilikua nabrowse mambo muhimu na sikua na budi kununua tu ili nimalize shida yangu.
Lakini kwa kweli wizi mwingi.
 
Mie niliwahi kuibiwa 1GB na Voda, yaani nimejiunga ikaja Meseji nimefanikiwa kujiunga dakika 150, SMS bila kikomo na 1GB kutumia wiki nzima kisha nikawasha data nashangaa sipati internet.

Nikadhani labda tatizo la mtandao nikajaribu baada ya robo saa kimya. Nikachukua simu ya my dear lara1 kucheki anabrows tu bila shida yeyote. Basi nikapiga *149*60# kujua Salio. Hee nikakuta nina dk 150, SMS bila kikomo na 0MB!

Wiki nzima Vodacom wanaishia kuniambia kifurushi kinarudishwa Wateja ni wengi mno. Sasa nikajiuliza Kama mie tuu sijarudishiwa je ni wangapi hawajarudishiwa na wizi huu tuvumilie hadi lini?

Ila mtoa mada achana na 0713 bora Voda hivyo hivyo hata Kama saa nyingine wanakwiba.
 
Kha! hata hallotel kaja jana tyr nae ameshaaza UJAMBAZI kweli Tz. ni shamba la bibi! ila hii inawezekana kutokana na USULTANI wa TCRA! hawa watu hakuna wanachokifanya! Ama wanapewa share au 'wanalipwa' na hawa wenye makampuni ya simu sio bure!
 
Mtoa uzi kumbuka kwmb hicho kifurushi cha Chuo ni kifurushi cha upendeleo tu so ukilalamika wakakitoa utaniudhi mpaka mimi.
Kifurushi bomba sana kile japo mi bado nipo secondary.
 
Mtoa uzi kumbuka kwmb hicho kifurushi cha Chuo ni kifurushi cha upendeleo tu so ukilalamika wakakitoa utaniudhi mpaka mimi.
Kifurushi bomba sana kile japo mi bado nipo secondary.
Na utakuta mtoa Uzi na yeye huwa anaenda (anaendaga) karibu na vyuo kujiunga tuu kumbe si mwanachuo Kama mie vile.
 
Mtandao wa tigo umeanza kutuibia mb 500 za kifurushi cha chuo nimejiunga jana eti leo kimeisha wakati Muda mwingi nilikuwa offline
mkuu unasoma chuo gan
koz gan
mkuu wa chuo anaitwaje
upo kitivo gan
dean wako ni nani
vese president ni nani

usije ukawa jitu la mtaan tu
 
Ndugu usije ukasema hivyo wakaviondoa maana wengine ndio huwa tunaponea hapo hapo japo sio wanachuo nadhani hata wewe sio mwanachuo....andika kmya kimya wasije wakasikia maana ile ni ofa tu..

Mtoa uzi kumbuka kwmb hicho kifurushi cha Chuo ni kifurushi cha upendeleo tu so ukilalamika wakakitoa utaniudhi mpaka mimi.
Kifurushi bomba sana kile japo mi bado nipo secondary.

Na utakuta mtoa Uzi na yeye huwa anaenda (anaendaga) karibu na vyuo kujiunga tuu kumbe si mwanachuo Kama mie vile.
Nimecheka sanaaa yani sikutegemea kabisa kucheka hivi
 
Back
Top Bottom