Kheri ya ijumaa kuu kwa wote.
Siku ya tareh 23 mwezi wa 3,nilifanya malipo kwa njia ya mtandao nililipa ticket ya buss dar to mwanza.
Malipo yangu hayakufanikiwa nikawasiriana na huduma kwa wateja wakaniambia kunatatizo la kimtandao kwahiyo fedha zangu zitarudishwa baada ya siku 3.
Kila baada ya siku tatu nikawa nawakumbusha ikaanza story ya masaa 24 nitarudishiwa changu,nikaona niende makao makuu makumbusho nikaambiwa wamesha chukua taarifa zangu hivyo nitarudishiwa baada ya masaa 24.
Nimekaa siku 2 nimewapigia wanasema mbona huku tumeshakuludishia? Jaman jaman jaman TIGO wamekuwa na huduma mbovu mbovu mnooo.
Nikarudi Tena makao makuu wakaniambia niwawie radhi pesa yangu Bado inaonekana ipo kwao nikae baada ya siku 3 itakuwa mikononi mwangu.juzi juma 5 nikawapigia kuuliza Mana siku 3 zimekata nikaambiwa masaa 24 nisubili nikabakia kucheka tu.leo nawapigia simu kwa number Yao ya 100 inapokelewa ila upande wangu si sikii chochote wamenipiga "MUTE" maana nikitumia simu ya mtu mwingine wanapatikana vizuli tu.
Wakuu nahitaji changu jasho langu sio vyema likapotea ki rahisi rahisi.